Ukweli wangu umeniponza, najuta

Ukweli wangu umeniponza, najuta

comfix

Member
Joined
Feb 15, 2014
Posts
59
Reaction score
11
Takriban wiki moja imepita tangu nilipofanya mazungumzo na mke wangu, nilidiriki kumweleza ukweli kuwa kwa kipindi kirefu nilikuwa natoka nje ya ndoa, na hivyo nikamwomba anisamehe na kuwa najutia nakumwahidi kuwa sintofanya hivyo tena kwani hakuna nilichokipata.

Baada ya mazungumzo yetu alionyesha kuniunga mkono kwa kunionyesha upendo wa dhati na mimi pia hali kadhalika.

Sasa kilichonichanganya namwona mke wangu kanichenjia hataki kuongea na mimi kila kitu anatuma mtoto, nimwulizapo kulikoni? kimya sijibiwi, kibaya zaidi hataki nimguse ukizingatia kuwa wanandoa ndiyo huwa njia yetu pekee ya kutatua na kuondoa tofauti zilizopo, hakuna amani Nifanye nini sasa wadau?
 
^^
Mpe muda, aweke vema taarifa uliyompa akilini mwake. Jitahidi sana kuonyesha majuto kwa yaliyopita ili akipata jibu huko anakowaza,uwe uamuzi wa kheri na si kisasi cha kimya kimya
^^
 
Kulikua na haja gani ya kumwambia ulikua unachepuka? Ningekua mimi ningekutema kabisa. Halafu unataka umguse ili umuambukize magonjwa?? Mkapime kwanza
 
Hongera kwa kua mkweli kwa mke wako...Truth and honesty is always good for any relationship. Ni kipindi tu anacho deal na maumivu ya ukweli huo, just let her heal ila uendelee kua karibu na kumuonyesha kuwa u meant what you said kwa matendo pia. Show her the reason why you chose her
 
Aisee! Mdomo unaponza kaka..... Hebu ichunguze kolomeo yako kuna sehem pana nundu hyo anayo mwanaume tu na sio mwanamke.... Hapo ndio siri za mwanaume zpo. Meza mdeki mtoto wa kiume sio unakatikiwa kiuno vizur unaanza kuropoka.
 
Takriban wiki moja imepita tangu nilipofanya mazungumzo na mke wangu, nilidiriki kumweleza ukweli kuwa kwa kipindi kirefu nilikuwa natoka nje ya ndoa, na hivyo nikamwomba anisamehe na kuwa najutia nakumwahidi kuwa sintofanya hivyo tena kwani hakuna nilichokipata. Baada ya mazungumzo yetu alionyesha kuniunga mkono kwa kunionyesha upendo wa dhati na mimi pia hali kadhalika. Sasa kilichonichanganya namwona mke wangu kanichenjia hataki kuongea na mimi kila kitu anatuma mtoto, nimwulizapo kulikoni? kimya sijibiwi, kibaya zaidi hataki nimguse ukizingatia kuwa wanandoa ndiyo huwa njia yetu pekee ya kutatua na kuondoa tofauti zilizopo, hakuna amani Nifanye nini sasa wadau?

Mkubwa, kwani kulikuwa kuna ulazima gani uliokufanya umwambie mambo kama hayo?? Kama uliweza kuyafanya kwa kujificha mpaka ulipoamua kumwambia mwenyewe pasina kugundulika basi ni wazi anajiuliza atajiamini vipi kuwa sasa ni kweli umetulia??

Hapo tumia uanaume wako kuweza kuyamaliza, ni kazi rahisi ukiwa makini ikizingatiwa kuwa hawa viumbe ni wetu hawa na Mungu alituumbia siye sema tuwache kuwa-misuse tu!
 
Mpe muda na ongeza mapenzi ja muda wa kukaa naye au kumtoa out pale unapapopata nafasi.
If necessary nenda naye mkapime afya atarudi kwenye hali ya kawaida pole na hongera.
 
Wewe zidisha kumpenda na kumwonesha mapenzi ya kweli zaidi ya siku za nyuma atajirudi tuu.
 
Takriban wiki moja imepita tangu nilipofanya mazungumzo na mke wangu, nilidiriki kumweleza ukweli kuwa kwa kipindi kirefu nilikuwa natoka nje ya ndoa, na hivyo nikamwomba anisamehe na kuwa najutia nakumwahidi kuwa sintofanya hivyo tena kwani hakuna nilichokipata. Baada ya mazungumzo yetu alionyesha kuniunga mkono kwa kunionyesha upendo wa dhati na mimi pia hali kadhalika. Sasa kilichonichanganya namwona mke wangu kanichenjia hataki kuongea na mimi kila kitu anatuma mtoto, nimwulizapo kulikoni? kimya sijibiwi, kibaya zaidi hataki nimguse ukizingatia kuwa wanandoa ndiyo huwa njia yetu pekee ya kutatua na kuondoa tofauti zilizopo, hakuna amani Nifanye nini sasa wadau?
Ulikuwa mkweli kupitiliza ungeomba ushauri kwanza kabla hujakiri makosa yako wenzako tunanaswa na vidhibiti kabisa na bado tunagoma kukiri ukweli. Tunashikiwa mpaka visu na misahafu lakini nikishasema SiKWELI hakuna kinachobadilisha huo msimamo
Zingatia si kila ukweli ni wa kusema
 
We nae kwa nini ukubali?si ungejitahidi kuyamaliza polepole bila kusema ukweli.chunga ulimi
 
Heheeeh! Unalo hilo!! Kila siku munaambiwa acheni michupuko mubaki njia kuu hamutaki! WANAWAKE nao siku hizi wanayo michepuko!!
 
Mkeo hakuamini tena. Maswali anajiuliza kama uliweza kumcheat hapo mwanzo na hakuona dalili zozote basi unaweza ukamcheat tena na wala asigundue lolote. Unapaswa kumpa sababu mpya za kukuamini. Badili mfumo wa maisha kwa kuleta taratibu mpya. Jitahidi kuwahi kurudi nyumbani na ikiwezekana unaweza ukawa unarudi na vijizawadi vidogo unavyohisi anavipenda. Muombe mtoke out kila unapopata nafasi. Hutakiwi kumlaumu pindi apokuchukia mfanye aamini unatambua maumivu yake ila msamaha wake bado ni muhimu kwako. Muonyeshe mlango wa kuelekea maisha mapya na mkabidhi funguo aufungue mlango huo, sidhani kama atakataa......... KUDADEKI ZAKO SIKU NYINGINE USIRUDIE KUTOA SIRI ZA KAMBI KWA SHEMEJE!
 
*************************************
Hivi,what if yeye ndo angekupasha hiyo habari? Unge-react vipi mkuu?

Mpe muda atafakari hatima ya mahusiano yenu.
 
Mkuu endelea kumbembeleza usiache ,nikupongeze tu kwa kurudi kwenye ndoa yako,ila wanawake karibia wengi tunakitu kinaitwa KISASI kwa njia yoyote ile(simaanishi kutoka nje japo wapo wanaofanya hivyo),so ,ni wanawake wachache sana na werevu ndio wanaweza kushindana na hili,hivyo ni wakati wake sasa kulipiza kwanjia hiyo aliyoichagua (na usipokuwa makini hapa waweza chapiwa mchana kweupe wajiona),nakushauri endelea kumuelimisha na zidi kumuonesha upendo... mwisho USIRUDIE TENA KUMSALITI MKEO inauma we hujui tu !
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom