Ukweli wa Japan kusogeza masaa mbele

Ukweli wa Japan kusogeza masaa mbele

ashidodi

JF-Expert Member
Joined
Sep 4, 2016
Posts
292
Reaction score
342
Habari za majukumu ndugu wana JF, poleni na mihangaiko ya hapa na pale....
Niende mojakwamoja, nimepata taarifa kuwa nchi ya JAPAN italazimika kusogeza MASAA mawili (2) MBELE kutokana na nchi hiyo kukumbwa na JOTO KALI. Masaa hayo husogezwa vipi na inasaidiaje kupunguza JOTO? Naomba msaada kwa mwenye uelewa was hili
Asanyeni sana
 
Ukisikia yajayo yanafurahisha ndo hii moja wapo kusogeza mda mbele
 
Kutasababisha muda wa kazi kuanza kucheleawa, na wafanyakazi watalazimika muda wa joto kuwa nyumbani.
Itaongeza ufanisi kazini
Kwahiyo unamaanisha kama kazi inaanza sa2 itatakiwa ianze sa4?
 
Mimi najua kila jumapili ya mwezi wa 3 uingereza huwa wanapeleka mbele saa moja
Ina maana ndio summer time inaanza
Mchana unakuwa mwingi

Na inapofika jumapili ya mwisho wa mwezi October inarudishwa saa moja nyuma
Kuashiria kuwa winter imeanza na usiku unakuwa mrefu.

Inaweza kuwa wanafuata system ya huku
Maana miezi hii jua linazama saa 3:30 usiku UK
 
Wabatumia remote ya startimes kufanya hayo yote
 
Google hili neno 'daylight saving'. Natumai litakupa muangaza
Asante sana nimeelewa sasa, kumbe ni nchi nyingi sana hufanya hivo inapotokea jua lina chelewa kuzama au kuwahi kuchomoza kabla ya muda wa kawaida, hili zoez lilianza miaka 100 iliyopita na kwa mara ya kwanza Canada ndio walianza na nchi zingine zikafatia, hii inahusu nchi ambazo jua huwa linaonekana kwa mda mfupi tu, yaani halihusishi nchi zilizo karibu na IKWETA sababu nchi hizo hupatwa jua kawaida kabisa. Asante
IMG_20180807_081915_292.jpg
 
Mimi najua kila jumapili ya mwezi wa 3 uingereza huwa wanapeleka mbele saa moja
Ina maana ndio summer time inaanza
Mchana unakuwa mwingi

Na inapofika jumapili ya mwisho wa mwezi October inarudishwa saa moja nyuma
Kuashiria kuwa winter imeanza na usiku unakuwa mrefu.

Inaweza kuwa wanafuata system ya huku
Maana miezi hii jua linazama saa 3:30 usiku UK
Yawezekana
 
Back
Top Bottom