Ukweli vurugu Mbagala si dini bali ujinga na umaskini | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ukweli vurugu Mbagala si dini bali ujinga na umaskini

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Father of All, Oct 14, 2012.

 1. Father of All

  Father of All JF-Expert Member

  #1
  Oct 14, 2012
  Joined: Feb 26, 2012
  Messages: 3,093
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  [h=3][/h]

  [​IMG] Ukichunguza kilichotokea Mbagala hivi karibuni ambapo makanisa yalichomwa moto na wahuni waliojiita waislam, unagundua kuwa kumbe kilichosababisha vurugu si kitendo cha mtoto kunajisi Korani bali chuki, ujinga, husuda na kukata tamaa. Kilichotokea Mbagala ambapo watoto wajinga wawili walibishania juu nguvu za imani zao kingetokea Masaki wala hakuna ambaye angepoteza muda.

  Hata mahuburi ya kijinga yanayofanywa na watu kama Ponda Issa Ponda huwa hayapenyi Masaki. Mikocheni, Kunduchi na maeneo mengi ya wenye nazo. Hivyo tatizo kubwa tulilokuwa nalo ni kuwa na watu wengi wajinga na maskini waliokata tamaa kiasi cha kuweza kutumia kisingizio chochote kuonyesha hasira zao. Hii huitwa venting kitaalamu ambapo mwenye hasira hutafutia sehemu ya kuzitolea au kuzitapika.

  Wenye kusoma na kufahamu dini watanikosoa. Hata kama hicho kilichotokea kingetokea wakati wa mtume Mohammad asingeamuru upuuzi kama ulioshuhudiwa Mbagala. Nani mara hii kasahau jirani yake Mohammad aliyekuwa akijisaidia njiani mwake ili kumuudhi kila kukicha hadi siku alipoungua akashindwa kufanya hivyo na Mohammad akamwombea na akapona na kusilimu? Tuhitimishe kwa kusema wazi kuwa vurugu za Mbagala zilivikwa udini lakini ukweli ni vurugu za kijinga na kimaskini.
   
 2. Jackbauer

  Jackbauer JF-Expert Member

  #2
  Oct 14, 2012
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 5,920
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  tusidanganyane eti waliofanya haya ni wajinga na wahuni wa mataani,si kweli...

  nenda kwenye shule za sekondari za bweni,nenda vyuoni,nenda makazini halafu pitia na hapa JF utaona dhahiri kuna vimelea vya chuki za kidini.lazima tukubali kuwa tatizo lipo ili tuweze kulitatua
   
 3. Aleyn

  Aleyn JF-Expert Member

  #3
  Oct 14, 2012
  Joined: Nov 12, 2011
  Messages: 10,228
  Likes Received: 13,680
  Trophy Points: 280
  Mimi nimekuja kwa jina la Baba yangu, wala ninyi
  hamnipokei; mwingine akija kwa jina lake
  mwenyewe, mtampokea huyo. YOHANE 5:43.
  Pia tusome Mathayo 5:11-12 Heri ninyi
  watakapowashutu mu na kuwaudhi na
  kuwanenea kila neno baya kwa uongo, kwa ajili
  yangu. Furahini, na kushangilia, kwa kuwa
  thawabu yenu ni kubwa mbinguni. Kwa maana
  ndivyo walivyowaudhi manabii kabla yenu
   
 4. mwakaboko

  mwakaboko JF-Expert Member

  #4
  Oct 14, 2012
  Joined: Sep 17, 2010
  Messages: 1,841
  Likes Received: 255
  Trophy Points: 180
  Tatizo lilianza pale kundi fulani la KIISLAM lilipoanza kuzunguka nchi nzima wakimlaani MWL.NYERERE, bila kuchukuliwa hatua zozote naona matokeo ya laana ya kulaani visivyolaaniwa yameanza kuonekana sasa, WALIFANYA HIVYO WAKIDHANI WANAWEZA KUMUONDOA MWL. KTK mioyo ya WATZ, sasa wameanza kumkumbuka kwa mazuri yake, kumbuka ukitoa laana kwa asiye na hatia hiyo laana inawarudia.

  Laana iwafikie wale wote wanaowadhulumu wasio na hatia. NO CRIME GOES UNPUNISHED,
  kinachouzi ni pale watu wazima wanapofanya mambo ya kipuuzi, LEO HII UKIWAULIZA WALE WALIOSHIRIKI KUHARIBU, KUIBA, KUCHOMA MAKANISA KWANINI WAMEFANYA YALE WALIYOFANYA SIJUI KAMA WANA MAJIBU YANAYOELEWEKA KWA WENYE AKILI .

  Watu wazima wanaingilia mabishano ya watoto, kama sio laana ni nini?
  Halafu wanaiba vifaa kanisani na kuchoma moto, ndivyo walivyofundishwa na mungu wao?
  nani aliwaambia kuwa yule mtoto amejificha kanisani kama sio kanisani walifuata nini?
  na kwanini waibe?
  wanafanya hivyo kwa maslahi ya nani?
  na wananufaika vipi wakichoma makanisa?
  waliagizwa na nani kwenda kuchoma makanisa?
  na kwanini hawakuendelea kupambana na polisi ili kumtoa waliyemtaka?
  huo ujasiri wa kushambulia makanisa wamepewa nani?
  ili iweje?
  walipwa na nani?
  ni nani aliwaambia kuwa kosa la mtoto huyo, adhabu yake ni capital punishment?
  nani iliidhinisha hiyo hukumu kwa maslahi ya nani?

  MUSLIMS wajue kuwa makanisa wanayaharibu yamejengwa na WATZ wenzao kwa nguvu zao sio msaada kutoka SAUDIA, IRAN, KUWAIT

  NI UJINGA KUMSHAMBULIA mtu kwa kosa la kitoto kama hili
   
 5. Inanambo

  Inanambo JF-Expert Member

  #5
  Oct 14, 2012
  Joined: Jun 26, 2011
  Messages: 2,864
  Likes Received: 1,148
  Trophy Points: 280
  piga ua hii ni Imani ya Dini yao tu coz husema Takbir Ala Akba wanapofanya Fujo. Maskini hata sisi tunao lakini hatajawaSocialised hivyo
   
 6. m

  mgomba101 JF-Expert Member

  #6
  Oct 14, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 1,788
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  mbali kuchoma moto makanisa wanaiba divai,ekaristi takatifu! mamburula hao elimu dunia imewapiga chenga.
   
 7. KISHOKA_ZUMBU

  KISHOKA_ZUMBU Senior Member

  #7
  Oct 14, 2012
  Joined: Apr 4, 2012
  Messages: 163
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 45
  udini upo sana hapa tanzania, ingawa tunajaribu kusema udini haupo na kuukemea lakini upo. viongozi wasipochukua hatua za makusudi kutambua uwepo wake na kutafuta suluhu ya kudumu, kuna siku kutatokea tatizo kubwa zaidi.
   
 8. Shark

  Shark JF-Expert Member

  #8
  Oct 14, 2012
  Joined: Jan 25, 2010
  Messages: 20,080
  Likes Received: 7,306
  Trophy Points: 280
  Mkuu Father of All umeongea jambo la msingi sana. Ukichunguza hili jambo critically kwa jicho la tatu ndipo utagundua chanzo cha haya yanayotokea sasa.

  Nakubaliana na wewe Sheikh Ponda hana nguvu kubwa Masaki, Oysterbay, Mikocheni maana huko wanakaa walio nazo.

  Uislamu unaweza ukawa umehusika lakini unapata nguvu na umaskini + ukosefu wa elimu. Nikisema katika watanzania tuliopo leo hii, Wasomi wa kikristo ni wengi kuliko waislam hakuna atakaebisha. Na hata nikisema wananchi wenye unafuu wa kimaisha wa kikristo ni wengi kuliko waislamu sintopata upinzani pia.

  Historia inatuonyesha kua waislamu tumekua nyuma kiuchumi na kielimu ( labda pia kisiasa) kwa muda mrefu sana, na hili linapelekea kudhani (labda kweli) kua kuna mkakati mahsusi uliopelekea haya.
   
 9. Cheche Mtungi

  Cheche Mtungi JF-Expert Member

  #9
  Oct 14, 2012
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 2,487
  Likes Received: 148
  Trophy Points: 160
  Unamuona Vasco hapo?ni kama anacheka vile,hana jipya kimoyomoyo anafurahia NA KUCHEKA!
   
 10. E

  Emmanuel_mtui Member

  #10
  Oct 14, 2012
  Joined: Apr 10, 2012
  Messages: 56
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Wanaharakati wote na wote wanaokubali ukweli hata kama hawapendi watakubaliana na mimi kuwa yaliyotokea mbagala dar tanzania ni mambo ya kutengenezwa na baadhi ya watu kwa labda kwa uelewa wao mdogo au kwa imani ya tamaa fulani fulani. Kwani kwa watanzania wa leo huwezi kuniambia eti tukio lile lingeweza kuwa na wahusilka wengi kwa kiasi hicho eti kwa tukio lisilotarajiwa. WATANZANIA AMKENI AMANI YETU NI MUHIMU ZAIDI YA UJINGA NA TAMAA ZA HAO WACHACHE WANAOJITAFUTIA UMAARUFU KWA MAKUNDI.
   
 11. m

  matubara JF-Expert Member

  #11
  Oct 14, 2012
  Joined: Jul 25, 2012
  Messages: 226
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Ujinga,umasikini na uchoyo ndio kitu kinachowasumbua ndugu zetu waislam. Waislamu ni wazito mno kuchangia hata kwenye taasisi zao wenyewe! Mfano mzuri ni msikiti walimotokea wale waliofanya hizo fujo-uko choka mbaya! Na waone jinsi wakristu watakavyochanga mamilioni fasta kukarabati uharibifu uliofanyika! Hapa Tanzani waislamu ni matajiri kuliko wakristo huku wakristo wengi wakiwa wamesoma kuliko waislamu,lakini je waislamu wanatumiaje utajiri wao hata kwa manufaa yao wenyewe? Jibu wanalo!
   
 12. N

  Ndjabu Da Dude JF-Expert Member

  #12
  Oct 14, 2012
  Joined: Aug 29, 2008
  Messages: 3,648
  Likes Received: 408
  Trophy Points: 180
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 13. a

  adolay JF-Expert Member

  #13
  Oct 14, 2012
  Joined: Dec 8, 2011
  Messages: 7,567
  Likes Received: 3,026
  Trophy Points: 280
  Baba wa wote.

  Umasikini na elimu inaweza kuwa sababu hapa kwetu tanzania lakini kwa asilimia kidogo sana.

  Inchini Irani ukijifanya kuhubiri ukristo roho yako iko mashakani

  Saudi arabia yaleyale

  Syria kama kawaida

  Bado father nahitaji kuwekwa sawa huko kote chuki kwa imani ya kikristu inasababishwa na umaskini?

  Kilichofanyika nimfumo wa maisha wa wenzetu. nimeishi Tanga kwa miaka mitano lakini simulizi nilizokuwa nazipata vijiweni zinatisha, nilibahatika kwa mda mrefu kupata simulizi mbalimbali kwasababu iliwachukua miaka mitatu kuitambua imani yangu kwasababu jina langu ni miongoni mwa majina yanayotumika kotekote na waliamini nipo upande wao japokuwa swala tano sikupatikana.

  Kama ni umasikini mbona wasimalizie hasira zao pale polisi

  Je kugomea sensa kwa ushawishi wa ponda pia umasikini?

  Je Kule zanzibar makanisa yaliyochomwa mfululizo mpaka kufikia zaidi ya ishirini ni umasikini?

  Ni umaskini gani huo wasioenda kuvamia benki kuu kuliko na fedha! wamebaki kuvamia na kuharibu makanisa?

  Father of all, kunatatizo kubwa tena sana la kiimani kiasi kwamba watu wanakuwa saturated kiakili kutokana na mahubiri ya kichochezi yakiwa na malengo maalumu nyuma ya pazia kimkakati. watbisha na kukanusha huo ndiyo ukweli.
   
 14. H

  Haika JF-Expert Member

  #14
  Oct 14, 2012
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 2,318
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 145
  ujinga umasikini, ukosefu ya hisia ya kupata haki iliyojengeka,
  sanasana UJINGA kuanzia wazazi hadi watoto wetu.

  mimijapo sijaelimika sana, lakini bado siwezi kuenda msikitini kufanya fujo, hali kadhalika huyu rafiki yangu muslamu hapa jirani najua na pia naweza muapia kuwa hawezi kufanya hivyo,

  haya matendo yanachochewa na ujinga,wenye nazo wanatumia wajinga,

  Tutvuna wote matunda ya kuacha shule zikae na watoto bila kuwapa elimu, kuharibu shule za ufundi ambazo walitoka watoto wengi wakiwa tayari kufanya kazi, sasa muda wa mavuno unakaribia,

  tuliambiwa na yule mwanamuziki, kama unadhani elimu ni gharama jaribu ujinga.
  serikali iliona ni gharama kusomesha watoto, sasa wote tutaanza kuona gharama ya ujinga.
  Watakuja waislamu watawashauri vijana wetu wainige mtaani na wataingia,
  watakuja wahubiri mahiri na watawashauri wamama na vijana kupigania haki yao, utatuona barabarani,
  si muda mrefu.
  ila tunaweza badili kwa kuelimisha kizazi kijacho kazi, kama msingi wa heshima na utu wa mtu
   
 15. Father of All

  Father of All JF-Expert Member

  #15
  Oct 14, 2012
  Joined: Feb 26, 2012
  Messages: 3,093
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Adolay you are dead right. Ila ninachoweza kukushauri mwanangu ni to narrow your thesis. Kama utasoma vizuri text nimeongelea Mbagala. Ili kuondoa utata nimejaribu kuleta mifano ya Masaki. Hivyo tunaongelea tukio la Mbagala na si perception ya waislam all over the globe. Nadhani mwanangu umenielewa.
   
 16. Father of All

  Father of All JF-Expert Member

  #16
  Oct 14, 2012
  Joined: Feb 26, 2012
  Messages: 3,093
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Huyo mama anayelia ni mnafiki sijawahi kuona. Linalia eti msahafu umekojolewa. Ila mijitu inavyozini na kuiba haioni kama ni kudhalilisha kazi ya mwenyezi Mungu ambaye amuumba mwili huo. Tunakwenda wapi kama tunashindwa kutafsiri vitu rahisi? Hivi kitabu na mwili wa binadamu nani zaidi? Korani ni bidaa kwa uislam kwa vile Muhamad hakuiacha.
   
 17. Father of All

  Father of All JF-Expert Member

  #17
  Oct 14, 2012
  Joined: Feb 26, 2012
  Messages: 3,093
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Sheikh Ahadi amemaliza kila kitu. Laiti wengi wangekuwa na welewa kama huu tusingefika hapa.
   
 18. a

  adolay JF-Expert Member

  #18
  Oct 14, 2012
  Joined: Dec 8, 2011
  Messages: 7,567
  Likes Received: 3,026
  Trophy Points: 280

  Sasa father of all mbona tunakazi ngumu, naiona hatari kubwa mbele yetu

  mipango na mikakati imeshaandaliwa, fedha za mafuta zipo kutuchonganisha.

  Watanzania wengi wanaumasikini wakutisha, wenyefedha wataendelea kutununua na kutushawishi kufanya fujo kila siku?

  Serikali ilipaswa kukemea na kusimamia sheria na taratibu kwa faida ya vizazi vya sasa na vizazi vya hapo badae.

  Redio zinachochea, magazeti yanachochea na akinaponda usiseme kama suala ni umasikini na serikali bado imelala fofofo

  tumekwisha.
   
 19. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #19
  Oct 14, 2012
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,312
  Likes Received: 5,600
  Trophy Points: 280
  Ni umasikini,no hope society,elimu duni ,mazingira duni,fikra potofu,wengi wamejazana sehemu ambazo zimesongamana hata huduma za jamii sasa imekuwa ngumu...mbagala kumesongamana sana sana kuna idadi kubwa sana ya masikini na kipato duni,fikra hakuna,wengi sana sana fanya utafiti
   
 20. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #20
  Oct 14, 2012
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,324
  Likes Received: 19,491
  Trophy Points: 280
  ni wivu wa kike
   
Loading...