Ukweli utakuweka huru: Dawa ya Zanzibar ni Rais Magufuli kukubali kufanya kazi na Maalim Seif

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,814
34,196
PIC+UKWELI.jpg

Rais Magufuli akisalimiana na Maalim Seif Ikulu .


Kwa kawaida katika maisha ya kila siku kiburi na jeuri havimsaidii mwanadamu. Nimesoma kwenye magazeti habari inayogusa maisha ya Watanzania wengi.


Habari hii ni ile inayohusu misaada ya fedha kutoka Marekani kwenye Mfuko wa Changamoto za Milenia (MCC) ambazo Tanzania inastahili kupata kwa ajili ya maendeleo ya wananchi wake maskini.

Ni habari ya kushtua na kusikitisha kwa Taifa changa kama Tanzania. Njiapanda hii inatokana na suala la matokeo ya Uchaguzi Mkuu uliofanyika Oktoba 2015, mwaka huu inadaiwa kwamba Katibu Mkuu wa CUF, Maalimu Seif Shariff Hamad ameshinda uchaguzi huo.

Kama ni kweli kashinda, kwa nini hatangazwi na nchi yetu inaendeshwa kwa demokrasia ya kweli na utawala bora?

Nchi za Ulaya, Marekani na zingine zimeonya kuendelea kufanyia suala hilo mchezo wa kuigiza kwani linaweza kukiingiza kisiwa hicho katika machafuko na hata yakasambaa Tanzania Bara. Inaonekana kumekuwa na vikao vingi vya kutafauta mwafaka ambao kwangu hauna maana, mwafaka hapa ni kumtangaza aliyeshinda, kuna majadiliano gani tena hapo? Katika uchaguzi majadiliano yanafanyika kupitia sanduku la kura na sauti ya wengi lazima isikilizwe.

Watazamaji na wasimamizi wa kimataifa na wa ndani walisema uchaguzi nchini ulikuwa huru na haki. Sasa kasoro hizi zinazoletwa na Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) zilisababishwa na nani? Hadi leo hakuna mtu aliyejitokea kujibu swali hio, hata mwenyekiti wa ZEC, Jecha Salim Jecha ameshindwa kujitokeza mbele ya Taifa na kutoa majibu ya maswali magumu waliyonayo wananchi.

Kwa nini Marekani na nchi za Ulaya, wanang?ang?ania kutangazwa kwa mshindi katika uchaguzi huo wa kihistoria? Ni kwa sababu wao wanajaribu kufuata sauti za sanduku la kura, hata kama kulikuwa na tatizo kwenye matokeo, lakini siyo kwa kiwango hicho.

Wao kama wadau wa maendeleo ya Tanzania na Zanzibar wataendelea vipi kuunga mkono ukandamizaji wa demokrasia wa kiwango hicho? Wananchi wao wanaotoa kodi ambazo zinaletwa huku watawauliza inakuwaje ?mnasapoti? Serikali isiyoheshimu utawala wa kidemokrasia.

Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) isifikiri hili ni jambo dogo linaloihusu Tanzania pekee, bali linahusu dunia nzima. Ni kujidanganya kwamba mambo yanayofanyika Tanzania huko nje yatakuwa yamefichika, tunaishi kwenye kijiji kidogo ambamo watu wote wanajuana. Ulimwengu wa teknolojia na utawandawazi unadai uwazi na ukweli ili uweze kuendelea kuishi na kuwa sehemu ya kijiji hiki. Hivyo wananchi wengi wanajiuliza jeuri ya kutaka kupindisha matokeo ya Uchaguzi Mkuu wa Zanzibar inatoka wapi?

Wakati Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inahubiri amani, inasikitisha kuona kwamba yenyewe haitendi vitu vya amani. Amani ya Zanzibar ikipote hivi wa kulaumiwa watakuwa CUF, CCM au SMZ? Ili kunusuru sintofahamu hiyo, ushauri wangu kwa Rais John Magufuli ni kuwashawishi CCM wenzake ili wakubaliane na Maalim Seif atangazwe mshindi wafanye naye kazi.

Hatukatai kwamba kuna hofu upande wa CCM na hata wananchi wa kawaida, halikadhalika baadhi ya viongozi wa dini hasa za Kikristo wenye mawazo kwamba CUF ikichukua madaraka Zanzibari itakuwa dola ya Kiislamu. Jambo hili litawezekana vipi wakati visiwa hivyo ni sehemu ya Muungano wa Tanzania?

Hapa ndipo tunapohitaji makubaliano jinsi ya kuiendesha Serikali ya Muungano kati ya CUF na CCM, lakini sidhani kama mwafaka wa nani kashinda na nani kashindwa utazaa matunda yoyote.

Tumwache mshindi atangazwe halafu yatafutwe makubaliano, kama CUF wanaweza kuwa washirika wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar chini ya Dk Ali Mohamed Shein, nao CCM wanaweza kuwa washirika wa CUF, ndiyo maana inaitwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa.

Mwenye jawabu na dawa ya hali tete ya Zanzibar ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk Magufuli. Ni yeye kwa sasa ambaye anafaa kuingilia kati ili mwafaka wa kulinda na kuendeleza amani upatikane.

Tumwombe Mungu ili Roho Mtakatifu amwangazie na ampe unyenyekevu Rais Magufuli ili atatue tatizo hili ambalo Desemba 28 litatimiza miezi miwili.

Tunapokaribia kusherehekea Sikukuu ya Krismasi na Mwaka Mpya kama Rais anavyosema tumwombee na tumtangulize Mwenyezi Mungu, basi tunaomba sasa mtoto Yesu atakayezaliwa siku ya Noeli (Mungu yu nasi) aingilie kati.

Nimkumbushe Rais Magufuli kwamba Noeli ni sikukuu ya mapinduzi ya kiroho, sikukuu ya uponyaji wa maovu duniani kwa nguvu za Mungu, Noeli ni sikukuu ya matumaini mapya. Krismasi ni sikukuu ya kuondoka katika giza na kuishi katika mwanga, sasa wewe kama Rais shiriki katika kuuleta mwanga wa mtoto Yesu nchini Tanzania.

Ni kwa mantiki hii naandika kwa kuthubutu kwamba dawa ya hali tete Zanzibar ni Rais Magufuli kukubali kufanya kazi na Maalim Seif wa CUF. Amani haiji ila kwa kutenda haki na Yesu anasema kwamba, ?Ukitaka amani tenda haki.?

Krismasi ni sikukuu ya kutenda haki. Usipotenda haki usitegemee amani hata ndani ya familia zetu, baba unapeleka pesa yote nyumba ndogo je, katika nyumba yako ya ndoa utakuwa na amani nayo? Kwa wasomaji wote wa Mwananchi na Watanzania kwa ujumla nawatakieni sikukuu njema ya Krismas na baraka tele kwa Mwaka Mpya 2016

chanzo.
http://www.mwananchi.co.tz/Makala/-/1597592/3007464/-/14qo4ds/-/index.html
 
Magufuli ameshakubali kufanya nae kazi. Kikwazo cha hii ishu tafuteni clip ya uhamsho wamewataja baadhi ya wanafiki wa zanzibar.
 
Naunga mkono hoja!.

Merry X-Mass & Prosperous New Year!.

Pasco

Zanzibar ni nchi ina rais wake ina katiba na bendera yake sasa Magufuri wapi na wapi ? Wazanzibari watu wa hajabu sana , wakati wa raha huwaambii kitu utasikia yakhe tuache tupumue , wakati Maji shingoni aaaah Magufuri . Mimi naona tuwaache wapumuliane !
 
Rais magufuli Hana mamlaka kwa sovereign ya Zanzibar ukizingatia inajihusisha na masuala yasiyo ya muungano!
maamuzi yafanywe na wazanzibar wenyewe
ni kukiuka sheria
 
Kwani wewe unadhan mpaka sasahiv hafanyi nae kazi?.......kilichomketa ikulu maalim seif ni nini hasa kama hawafanyikazi pamoja......hebu fikiri kabla ya kuzungumza.
 
Nami naunga mkono hoja. Chaguo la wananchi kupitia sanduku la kura ni Maalim Seif. Apewe pande hii ya muungano mara moja.
 
Tatizo hufuatilii habari..kinachomleta Seif ikulu ni kwamba aliomba mda mrefu mwenyewe kuonana na magufuli na sio magufuli alimwita kwa mujibu wa msemaji wa ikulu au afisa habari kama sijakosea.
 
Atangazwe. Magufuli ni raisi wa jamhuri wa muungano wa Tanzania, na amani ikikosekana zanzibar maana yake imekosekana tanzania nzima, ndo maana wamarekani wameinyima Tanzania msaada Tanzania (bara +visiwani). Magu akae na dk shein na chama chao (ccm) wakubali matokeo. Tatizo kubwa lilipo sio swala kikatiba kwa magufuli kuingilia huo mgogoro bali ni hofu ya muungano na pia ccm kuachia ngazi, kama ccm ikiwa tayari issue ya zenji na muafaka mbona ni wa dk mbili tu unakwisha.
 
Back
Top Bottom