Ukweli usioujua kuhusu uchaguzi wa meya jijini Arusha | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ukweli usioujua kuhusu uchaguzi wa meya jijini Arusha

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzee wa Rula, Jan 14, 2011.

 1. Mzee wa Rula

  Mzee wa Rula JF-Expert Member

  #1
  Jan 14, 2011
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 8,177
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Wana JF najua ni wengi wanajiuliza maswali mengi juu ya uhalali wa uchaguzi wa meya wa jiji la Arusha ambao umekuwa mjadala mpaka leo. Swali wengi wanalojiuliza je uchaguzi ulikuwa halali au si halali?
  Nataka niweke wazi uchaguzi ule ulikuwa halali kabisa na taratibu zilifuatwa kabisa. Kabla ya uchaguzi kufanyika kulikuwa na utata wa mjumbe mmoja wa CCM Mary Chitanda kupiga kura kwa sababu yeye si mwakilishi wa mkoa wa Arusha. Yeye ni katibu wa CCM mkoa wa Arusha lakini kwa sasa yeye ni mbunge wa viti maalum mkoani Tanga. CCM ilikuwa na wajumbe 15 ie madiwani na huyo mwenye utata 1 jumla ni 16. CDM ilikuwa na wajumbe 14 pamoja na G. Lema mbunge.
  Utata huu ulipelekea kuomba ufafanuzi, na ufafanuzi ulipatikana kuwa mjumbe yule yaani Mary Chitanda alikuwa halali kwa maandishi na siyo mdomo kwa vyama vyote, hiyo ilikuwa siku ya pili baada ya kuahirisha uchaguzi jana yake.
  Hilo ndiyo jambo kuu lilikuwa likibishaniwa. Sasa endapo jambo hili lilipatiwa ufumbuzi kwa maandishi inakuwaje leo hii viongozi wa CDM waendeleze malumbano jukwaani?
  Ni jambo lisilofichika kwa nini Mary Chitanda asiende kupiga kura Tanga badala yake Arusha. Hilo ndilo suala la msingi kabisa lakini majibu yake vile vile kisheria hakuna kipengele kinachomkataza kupiga kura kwani bado ni kiongozi wa wanaCCM Arusha, na kuzingatia sheria haimbani CCM wakaonelea basi ni vema wakaitumia loopwhole hiyo.
  Tuachane na ubishi kama sheria haimkabi basi CDM hawana haja ya malumbano. Machoni pa watu itaonekana si halali lakini mbele ya sheria inaonekana sawa. Katika uchaguzi wa urais hakuna mahakama yenye uwezo wa kutengua mara baada ya matokeo kutangazwa na tume ya uchaguzi. Hapa tunajifunza mapungufu ya sheria zetu za bongo. Hili ni jambo lisilopingika kabisa na kwa hili linahitaji mabadiliko.
  Uchaaguzi umekwisha na meya keshapatikana sasa kama sheria zilikikwa basi tukapate haki yetu mahakamani na siyo kwa mashinikizo ya jukwaani.
  CDM ni chama makini lakini kimepotoka kwa hili kwa ndiyo maana yake hawataki kwenda mahakamani kwa sababu wanajua hawana jipya. Kinachofanyika saizi ni propaganga ya sintofahamu ya tukio hili kwa wananchi!
  Ni kweli mara baada ya kupewa taarifa ya uhalali wa Mary Chitanda CDM walitoka nje kujadili wakawaacha wajumbe wengine 17 wakiwa ndani na kipindi hicho walishasaini tayari column ya mahudhurio! Ilipoonekana wamechelewa kurudi CCM hapo ndipo walipocheza rafu kwa kuendesha uchaguzi kwani tayari walikuwa na sababu zote za kushinda kesi. Sijui ni daftari au niiteje umesaini, kisha umetoka nje kujadili basi jamaa wakaendelea ndani na uchaguzi. CDM walishituka pindi matokeo yanatangazwa na kuja ukumbini wakiongozwa na mbunge wao Lema wakaambiwa nyie si MMESUSIA uchaguzi basi endeleeni ila viongozi wamepatikana.
  Huo ndiyo ukweli wa uchaguzi wa meya Arusha.
  Kwa kuwa ukweli huu umejificha kauli nyingi za kulaani zilitokea na kuzidi hasa baada ya maandamano kuzuiliwa na kupeleka vifo.
  Kauli za kiburi toka kwa viongozi wa CCM akiwemo Makamba zikaamsha hisia kali. CCM ni kama walikuwa wanawakebehi CDM kwa sababu walijua hawana pa kushika mahakamani na ndiyo maana wanawashinikiza viongozi wa CDM waande huko ili haki ijulikane.
  Usichokijua ni hiki, kwa nini wasiende mahakamani wafungue kesi kisha waitishe maandamano ili kushinikiza haki ya kusikilizwa kesi upesi. Kukataa kwao kwa kisingizio mahakama haitatenda haki kunatilisha mashaka na waelewe kuwa mashinikizo yao hayana direct impact badala yake yanawapa changamoto viongozi wa CCM.
  Mwisho naalani kwa kauli moja kuwa nguvu iliyotumika kuzima maandamano yale ilikuwa kubwa mno na viongozi wetu wa serikali waache kutumika kisiasa. La Arusha latosha kuwa funzo.
  Kikwete zlisema tukio la Arusha ndiyo mwanzo na mwisho naomba iwe kweli ingawaje nasikia Mbeya vijana wake wamekwisha ua tena!!!
  MD usiichangane na thread yoyote ile, iweke ili watu wajue na ku challange pale wanapoona siyo sahihi.
   
 2. m

  maselef JF-Expert Member

  #2
  Jan 14, 2011
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 255
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Wale wale wasiojua mambo. Your argument is baseless and doesn't click sensibly.
   
 3. Mzee wa Rula

  Mzee wa Rula JF-Expert Member

  #3
  Jan 14, 2011
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 8,177
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Lete habari wewe ni sehemu gani haikuingii akilini, naamini bado upo gizani na jambo usilijua litakusumbua sana.
   
 4. m

  mangoa Member

  #4
  Jan 14, 2011
  Joined: Jun 2, 2010
  Messages: 31
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nimefurahi kupata mtu anayeweza kuwaambia ukweli wana jamii nimependa askofu laizer na wenzake waujue ukweli huu,unajua haki inapatikana mahakamani tu ndo mana hata dr burian akaenda mahakamani na malla nae aende mahakamani,thanks
   
 5. VoiceOfReason

  VoiceOfReason JF-Expert Member

  #5
  Jan 14, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 5,234
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 0
  Hivi ni wangapi walipiga Kura..... na uchaguzi kuwa halali ni idadi gani ambayo inabidi ipige kura
   
 6. M

  Mwan mpambanaji JF-Expert Member

  #6
  Jan 14, 2011
  Joined: Apr 3, 2008
  Messages: 468
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  We mzee wa rula sielewi kama umelipwa kudanganya umma,au umeamuwa kwa maslahi yako mwenyewe,ila ukweli una tabia ya kujitetea,na katika hili ukweli utajitetea,ni hivi baada ya wajumbe wa cdm kuingia ukumbini na kumkuta mary chatanda,ambaye hata kabla habari zilishavuja kuwa ccm watamleta hali iliyofanya cdm kujipanga mapema,hawakusaini kwenye rejista na hili liko wazi na yeyote anawezaomba pale halmashauri ili aone hiyo rejesta kama kuna majina ya cdm,ubishi uliendelea kwa siku nzima,na hakuna suluhu na kwaMujibu wa kanuni mkurugenzi alipaswa kuhairisha kikao,alifanya hivyo kwa maelezo kuwa kesho yake yaani dec 18 wajumbe wote wakutane olasiti garden kwa ajili ya mafunzo ya madiwani,siku hiyo wajumbe wote wa chadema walifika hapo olasiti kama barua zao zilisema,hadi saa tano wajumbe wa ccm hawakuonekana,ghafla habari zikasema ccm wamechagua meya wao,hapo ndipo tatizo lilipoanzia hadi sasa,akidi haikutimia na hili liko wazi,,,,,
  ni saa ya ukombozi.....................
   
 7. M

  Malunde-Malundi JF-Expert Member

  #7
  Jan 14, 2011
  Joined: Jan 10, 2008
  Messages: 1,287
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  anaongea pumba mwanzisha mada
   
 8. M

  Malunde-Malundi JF-Expert Member

  #8
  Jan 14, 2011
  Joined: Jan 10, 2008
  Messages: 1,287
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  full pumba
   
 9. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #9
  Jan 14, 2011
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Yes -- hili suala la quorum, mbona wanalikwepa sasa? Walitimia theluthi mbili kama idadi inavyotakiwa na kanuni?
   
 10. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #10
  Jan 14, 2011
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Mzee wa Rula hapo umeweka rula inapotakiwa tena ni rula yenye pima maji.
   
 11. Monstgala

  Monstgala JF-Expert Member

  #11
  Jan 14, 2011
  Joined: Aug 25, 2009
  Messages: 1,080
  Likes Received: 77
  Trophy Points: 135

  Ng'ombe we endelea kujichanganya katika kauli zako mwenyewe.
   
 12. C

  Calist Senior Member

  #12
  Jan 14, 2011
  Joined: Dec 17, 2010
  Messages: 131
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Seenzi sana weye, ccm wenyewe bado wanaomba ufafanuzi kwa pm sio kili ufafanuzi unakidhi haja. Na quorum je ?
   
 13. R

  Rogers_ic Member

  #13
  Jan 14, 2011
  Joined: Nov 7, 2010
  Messages: 51
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  it is stupid to support stupid matters, mwenye akili nzima hawezi kuwa support ccm ku-take advantage kutotenda haki. it is silly enough beyond explanation, kwanini wasiwasubiri wafanye kikao kwa amani
   
 14. Mzee wa Rula

  Mzee wa Rula JF-Expert Member

  #14
  Jan 14, 2011
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 8,177
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Huna hoja, nadhani unataka kuleta sanaa kwenye jumba la sanaa!!!
   
 15. l

  limited JF-Expert Member

  #15
  Jan 14, 2011
  Joined: Feb 18, 2009
  Messages: 300
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35

  hizo loopholes na katiba ambayo haina maslahi to multparty ndio chanzo na ukiritimba wa ccm kwamba ndio chama pekee chenye haki
   
 16. Mzee wa Rula

  Mzee wa Rula JF-Expert Member

  #16
  Jan 14, 2011
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 8,177
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Sijatumika na sitatumika ila huo ndiyo ukweli ninaioufahamu. Kama huamini CDM hawawezi kwenda mahakamani mpaka kiama. Ukiona CDM hawaendi mahakamani jua mimi ni mkweli katika hili. Kwamba walitakiwa kukutana Olasiti Garden ni jambo la kushangaza, mimi nafahamu hawa jamaa walikuwa Equator Hotel iliyopo opposite na halmashauri.
   
 17. mchonga

  mchonga JF-Expert Member

  #17
  Jan 14, 2011
  Joined: Dec 3, 2006
  Messages: 1,250
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  crap
   
 18. Mzee wa Rula

  Mzee wa Rula JF-Expert Member

  #18
  Jan 14, 2011
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 8,177
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  2/3*32 = 21. Wao walikuwa 17, na CDM walihudhuria kisha wakatoa sasa wamlaumu nani. Hawakutimia kweli lakini walisusia.
   
 19. Consultant

  Consultant JF-Expert Member

  #19
  Jan 14, 2011
  Joined: Jun 15, 2008
  Messages: 5,788
  Likes Received: 6,301
  Trophy Points: 280

  Taratibu zilifuatwa??
   
 20. C

  Chan Senior Member

  #20
  Jan 14, 2011
  Joined: Jan 3, 2011
  Messages: 117
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  We kweli kilaza rudi shule kuliko kuonesha ubwege hapa jukwaani.
   
Loading...