Ndoa ni nusu ya dini

Dr criminal

JF-Expert Member
May 16, 2022
2,278
4,270
Hey there, i'm using JF

Wenye imani ya dini kama yangu na wengine ambao upendelea kujifunza vitu haijailishi chanzo cha hayo maarifa natumai tutakuwa tunaifahamu hii hadithi maarufu sana "Ndoa ni nusu ya Dini".

Ebu fikiria uislamu ulivyokuwa na mambo mengi swala tano, kufunga mwezi mtukufu, kutoa zaka, sadaka, kuhiji makka na makolo kolo mengine lakini unaambiwa hayo yote yatatengeneza nusu ya dini na nusu iliyobaki itatengenezwa na ndoa.

Kwa ufupi, as long as hujaoa au kuolewa huwezi timiza 100% ya dini, na ile umeoa tu kuolewa basi unakuwa umepata marks 50% za dini.

Nikawaza "Ndoa ina nini cha msingi hasa mpaka kupewa uzito huo?"

Ndugu zangu ndoa ndio msingi wa kila kitu, taifa linatengenezwa na ndoa, ukoo unatengenezwa na ndoa, Kijiji ni mkusanyiko wa ndoa, amani ya nchi yetu kiini ni ndoa, yani ndoa ndio starting point ya maisha yamwanadam.

Ndoa ni nyumbani mahali ambapo kuna watu ambao wakikuona wanafurahi kuwepo hai vivyo hivyo ukiwona unajiona mwenye bahati kuendelea kuwa hai, watu wanaokupa sababu yakuamka Kila asubuh kwenda kupambana.

"Kama ni hivyo mbona ndoa nyingine ni mateso matupu?"

Ndugu yangu hakuna kitu kinaitwa pingu yamaisha, mkishindwana talaka itolewe, hakuna ugomvi, hakuna maneno kila mtu ashike hamsini zake.

"Ukiona unateseka kwenye ndoa, toa au dai talaka." ndoa sio jela, ndoa sio uwanja wa ngumi, hayo mambo sijui watoto itakuaje, wewe tangu shawaha, mimba, leo mtoto anaongea ndo unajifanya kumuwazia sana? ebu tuwe tunafanya kazi zetu alafu mengine tumuachie mungu, ukiona hakufai mwache habari za watoto zisikuumize kichwa.

Kusema "Kataa Ndoa" kisa fulani kachapiwa mke wake ni sawa na kusema "Kataa kumiliki gari" kisa fulani alipata ajari ya gari akafa.

Ni Kweli Kuna ndoa zilikuwa na mwisho mbaya lakini haifanyi ndoa kuwa haramu, ndoa bado ni taasisi tunayohiitaji zaidi hasa kizazi hiki, mapropagandist wanaichafua sana dunia, kuteketeza taasisi nyeti kama ndoa tunawasaidi kutimiza malengo yao.

Mpaka unafikia uwamuzi wa kuoa au kuolewa we ni mtu mzima unajua baya na jema, kama Kuna kitu hakipo sawa ongea na mwenzio, Kuna vitu vinaongeleka, vinaeleweka na vinasameheka ila kama vitu havisameeki na kama aelewi piga chini, kama Kuna sehem ilitakiwa kuwa na amani iliyotukuka basi ni kwenye ndoa.

Alafu ndoa isiwe ndio mwisho wa maisha yako bali iwe ni sehemu ya maisha yako kiasi kwamba mambo yasipo kuwa mambo unaweza anza upya.

Pia nikiri kwamba sheria inakuja kuharibu taasisi ya ndoa, hasa kwenye suala zima la mali na malezi ya mtoto/watoto ikitokea mmegombana, lakini sheria zinatungwa na nani?, strange idadi kubwa ya wabunge ni wanaume mkatunga sheria ya kujikandamiza nyinyi wenyewe, ama kweli ukiyaona ya Mussa...

Oa/Olewa ila ndoa isikufunge, kama unateseka Kwa namna yeyeto ile toa/dai talaka ondoka, ndoa ni uwanja wa amani.

Sipingi mtu kuwa shoga, lakini kwanini utumie nguvu nyingi sana ku-normaliize ushoga?

Siwapingi wanao Kataa ndoa, lakini kwanini mtumie nguvu nyingi sana ku-normaliize kukataa ndoa?

~ Acha uoga
~ Acha ujinga
~ Acha mikumbo
~ Acha utoto

Kijana kama mda umefika na upo vizuri, oa.

Dr criminal
 
Ndoa ni utumwa kwa sasa ...labda ipatikane katiba mpya iangalie hili swala la ndoa kwa undani.kuna vitu havipo sawa kwenye ndoa .mfano amekukuta na mali zako mkiachana anataka pasu pasu, kumbe lengo lake ni mali zako huoni uonezi huu??! tena anakufanyia maksudi muachanee...

Kingine nimekufumania nikakupiga chini unaenda nishtaki sijui dawati la jinsia sihudumii mtoto/watoto wakati chanzo ni huyo mwanamke na usaliti wake na huko jinsia wanasahau pia hata mimi nina maumivu ya kusalitiwa wanamsikiliza yeye mimi nani ataniponya kidonda changu?? tena inauma haswa kwa mtu aliyekuwa anajitoa haswa kwenye ndoaa.kumbe mwanzangu ana mtu wake anayemuelewa na hata hela ya kusuka hachangii yeye ni kumshughulikia tu mkeo....
 
Yaap, mwenyew hapo juu nimekir kwamba hiyo sheria ni kandamizi

Lakini wabunge wengi si wanaume, kwa maana hii sheria tumeitunga sisi wanaume.

Ni ndoa zote zimeishia uko?

Hiyo ndio njia pekee ya kitatua swala hilo?

Kuna changamoto sio za kukwepa ni kutatua
 
Hey there, i'm using JF

Wenye imani ya dini kama yangu na wengine ambao upendelea kujifunza vitu haijailishi chanzo cha hayo maarifa natumai tutakuwa tunaifahamu hii hadithi maarufu sana "NDOA NI NUSU YA DINI"

Ebu fikiria uislamu ulivyokuwa na mambo mengi swala tano, kufunga mwezi mtukufu, kutoa zaka, sadaka, kuhiji makka na makolo kolo mengine lakini unaambiwa hayo yote yatatengeneza nusu ya dini na nusu iliyobaki itatengenezwa na ndoa

Kwa ufupi, as long as hujaoa au kuolewa huwezi timiza 100% ya dini, na ile umeoa tu kuolewa basi unakuwa umepata marks 50% za dini.

Nikawaza "Ndoa ina nini cha msingi hasa mpaka kupewa uzito huo?"

Ndugu zangu ndoa ndio msingi wa kila kitu, taifa linatengenezwa na ndoa, ukoo unatengenezwa na ndoa, Kijiji ni mkusanyiko wa ndoa, amani ya nchi yetu kiini ni ndoa, yani ndoa ndio starting point ya maisha yamwanadam.

Ndoa ni nyumbani mahali ambapo kuna watu ambao wakikuona wanafurahi kuwepo hai vivyo hivyo ukiwona unajiona mwenye bahati kuendelea kuwa hai, watu wanaokupa sababu yakuamka Kila asubuh kwenda kupambana.

"Kama ni hivyo mbona ndoa nyingine ni mateso matupu?"

Ndugu yangu hakuna kitu kinaitwa pingu yamaisha, mkishindwana talaka itolewe, hakuna ugomvi, hakuna maneno kila mtu ashike hamsini zake.

"UKIONA UNATESEKA KWENYE NDOA, TOA AU DAI TALAKA" ndoa sio jela, ndoa sio uwanja wa ngumi, hayo mambo sijui watoto itakuaje, wewe tangu shawaha, mimba, leo mtoto anaongea ndo unajifanya kumuwazia sana? ebu tuwe tunafanya kazi zetu alafu mengine tumuachie mungu, ukiona hakufai mwache habari za watoto zisikuumize kichwa.

Kusema "KATAA NDOA" kisa fulani kachapiwa mke wake ni sawa na kusema "KATAA KUMILIKI GARI" kisa fulani alipata ajari ya gari akafa.

Ni Kweli Kuna ndoa zilikuwa na mwisho mbaya lakini haifanyi ndoa kuwa haramu, ndoa bado ni taasisi tunayohiitaji zaidi hasa kizazi hiki, mapropagandist wanaichafua sana dunia, kuteketeza taasisi nyeti kama ndoa tunawasaidi kutimiza malengo yao.

Mpaka unafikia uwamuzi wa kuoa au kuolewa we ni mtu mzima unajua baya na jema, kama Kuna kitu hakipo sawa ongea na mwenzio, Kuna vitu vinaongeleka, vinaeleweka na vinasameheka ila kama vitu havisameeki na kama aelewi piga chini, kama Kuna sehem ilitakiwa kuwa na amani iliyotukuka basi ni kwenye ndoa.

Alafu ndoa isiwe ndio mwisho wa maisha yako bali iwe ni sehemu ya maisha yako kiasi kwamba mambo yasipo kuwa mambo unaweza anza upya.

Pia nikiri kwamba sheria inakuja kuharibu taasisi ya ndoa, hasa kwenye suala zima la mali na malezi ya mtoto/watoto ikitokea mmegombana, lakini sheria zinatungwa na nani?, strange idadi kubwa ya wabunge ni wanaume mkatunga sheria ya kujikandamiza nyinyi wenyewe, ama Kweli ukiyaona ya mussa..

Oa/Olewa ila ndoa isikufunge, kama unateseka Kwa namna yeyeto ile toa/dai talaka ondoka, ndoa ni uwanja wa amani.

Sipingi mtu kuwa shoga, lakini kwanini utumie nguvu nyingi sana ku-normaliize ushoga?

Siwapingi wanao Kataa ndoa, lakini kwanini mtumie nguvu nyingi sana ku-normaliize kukataa ndoa?

Acha uoga
Acha ujinga
Acha mikumbo
Acha utoto

Kijana kama mda umefika na upo vizuri, oa

Dr criminal

"Ndoa ni nyumbani mahali ambapo kuna watu ambao wakikuona wanafurahi kuwepo hai vivyo hivyo ukiwona unajiona mwenye bahati kuendelea kuwa hai, watu wanaokupa sababu yakuamka Kila asubuh kwenda kupambana"

Haya maneno magumu sana, inapaswa, ila sio guarantee
 
Ndugu zangu ndoa ndio msingi wa kila kitu, taifa linatengenezwa na ndoa, ukoo unatengenezwa na ndoa, Kijiji ni mkusanyiko wa ndoa, amani ya nchi yetu kiini ni ndoa, yani ndoa ndio starting point ya maisha yamwanadam.
Taifa la Vatican limetengenezwa na nini ?

Karibu.
 
Kijana kama mda umefika na upo vizuri, oa
emoji736.png
.
Kwa nini aoe ?
 
So tutakaa kutafuta maendeleo kwa ajili ya mwanamke tu?? yani nimeoa feminist tumeachana, mali zangu zimepigwa pasu, nimeoa tena imetokea the same mali zimepigwa pasu, aiseee....!!! Mtoa mada umepuyanga vibaya sana...bila sheria ya ndoa kubadilishwa hatuoi,, KATAA NDOA, NDOA NI UJAMBAZI, NDOA NI UHAINI.
 
"Ebu fikiria uislamu ulivyokuwa na mambo mengi swala tano, kufunga mwezi mtukufu, kutoa zaka, sadaka, kuhiji makka na makolo kolo mengine lakini unaambiwa hayo yote yatatengeneza nusu ya dini na nusu iliyobaki itatengenezwa na ndoa."

☝️☝️☝️☝️ kama unaona hayo ni Mengi inabidi ujitafakari zaidi (ikiwa wewe ni muislamu , maana post yako inaviashira kuonesha wewe ni muislamu).

N.b
Wengi wanaotoaga kauli za hivyo kwa asilimia kubwa huwa mlango wa msikiti wanauona mara moja moja siku ya ijumaa , na kufunga ni mpaka ramadhani tena si siku zote ila kwenye kuoa tu tena wake zaidi ya mmoja bila kuangalia sheria na hukum zinasemaje .
 
Back
Top Bottom