Ukweli usemwe Polepole ni dhaifu na hakukata kiu

Ukweli usemwe Polepole ni dhaifu na hakukata kiu

PLOII

JF-Expert Member
Joined
Sep 24, 2013
Posts
1,101
Reaction score
809
Habari za Sabato watu wa Mungu,

Niende kwenye Mada Kwa ufupi Sana,

Nimewaza mengi lakini kubwa huenda Wazee wetu walioasisi hili Taifa letu (Tanganyika) hakuwa JASIRI kama ambavyo tunawasoma kwenye historia.

Kiongozi shupavu haogopi ushindani, kuwajibika na kukubali ukosoaji mfano tangu tupate UHURU wa Nchi yetu wakosoaji wengi walipitia nyakati ngumu akina Christopher Tumbo wakapewa vyeo nje ya Nchi (Uingereza) Lengo kunyamazisha Upinzani(iwapo baadae aliachana na hiyo nafasi na kurudi nyumbani kuendeleza MAPAMBANO) na wengine akina Bi. Titi wakafungwa Kwa kosa la uhaini pia wengine wakawekwa kizuizini (Detention) kama Tuntameke Sanga (Msomi huyu) hiyo ndio historia ya watangulizi wetu.

Watangulizi wetu waliandaa Katiba ya Leo ambayo kwetu inaonekana inaminya Demokrasia pia walianzisha mfumo wa uongozi ambao hadi Leo tunae Mama yetu kipenzi Samia na huo mfumo hujabadilika bali wamebadilika watu Kwa maana kuna vijana wamezaliwa kwenye uso wa Nchi yetu (Tanganyika) natumia neno Tanganyika Kwa sababu watu wa upande wa visiwani Wana tabia tofauti kabisa na ni waungwana Madhira Yao yote ni influence ya Tanganyika (refer General election 2015).

Hadithi zote za kiutawala na uongozi zinawekwa kuwa Siri, kuwa ni Jambo la Usalama wa Taifa na hapa ndio kiini macho kinaanzia. Shujaa pekee ni Yule atakayekuja akafungua yaliyomo huko ndani maana yale ya historia wengi tunayajua.

Humphrey Polepole hakuja na Jambo jipya bado ana tabia zile zile za kale kuficha ficha mambo tunayohitaji kujua, Kijana kaja na historia yake ambayo sio hitaji Kwa wengi wetu mfano Mimi binafsi ningependa kama angesema Kwa uwazi hao "WAHUNI" waliotaka kuchakachua uchaguzi wa 2015 na mchakato wa Katiba 2014. Huyu kijana nilitegemea aseme Nani anaongoza na kutoa maelekezo katika Nchi yetu maana anasema " kama nyumba haina mwenyewe"
Anasema kuna kikundi kina nguvu na anawajua wahusika basi wataje ndio mambo tunataka lakini kaishia kusema historia na kutumia codes of which most of us we are very aware of it.

Humphrey cannot be compared with Nape na Mkapa na wengine Kwa sababu Rais wetu huyu 1995-2005 aliwahi kusema kupitia kitabu chake " CCM tulichukuwa pesa za Serikali Kwa ajili ya kampeni ya wagombea wetu" hii statement ina uzito wake pia kijana wetu Nape akasema "tutashinda hata Kwa goli la mkono 2015"
akamshauri Byabato Kule Bukoba akae Kwa kutulia maana yeye ni mzoefu kweli na atampa mbinu ya ushindi "issue sio kupiga Kura ila anayesimamia Kura kuhesabiwa na matokeo kutangazwa......."
Kuna DC akasema wazi kuwa 2020 Madiwani hawakufanya kampeni bali walipitishwa na yeye alishiriki ipasavyo...." nilifanya Kazi kubwa na naenda hadi porini kufanya Kazi......."

Kwangu naweza kusema hawa ndio waliongea kishujaa sio Balozi wetu Polepole anatoa simulizi nani asiyejua alihusika kwenye ulanguzi wa viongozi wa vyama pinzani ( refer case ya Mashinji) akiwa kama mkurugenzi wa mafunzo na Itikadi alibeba 30M kumlipia fine aliyekuwa Katibu Mkuu wa CHADEMA (hapa namaanisha kama ameamua kuokoka toa vyote vilivyo vya shetani sio kubaki na hirizi na vyungu ukisema unaacha Kwa ajili ya kusikilizia). Kasahau 2020 Fomu ya URAIS ilikuwa Moja though anajitetea kuwa Prime Minister & Vice president hawatakiwi kuwa President wa Nchi ....... ......
But anasahau Samia Kwa sasa sio Vice president ni President na haongozi kwenye term ya V yupo ya Vi kama Watangulizi wake katika awamu zao wali- enjoy the so- called Fomu Moja why not Samia, hapa nongwa ya nini na ifahamike kila zama na namna yake na kila kiongozi anapata uongozi Kwa style yake refer case ya GERALD FORD alikuwa US House of Representative lakini 1973 Spiro Theodore Agnew stepped down na Ford akawa Vice na August 1974 Nixon Richard akaondoka kwa kashifa ya "Watergate Scandal" na Ford akawa Rais wa USA. Huu ni mfano tu kuwa kila mtu anakuwa kiongozi Kwa namna tofauti Mungu anavyo mwezesha.

Kwangu Nape na Mkapa ndio mashujaa wa kusema ukweli uliofichwa Humphrey Polepole bado hajaleta Jambo Jipya yupo kwenye kutafuta legality sio legitimacy kama ambavyo alimsaidia Rais wa awamu ya TANO kutimiza the- so called LEGITIMACY Leo kijana hataki hiyo Kwa Rais Samia.

NB: Nazani Kwa kizazi cha Leo wanamhitaji mtu atakayesema ukweli mchungu ambao utapelekea mageuzi kwenye maisha ya watu wa kizazi hiki, kizazi hiki kinahitaji MITAJI, AJIRA, AFYA BORA, MAZINGIRA MAZURI YA BIASHARA, UWEKAZAJI WENYE TIJA na MIKOPO hasa Kwa watoto wetu (HESLB). Kama kuna mtu analeta narratives za Maisha yake is out of focus.

Shukran Sana ndugu zangu Naomba niishie hapa.
 
Back
Top Bottom