Ukweli usemwe, Dr. Slaa hakuwahi kuukamia Urais

Petro E. Mselewa

JF-Expert Member
Joined
Dec 27, 2012
Posts
10,347
Reaction score
26,153
Dr. Wilbrod P. Slaa ni mwanasiasa aliyekamilika. Yeye amejaliwa uelewa,uwezo wa kujenga hoja,ubunifu,uongozi na hata kupambania ustawi wa Taifa hili. Dr. Slaa ana rekodi iliyotukuka kuanzia Baraza la Maaskofu Tanzania,Jimboni Karatu hadi kwenye uongozi CHADEMA kama Makamu wa Mwenyekiti na sasa Katibu Mkuu.

Kutokana na sifa nyingi nzuri kuliko udhaifu wake,Dr. Slaa amejizolea wafuasi na watu wanaomuamini. Hao wamekuwa wakikesha wakimuombea maisha marefu ili mabadiliko yapatikane kwa njia ya kisiasa na tuwe na Tanzania mpya. Mimi binafsi ingawa si mwanachama wa CHADEMA wala chama chochote ni mfuasi wa Dr. Slaa. Naamini katika maono na mipango yake. Ameijenga CHADEMA kwa hali na mali na hataweza kuibomoa.

Dr. Slaa hakuhitaji kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Maaskofu kuwatumikia wakatoliki na watanzania kwa ujumla. Hakuhitaji ukuu wa mkoa au wilaya kuwatumikia wananchi wa Karatu na watanzania. Hakuhitaji Uwaziri Mkuu au Uwaziri kuwatumikia watanzania kama Mbunge wa kupigiwa mfano.

Dr. Slaa hata mwaka 2010 hakuomba kugombea Urais bali aliombwa akibebwa na rekodi zake za kuvutia za uongozi. Akakubali kugombea akizingatia mahitaji na maslahi ya Taifa. Dr. Slaa hakuwa anausaka wala kuukamia Urais hata mwaka huu. Ni mwanasiasa anayeamini katika Katiba na Taratibu za chama chake. Dr. Slaa akipitishwa au asipopitishwa,kama ameomba ridhaa,ataendeleza mapambano yake kisiasa. Hana uchu wala vurugu kuhusu Urais. Ukweli usemwe ili ujitenge na propaganda.
 
safi sana kwa uchambuzi sababu ccm umu wanatokwa na mapovu leo ndio wanataka slaa agombanie urais

wasubiri sindano iwaingie
 
Dr. Slaa kwa sisi tunaosoma theolojia ana upendo wa AGAPE kwa watanzania, hana tamaa ya cheo,hana chuki,ana moyo wa huruma na anachukia dhuluma.

Mungu azidi kumlinda na endelee kumtumia ili atutumikie watanzania kwa moyo wote na upendo katika nafsi iliyombele yake
 
Hivi kwa nini usiondoke nae kuliko kushinda unabadili posti kwa jambo lilelile? Hivi Slaa anaweza kushindana na Magufuri kweli na akafikikia hata asilimia 35%? Acheni kuhadaa Watanzania wanaotaka kuutokomeza mfumo ovyo wa CCM,Mara ngapi upinzani unagaragazwa na kisingizia kuibiwa kura. Unakera sana kwa kujiona unafahamu sana siasa za upinzani na nina wasiwasi sana na wewe kama si CCM au ACT.
 
Dr. Wilbrod P. Slaa ni mwanasiasa aliyekamilika. Yeye amejaliwa uelewa,uwezo wa kujenga hoja,ubunifu,uongozi na hata kupambania ustawi wa Taifa hili. Dr. Slaa ana rekodi iliyotukuka kuanzia Baraza la Maaskofu Tanzania,Jimboni Karatu hadi kwenye uongozi CHADEMA kama Makamu wa Mwenyekiti na sasa Katibu Mkuu.

Kutokana na sifa nyingi nzuri kuliko udhaifu wake,Dr. Slaa amejizolea wafuasi na watu wanaomuamini. Hao wamekuwa wakikesha wakimuombea maisha marefu ili mabadiliko yapatikane kwa njia ya kisiasa na tuwe na Tanzania mpya. Mimi binafsi ingawa si mwanachama wa CHADEMA wala chama chochote ni mfuasi wa Dr. Slaa. Naamini katika maono na mipango yake. Ameijenga CHADEMA kwa hali na mali na hataweza kuibomoa.

Dr. Slaa hakuhitaji kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Maaskofu kuwatumikia wakatoliki na watanzania kwa ujumla. Hakuhitaji ukuu wa mkoa au wilaya kuwatumikia wananchi wa Karatu na watanzania. Hakuhitaji Uwaziri Mkuu au Uwaziri kuwatumikia watanzania kama Mbunge wa kupigiwa mfano.

Dr. Slaa hata mwaka 2010 hakuomba kugombea Urais bali aliombwa akibebwa na rekodi zake za kuvutia za uongozi. Akakubali kugombea akizingatia mahitaji na maslahi ya Taifa. Dr. Slaa hakuwa anausaka wala kuukamia Urais hata mwaka huu. Ni mwanasiasa anayeamini katika Katiba na Taratibu za chama chake. Dr. Slaa akipitishwa au asipopitishwa,kama ameomba ridhaa,ataendeleza mapambano yake kisiasa. Hana uchu wala vurugu kuhusu Urais. Ukweli usemwe ili ujitenge na propaganda.

Mkuu Mselwa ningeomba uwakopi hao wanachafua JM na propaganda zao. Mkuu nimeipenda kwani it speaks for itself. Shukrani kwani hii mijamaa inatafuta kila mbinu kuleta vurugu ndani ya chama.
 
Hakika huyu mzee Mungu ampe hekima na busara ktk kipindi hiki kwani atapokea cm nying zikimuhamasisha kufanya visivyo lakin Mungu akupe busara baba harakati na mchango wako tunautambua na tunakuhitaj zaid ya oxygen ukiwa ndan ya chama kubwa chadema/Ukawa!!
 
Hivi kwa nini isiondoke nae kuliko kushinda unabadili posti kwa jambo lilelile? Hivi Slaa anaweza kushindana na Magufuri kweli na akafikikia hata asilimia 35%? Acheni kuhadaa Watanzania wanaotaka kuutokomeza mfumo ovyo wa CCM,Mara ngapi upinzani unagaragazwa na kisingizia kuibiwa kura. Unakera sana kwa kujiona unafahamu sana siasa za upinzani na nina wasiwasi sana na wewe kama si CCM au ACT.

Mkuu nisome vyema na unaruhusiwa kubadili maoni yako
 
Naona kwa mbali zinaanza hoja za kumjaji Dr.Slaa ,bado kidogo tutasikia alikuwa msaliti wa chama.

Dr.Slaa Mungu akupe maamuzi ya hekima kwa wakati huu, kazi uliyoufanyia upinzani Tanzania hautasahaulika kamwe .

Dr.Slaa mzalendo wa ukweli, tatizo lako huna pesa za kununua kura milioni mbili .
 
Hivi kwa nini usiondoke nae kuliko kushinda unabadili posti kwa jambo lilelile? Hivi Slaa anaweza kushindana na Magufuri kweli na akafikikia hata asilimia 35%? Acheni kuhadaa Watanzania wanaotaka kuutokomeza mfumo ovyo wa CCM,Mara ngapi upinzani unagaragazwa na kisingizia kuibiwa kura. Unakera sana kwa kujiona unafahamu sana siasa za upinzani na nina wasiwasi sana na wewe kama si CCM au ACT.

Mkuu usilipuke kwa mihemko, ujana unapapara. Hifadhi maneno ya akiba ikulu haiwezi kuwa kipaumbele kabla ya maadili kwa mtu makini. Lowasa anataka power kama ilivyokuwa kwa Legan wa marekani, swala la chama halimuhusu kabisa.
Mbaya zaidi madume manne ya ukawa yanaongea kwa mihemko as if no Lowasa no upinzani.
 
Ni mwanasiasa anayeamini katika Katiba na Taratibu za chama chake. Dr. Slaa akipitishwa au asipopitishwa,kama ameomba ridhaa,ataendeleza mapambano yake kisiasa. Hana uchu wala vurugu kuhusu Urais. Ukweli usemwe ili ujitenge na propaganda.

Anaamini katiba na taratibu za chama ila mmemsaliti kwa kuteua mgombea bila kufata katiba na taratibu za chama. Malipo yenu October 25.
 
Dr. Wilbrod P. Slaa ni mwanasiasa aliyekamilika. Yeye amejaliwa uelewa,uwezo wa kujenga hoja,ubunifu,uongozi na hata kupambania ustawi wa Taifa hili. Dr. Slaa ana rekodi iliyotukuka kuanzia Baraza la Maaskofu Tanzania,Jimboni Karatu hadi kwenye uongozi CHADEMA kama Makamu wa Mwenyekiti na sasa Katibu Mkuu.

Kutokana na sifa nyingi nzuri kuliko udhaifu wake,Dr. Slaa amejizolea wafuasi na watu wanaomuamini. Hao wamekuwa wakikesha wakimuombea maisha marefu ili mabadiliko yapatikane kwa njia ya kisiasa na tuwe na Tanzania mpya. Mimi binafsi ingawa si mwanachama wa CHADEMA wala chama chochote ni mfuasi wa Dr. Slaa. Naamini katika maono na mipango yake. Ameijenga CHADEMA kwa hali na mali na hataweza kuibomoa.

Dr. Slaa hakuhitaji kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Maaskofu kuwatumikia wakatoliki na watanzania kwa ujumla. Hakuhitaji ukuu wa mkoa au wilaya kuwatumikia wananchi wa Karatu na watanzania. Hakuhitaji Uwaziri Mkuu au Uwaziri kuwatumikia watanzania kama Mbunge wa kupigiwa mfano.

Dr. Slaa hata mwaka 2010 hakuomba kugombea Urais bali aliombwa akibebwa na rekodi zake za kuvutia za uongozi. Akakubali kugombea akizingatia mahitaji na maslahi ya Taifa. Dr. Slaa hakuwa anausaka wala kuukamia Urais hata mwaka huu. Ni mwanasiasa anayeamini katika Katiba na Taratibu za chama chake. Dr. Slaa akipitishwa au asipopitishwa,kama ameomba ridhaa,ataendeleza mapambano yake kisiasa. Hana uchu wala vurugu kuhusu Urais. Ukweli usemwe ili ujitenge na propaganda.
umeongea jambo zito sana ninaamini Dr Slaa ameweka manufaa ya taifa na wananchi mbele ni kweli tafiti nyingi zinaonyesha ana nguvu sana lakini kwa mfumo uliopo labda ukawa wakiiunganisha nguvu na baadhi ya wana siasa wa ccm tunaweza libomoa liccm
 
Shukrani Mkuu

Mkuu kipindi hiki ndicho makamanda wanatakiwa kuwa makini kuliko vyote....

Nakumbuka Dr. Slaa alikua tayari kumpokea Sitta akagombee Urais na ilibidi aingie mwishoni baada ya Sitta kuwaacha kwenye mataa....

Kumsajili kiongozi wa vita kutoka kwa adui zenu ni vizuri zaidi kwakuwa mnapata mbonu na nguvu zaidi za kumpiga adui....
 
Mkuu usilipuke kwa mihemko, ujana unapapara. Hifadhi maneno ya akiba ikulu haiwezi kuwa kipaumbele kabla ya maadili kwa mtu makini. Lowasa anataka power kama ilivyokuwa kwa Legan wa marekani, swala la chama halimuhusu kabisa.
Mbaya zaidi madume manne ya ukawa yanaongea kwa mihemko as if no Lowasa no upinzani.
Lowassa hajawahi mzidi Dr Slaa kwa polls za wazi popote pale , ninadhani kuna la ziada ambalo chadema na ukawa wameliona mbele hadi Lowassa akakubaliwa kuingia chadema wengi tumekwazwa na jambo hilo lakini nadhani kulikuwa na sababu ya muhimu wananchi na wafuasi wa chadema hatujawekwa wazi zaidi kinachotakiwa ni kuivunja system ya kifedhuli inayolindwa na chama cha CCM
 
Back
Top Bottom