Ukweli unaanza na wewe mwenyewe.

ndayilagije

JF-Expert Member
Nov 7, 2016
7,492
8,295
Heri ya mwaka mpya.
Hakuna mtu anayependa uongo jamani hapa tusidanganyane..kila mtu anapenda ukweli. Iwe kwenye biashara, mapenzi ,siasa au popote pale. Ukweli ni muhimu.
Tatizo ni pale unapotaka kuambiwa ukweli ambao hupendi kujiambia.
Tuanze mwaka kwa kujiambia ukweli.
Ukishindwa sema nimeshindwa,ukipenda sema nimependa,usipoelewa sema sielewi. Ukiwa huna kiri kwa Moyo na kinywa kuwa sina. Kama hujui usione taabu kusema hili silijui.
Hata ukikosolewa sema sawa wewe umeona hivyo,ila mimi nimeona hivi.
Ukizidiwa kubali tu hapa nimezidiwa !inabidi nijitahidi. Ukichoka pia sema hili limenichosha,silihitaji tena.
Ukiona taabu kumwambia mtu unavyoamini basi kaa kimya,usimdanganye .
Watu tunajisifiasifia ujinga sana,hata ukila mlenda sema tu moyoni kuwa ninataka nyama lakini sina huu mlenda nimekula tu. Siyo unaanza nyama za kazi gani sasa,kwanza zinaleta gout.
Pambania Imani yako,pigania nafasi yako kama unaamini unastahili kitu fulani,hata Kama huna sema kile nastahili kuwa nacho.
Unafiki wa kujinafika ni mbaya kuliko wa kunafikiwa na wengine.
Hakuna mtu ataona zuri ndani yako zaidi yako wewe angalia vile unavyoyapokea maneno ya wanaokukatisha tamaa,ukiyaamini yatakuwa kweli.
Katika unyonge wako jua wapo uliowazidi.
Usiache kuwasaidia kwa maana mkono utoao umebarikiwa kuliko upokeao.
Kumbuka wewe ni wewe.ngo'mbe wake siyo mbuzi wako.
Heri ya mwaka mpya.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom