Ukweli Nyuma ya Teknolojia za Kisasa

bless on

JF-Expert Member
Joined
May 22, 2026
Posts
1,111
Reaction score
2,707
Zamani zadi ya miaka 2,000 iliyopita, Socrates, mwanafalsafa maarufu wa Kigiriki, alipinga maandishi akidhani yataharibu uwezo wa binadamu wa kukumbuka mambo kichwani. Hofu kama hii imejirudia kila teknolojia mpya inapokuja na uwezo ambao watu hawajawahi kuuona. Internet, radio, upigaji picha, telegraph, umeme, AI na machine learning zote zimewahi kuonekana za ajabu kabla watu hawajaelewa kinachoendelea nyuma yake.

Hizi si teknolojia za uchawi. Lakini zinafanya mambo ambayo wakati mwingine yanaonekana hivyo.

1. AI inawezaje kuzungumza kama binadamu?
Inaandika, inaongea, inachambua na hata kutengeneza picha.

2. Algorithm inajuaje unachotaka kuona?
Unaongea kuhusu bidhaa fulani. Dakika chache baadaye, unaiona kwenye simu.

3. Face Recognition
Kamera inaweza kukutambua bila wewe kutaja jina lako.

4. GPS inajuaje ulipo?
Simu yako inaweza kujua ulipo hata kama hujui mahali hapo.

Targeted Ads
Tangazo linaonekana wakati ambao unaanza kujiuliza: “Wamenisikia?

Mara nyingi kuna data, sensors na algorithms zinazofanya kazi kimya kimya nyuma ya pazia. Tatizo ni kwamba hatuoni mchakato, tunaona matokeo tu. Na pale ambapo hatuoni kinachoendelea, ubongo wetu huanza kujaza pengo kwa tafsiri yake.
 
Sisi weusi ni kulaumu mbona kwetu serikali hairuhusu AI , kipind fulani nilikuwa kwenye mambo fulani basi kwenye group letu tulikuwa mpaka na kiongozi ambaye angeenda kuomba serikali iruhusu matumizi ya safaru za kidigitali , tena ushabiki mkubwa .

Kwa afrika , hilo suala ni gumu sana ,tutaendelea kuzalish watumiaji wa AI n content creators ila sio wnaojua hivyo vitu vimeundwa vipi ..Tunapenda ushbiki na kulaumu , mbona kwetu hatutumii AI nchi fulani wo wanatumia .
 
Kwani uchawi haupo?
This is your problem, not AI's

Kama mwanadamu anaweza kumtukuza mtu alieua watu na kubaka watu ili amfikishie dini kwa nini mtu huyo huyo asifikirie AI ni uchawi?

Kipindi mzungu ana invest kushindana na fikra yake, waafrika mlikuwa mnatukuza mambo ya kufikirika ndio maana mnaona AI ni maajabu ya mauza uza
 
Inatumika ila kwa kiwango kidogo sana.
 
Mkuu bless on imeandikwa maarifa yataongezeka!

Ila nadhani binadamu anafanya mambo makubwa sana...

Nahisi wale malaika walio wafundisha uchawi wakati wa gharika wamerudi kivingine kabisa...

Kuna huyu nikola tesla huanajiuliza nini kiko nyuma ya 369 method!
 
Unashauri au kupendekeza nini kifanyike?
 
Nahisi wale malaika walio wafundisha uchawi wakati wa gharika wamerudi kivingine

Hapa panafikirisha.
 
Nahisi wale malaika walio wafundisha uchawi wakati wa gharika wamerudi kivingine

Hapa panafikirisha.
Usiumie kufikiri; Kajisomee kitabu cha Enock (Henoko) sura ya 9-12. utakutana na habari habari tajwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…