Ukweli niupate wapi?

Ukweli niupate wapi?

Mapema mwezi uliopita nilikwenda Dar -Es-Salaam kwa masuala tofauti ktk ofisi moja ya Serikali,nilishangazwa sana na kilichonikuta.Niliingia ofisi hiyo na kumkuta dada mmoja baada ya kuruhusiwa na katibu mtasi wake,baada ya kusalimiana nilianza kueleza shida yangu,lakini cha Kushangaza ilionekana Kama vile kapumbazika hivi na kisha akaniambia "samahani kaka naomba uje kesho nitakuwa na majibu ya tatizo lako"?nilishukuru kisha nkaondoka,niliporudi kesho yake pamoja na majibu ya tatizo langu alinitaka niache namba ya simu kwaajili ya kujua jambo langu linaendeleaje.

Ilipofika saa kumi siku hiyo nilipokea simu ,mpiga simu alijitambulisha kuwa ni yule afisa aliekuwa anashughulikia suala langu,kisha akaniomba tukutane hoteli moja jijini saa moja maana kuna jambo alitaka kunieleza juu ya tatizo langu Kabla sijaondoka maana nilikuwa nimemueleza kuwa ningeondoka kesho yake kurudi mkoani kwangu ,nilimjibu kuwa hiyo hoteli siijui kisha akaniambia nichukue tax watanifikisha pale.

Baada ya kufika kwenye hoteli na kukutana nae nilishangazwa sana na maneno yake,pale aliposema ananishangaa kujifanya simjui wakati yeye ananijua na alikuwa mapenzi wangu miaka 7 iliyopita na alienda mbali zaidi kwa kusema nilimuachia mimba na sasa ana mtoto wa kike mwenye umri wa miaka Saba.Kwangu ilikuwa kama hadithi za bibi maana alichokesema sikukitalajia.pamoja na maelezo yake marefu na lawama nyingi nilimuomba anihakikishie hilo maana mimi sikujua lolote.

Akisema mwaka 2010 tulikutana Mjini Iringa ,alikuwa akisoma chuo kimojawapo akisoma shahada ya kwanza na alikuwa mpangaji wa shangazi yangu aliekuwa anafanya kazi ofisi ya mkuu wa mkoa na ndipo tulipoanzisha mahusiano na baada ya siku tatu niliondoka kurudi chuoni nilipokuwa nikisoma mkoani Morogoro na baada ya kuondoka hakuwa na mawasiliano na mimi tena na aliogopa kumuuliza Yule aliedai kuwa ni shangazi baada ya mwezi mmoja alimaliza masomo yake na kurudi kwao.baada ya kujingudua ana ujauzito aliamua kunifata ktk chuo nilichodai nasoma lakini alinitafuta bila mafanikio,ndipo aliporudi Iringa na kuambiwa kuwa Yule shangazi alikuwa amefariki na kuwa nyumba ilikwisha uzwa na alifanya juhudi lakini bila mafanikio.
Baada ya kumsikiliza nilimtaka radhi kwa kumpa pole maana sikuwa mimi na lazima atakuwa amenifananisha.kwani 1. Sikuwahi kwenda Iringa mwaka huo,2. sikuwahi kuwa na shangazi aliekuwa aliishia Iringa na kibaya zaidi sikuwa na shangazi aliekuwa hai mwaka huo maana shangazi yangu pekee alifariki mwaka 2001 3. Sikuwahi kusoma Morogoro.Alinisihi sana kuwa mwanangu ananihitaji sana kwani anamuuliza baba yake yupo wapi na yeye hajaolewa maana aliapa kutoolewa mpaka ampate baba wa mtoto wake ambao waliagana kuoana na hakupenda kuzaa watoto kwa baba tofauti.
Pamoja na kuongea mengi na kuendelea kuwasiliana sielewi nini a nataka huyu dada na kwanini anaamini mimi ndie baba wa huyo mtoto? Binafsi ninauhakika Mimi sie ingawa yeye anaamini Mimi ndie ,mpango wetu ni kwenda kupima DNA ilitujilidhishe ingawa mimi sioni haja ya kujisumbua kwa hili.ninaona Imani yake kwangu ni kubwa kiasi kwamba nadhani atajidhuru ikiwa itagundulika sio kana alivyodhani.Ushahuri wenu tafadhari

Utakapokuta DNA ni sawa na huyo mtoto ndio utakapo toa mimacho [emoji15]
Wazungu wanaita DOUBLE GANGER
 
Kaka nielekeze ofisi ilipo namie niende labda ndo tabia yake anahamu na mipododo... ni pm asee
 
Mkuu hebu fafanua hapa kidogo. Anasema mmekutana 2010 wewe ukaodoka kwenda Morogoro. Alisema ulikuwa bf wake miaka 7 nyuma na mtoto ana miaka 7 hebu nipe jibu hapa. 2010 mpaka 2016 ni miaka 6 sasa hio miaka 7 inatokea wapi?
 
Kuna uwezekano huyo dada alimpenda sana jamaa (baby daddy), na alipoondoka jamaa, dada akatengeneza uzio fulani kichwani mwake kujikinga na maumivu ya kuachwa kwa kujiaminisha kuwa jamaa atarudi siku moja, na wataendelea na maisha yao. So baada ya muda wa kuwa in denial, hiyo hali imejijenga kama uhalisia kichwani mwake. Pengine una qualities ambazo alikuwa nazo jamaa, so mwanamama anamuona jamaa kwako.

Unaweza kumsaidia kwa kumtafutia wataalamu wa saikolojia, na mhudhurie wote coz pengine ni wewe ndio uko in denial kwa sababu zako tofauti. Naamini baada ya kumuona mtaalam, hakutakuwa na umuhimu wa DNA.
 
Binadamu wawili wawili inawezekana sana mnafanana sana na huyo jamaa yake na hana nia mbaya yoyote kwako, lakini msema kweli wa kumuhakikishia huyo dada kwamba wewe si Baba wa huyo binti yake ni DNA. Anaonekana ana nafasi nzuri kama yuko tayari kuingia gharama za DNA mwache alipe ili ajihakikishie kwamba AMEKURUPUKA.
 
Mungu ndie jibu la kumrudisha baba wa mtoto wake.

Asikulazimishe bure.
 
naona taratiibu unaanza kuelekea kibra... soon utaelewa na hzi sikukuu znazokuja
 
Mapema mwezi uliopita nilikwenda Dar -Es-Salaam kwa masuala tofauti ktk ofisi moja ya Serikali,nilishangazwa sana na kilichonikuta.Niliingia ofisi hiyo na kumkuta dada mmoja baada ya kuruhusiwa na katibu mtasi wake,baada ya kusalimiana nilianza kueleza shida yangu,lakini cha Kushangaza ilionekana Kama vile kapumbazika hivi na kisha akaniambia "samahani kaka naomba uje kesho nitakuwa na majibu ya tatizo lako"?nilishukuru kisha nkaondoka,niliporudi kesho yake pamoja na majibu ya tatizo langu alinitaka niache namba ya simu kwaajili ya kujua jambo langu linaendeleaje.

Ilipofika saa kumi siku hiyo nilipokea simu ,mpiga simu alijitambulisha kuwa ni yule afisa aliekuwa anashughulikia suala langu,kisha akaniomba tukutane hoteli moja jijini saa moja maana kuna jambo alitaka kunieleza juu ya tatizo langu Kabla sijaondoka maana nilikuwa nimemueleza kuwa ningeondoka kesho yake kurudi mkoani kwangu ,nilimjibu kuwa hiyo hoteli siijui kisha akaniambia nichukue tax watanifikisha pale.

Baada ya kufika kwenye hoteli na kukutana nae nilishangazwa sana na maneno yake,pale aliposema ananishangaa kujifanya simjui wakati yeye ananijua na alikuwa mapenzi wangu miaka 7 iliyopita na alienda mbali zaidi kwa kusema nilimuachia mimba na sasa ana mtoto wa kike mwenye umri wa miaka Saba.Kwangu ilikuwa kama hadithi za bibi maana alichokesema sikukitalajia.pamoja na maelezo yake marefu na lawama nyingi nilimuomba anihakikishie hilo maana mimi sikujua lolote.

Akisema mwaka 2010 tulikutana Mjini Iringa ,alikuwa akisoma chuo kimojawapo akisoma shahada ya kwanza na alikuwa mpangaji wa shangazi yangu aliekuwa anafanya kazi ofisi ya mkuu wa mkoa na ndipo tulipoanzisha mahusiano na baada ya siku tatu niliondoka kurudi chuoni nilipokuwa nikisoma mkoani Morogoro na baada ya kuondoka hakuwa na mawasiliano na mimi tena na aliogopa kumuuliza Yule aliedai kuwa ni shangazi baada ya mwezi mmoja alimaliza masomo yake na kurudi kwao.baada ya kujingudua ana ujauzito aliamua kunifata ktk chuo nilichodai nasoma lakini alinitafuta bila mafanikio,ndipo aliporudi Iringa na kuambiwa kuwa Yule shangazi alikuwa amefariki na kuwa nyumba ilikwisha uzwa na alifanya juhudi lakini bila mafanikio.
Baada ya kumsikiliza nilimtaka radhi kwa kumpa pole maana sikuwa mimi na lazima atakuwa amenifananisha.kwani 1. Sikuwahi kwenda Iringa mwaka huo,2. sikuwahi kuwa na shangazi aliekuwa aliishia Iringa na kibaya zaidi sikuwa na shangazi aliekuwa hai mwaka huo maana shangazi yangu pekee alifariki mwaka 2001 3. Sikuwahi kusoma Morogoro.Alinisihi sana kuwa mwanangu ananihitaji sana kwani anamuuliza baba yake yupo wapi na yeye hajaolewa maana aliapa kutoolewa mpaka ampate baba wa mtoto wake ambao waliagana kuoana na hakupenda kuzaa watoto kwa baba tofauti.
Pamoja na kuongea mengi na kuendelea kuwasiliana sielewi nini a nataka huyu dada na kwanini anaamini mimi ndie baba wa huyo mtoto? Binafsi ninauhakika Mimi sie ingawa yeye anaamini Mimi ndie ,mpango wetu ni kwenda kupima DNA ilitujilidhishe ingawa mimi sioni haja ya kujisumbua kwa hili.ninaona Imani yake kwangu ni kubwa kiasi kwamba nadhani atajidhuru ikiwa itagundulika sio kana alivyodhani.Ushahuri wenu tafadhari
Huna akili
 
Back
Top Bottom