kabiriga
JF-Expert Member
- Nov 18, 2012
- 1,098
- 1,150
Mapema mwezi uliopita nilikwenda Dar -Es-Salaam kwa masuala tofauti ktk ofisi moja ya Serikali,nilishangazwa sana na kilichonikuta.Niliingia ofisi hiyo na kumkuta dada mmoja baada ya kuruhusiwa na katibu mtasi wake,baada ya kusalimiana nilianza kueleza shida yangu,lakini cha Kushangaza ilionekana Kama vile kapumbazika hivi na kisha akaniambia "samahani kaka naomba uje kesho nitakuwa na majibu ya tatizo lako"?nilishukuru kisha nkaondoka,niliporudi kesho yake pamoja na majibu ya tatizo langu alinitaka niache namba ya simu kwaajili ya kujua jambo langu linaendeleaje.
Ilipofika saa kumi siku hiyo nilipokea simu ,mpiga simu alijitambulisha kuwa ni yule afisa aliekuwa anashughulikia suala langu,kisha akaniomba tukutane hoteli moja jijini saa moja maana kuna jambo alitaka kunieleza juu ya tatizo langu Kabla sijaondoka maana nilikuwa nimemueleza kuwa ningeondoka kesho yake kurudi mkoani kwangu ,nilimjibu kuwa hiyo hoteli siijui kisha akaniambia nichukue tax watanifikisha pale.
Baada ya kufika kwenye hoteli na kukutana nae nilishangazwa sana na maneno yake,pale aliposema ananishangaa kujifanya simjui wakati yeye ananijua na alikuwa mapenzi wangu miaka 7 iliyopita na alienda mbali zaidi kwa kusema nilimuachia mimba na sasa ana mtoto wa kike mwenye umri wa miaka Saba.Kwangu ilikuwa kama hadithi za bibi maana alichokesema sikukitalajia.pamoja na maelezo yake marefu na lawama nyingi nilimuomba anihakikishie hilo maana mimi sikujua lolote.
Akisema mwaka 2010 tulikutana Mjini Iringa ,alikuwa akisoma chuo kimojawapo akisoma shahada ya kwanza na alikuwa mpangaji wa shangazi yangu aliekuwa anafanya kazi ofisi ya mkuu wa mkoa na ndipo tulipoanzisha mahusiano na baada ya siku tatu niliondoka kurudi chuoni nilipokuwa nikisoma mkoani Morogoro na baada ya kuondoka hakuwa na mawasiliano na mimi tena na aliogopa kumuuliza Yule aliedai kuwa ni shangazi baada ya mwezi mmoja alimaliza masomo yake na kurudi kwao.baada ya kujingudua ana ujauzito aliamua kunifata ktk chuo nilichodai nasoma lakini alinitafuta bila mafanikio,ndipo aliporudi Iringa na kuambiwa kuwa Yule shangazi alikuwa amefariki na kuwa nyumba ilikwisha uzwa na alifanya juhudi lakini bila mafanikio.
Baada ya kumsikiliza nilimtaka radhi kwa kumpa pole maana sikuwa mimi na lazima atakuwa amenifananisha.kwani 1. Sikuwahi kwenda Iringa mwaka huo,2. sikuwahi kuwa na shangazi aliekuwa aliishia Iringa na kibaya zaidi sikuwa na shangazi aliekuwa hai mwaka huo maana shangazi yangu pekee alifariki mwaka 2001 3. Sikuwahi kusoma Morogoro.Alinisihi sana kuwa mwanangu ananihitaji sana kwani anamuuliza baba yake yupo wapi na yeye hajaolewa maana aliapa kutoolewa mpaka ampate baba wa mtoto wake ambao waliagana kuoana na hakupenda kuzaa watoto kwa baba tofauti.
Pamoja na kuongea mengi na kuendelea kuwasiliana sielewi nini a nataka huyu dada na kwanini anaamini mimi ndie baba wa huyo mtoto? Binafsi ninauhakika Mimi sie ingawa yeye anaamini Mimi ndie ,mpango wetu ni kwenda kupima DNA ilitujilidhishe ingawa mimi sioni haja ya kujisumbua kwa hili.ninaona Imani yake kwangu ni kubwa kiasi kwamba nadhani atajidhuru ikiwa itagundulika sio kana alivyodhani.Ushahuri wenu tafadhari