Ukweli ni upi kuhusu Oscar Kambona?

Nyerere nasikia alikuwa anaogopa sana challenge za wasomi na ndio maana kipindi cha utawala wake wasomi wengi walikimbilia nje. Pia kuna tetesi kwamba Nyerere alienda Makerere University kwa nia ya kusoma Udaktari lakini alifeli sana masomo ya science, lakini kutokana na urafiki wa wakoloni na familia ya Nyerere wakaona siyo busara wa kijan wao huyo kuja bila degree, hivyo wakamwambia asome art yaani Education hasa kwenye masomo ya historia. Sasa kuanzia aliwaogopa sana wasomi kwani shuleni walimzidi akadhani na huku kwenye siasa watamfunika vilevile.
 
Wazee wa TANU walikosea sana kumpa huyu jamaa nchi kwa nini asipewe Kambona(jina safi kabisa la kimwera hili) ili kabila lina weledi na mambo ya uongozi natumai mh. Bernad Membe atafaa kuiongoza nchi hii na kukizi mahitaji ya watanzania.
 
Nyerere
nasikia alikuwa anaogopa sana challenge za wasomi na ndio maana kipindi
cha utawala wake wasomi wengi walikimbilia nje. Pia kuna tetesi kwamba
Nyerere alienda Makerere University kwa nia ya kusoma Udaktari lakini
alifeli sana masomo ya science, lakini kutokana na urafiki wa wakoloni
na familia ya Nyerere wakaona siyo busara wa kijan wao huyo kuja bila
degree, hivyo wakamwambia asome art yaani Education hasa kwenye masomo
ya historia. Sasa kuanzia aliwaogopa sana wasomi kwani shuleni walimzidi
akadhani na huku kwenye siasa watamfunika vilevile.

kuna baadhi ya wanahistoria wanadai Kambona angelikuwa rais bora kuliko Nyerere, walichukuliaje swala hili?
 
kuna baadhi ya wanahistoria wanadai Kambona angelikuwa rais bora kuliko Nyerere, walichukuliaje swala hili?
Historia ya Kambona siijui sana, kwani ilifichwafichwa aidha bahati mbaya au makusudi. Maoni ni subjective issue,

 
inaonekana TANU iliharibu nyota ya Kambona maana ukiangalia kwa makini mapendekezo yake, yalikuwa ya kimsingi na yangepewa nafasi huenda hivi leo tungekuwa tunajadili historia tofauti.

hakika, sio tu Kambona wapo wengi sana kama akina Tuntemeke Sanga, Tumbo na wengineo wote waliopishana mawazo na watawala waliojiita waasisi.
 
hakika, sio tu Kambona wapo wengi sana kama akina Tuntemeke Sanga, Tumbo na wengineo wote waliopishana mawazo na watawala waliojiita waasisi.

Unakisea kusema walijiita waasisi kwani hata akina babu, kambona, tuntemeke sanga wangewashinda akili akina nyerere na karume leo wangeitwa waasisi, chuki na jazba si suluhisho la mambo so tuwe rational,

Nyerere na kambona walitofautiana ki itikadi na ndiyo ulikuwa mwanzo wa kutokuelewana kwao

ni ukweli kama tungechukua falsafa za akina kambona keo tungekuwa na tz ya tofauti kabisa kwani nadhan watu wengi tusingekuwa hum tunachangia kulingana na sera za kibepar ambazo huwa hazijar wanyonge ambapo zenyewe huwa zina wapromote matajiri na kuendeleza kukuza matabaka,

tanzania ya leo hata kama ipo na matabaka na mabepari kiukweli ilijengwa kijamaa na sera za akina nyerere ambazo akina kambona walizikimbia

siwezu kulazimisha kumpenda nyerere ila ukweli unabaki palepale kwamba enzi zake ardhi ilikuwa haichewi si tu na wawekezaji bali mabepar ambao wananunua halaf hawaifanyii chochote,

enzi zake ulikuwa huwez kuta mtuanaripishwa huduma za afya na hata shule ilikuwa ni uwezo wako tuu,

hivyo sera za ujamaa zina mazur yake kwan zimesababisha hata hawa wajanja wanaouza nchi kwa sasa kuikuta ipo

kwan kunanchi kama kenya wao walianza zaman kwa sasa hakuna cha kuuza tena....

sera ni sera na chuki i chuki, mimi nimejaribu kuongelea sera kati ya akina kambona dhid ya nyerere...

wasalaa.
 
the best president that we never had, huyu jamaa angetufikisha mbali Sana. nyerere alimkimbiza kizuizini kwani alikuwa anapinga Sera za ujamaa
 
Ziara mbili Ughaibuni zilivunja urafiki na Nyerere
KUNA wakati nilimsikia Hamad Rashid akitoa hoja
bungeni. Wakati huo mbunge huyo wa CUF
alikuwa kiongozi wa Upinzani bungeni. Hamad
Rashid aliomba kambi ya Upinzani bungeni
ibadilishwe jina na badala yake iitwe kambi ya
Ushindani bungeni. Ni kwa vile neno ‘upinzani’
linatafsiriwa vibaya na wananchi. Spika Samwel
Sitta alisimama na kutamka; “ Mtaendelea kuitwa
hivyo hivyo kambi ya Upinzani, kwa vile nyinyi ni
watu wa kupingapinga tu!”
Na maneno haya ya Samwel Sitta yanatokana na
historia yetu. Maana; haya ni makosa ya kihistoria
yaliyofanywa na waliojenga msingi wa taifa letu.
Na ndio tunayoyaona hata katika mfarakano wa
miaka 50 iliyopita kati ya Julius Nyerere na Oscar
Kambona.
Na mara ile, mwaka 1965, TANU ilipoachana na
mfumo wa vyama vingi na kuasisi mfumo wa
chama kimoja, Kambona alipata kutamka: ”Kwa
nini tupige marufuku vyama vingine vya siasa
wakati tunajua wananchi walio wengi wanaipigia
kura TANU?” Kambona akaongeza kusema: ”Bila
shaka, umaarufu wa TANU utabaki kwa muda
mrefu, lakini, je, pale umaarufu wa TANU
utakapopungua, ina maana tuwe madikteta?”,
alihoji Kambona.
Nimepata kukumbushia mara kadhaa kuwa
historia ni mwalimu mzuri. Na wanadamu
hatupaswi kuwa vipofu wa historia yetu wenyewe.
Kuifumbia macho historia yako ni kujiandalia njia
ya kutumbukia korongoni kwa kujitakia.
Tunapoadhimisha miaka 50 ya Uhuru wa
Tanganyika, tuna lazima ya kuipitia na kuitafakari
historia yetu. Kwa macho makavu na maangavu,
tuangalie nyuma tulikota. Tuangalie tulipo sasa.
Ndio, tufanye hivyo ili tuutafute mwelekeo
mwema wa nchi yetu hata kwa miaka mingine 50
ijayo.
Tuna maswali mengi ya kujiuliza, moja kuu ni hili;
Je, ni nchi ya namna gani tutayotaka kuijenga na
hata kuvirithisha vizazi vijavyo? Kwa maneno
mengine; ni jamii gani tunayotaka kuijenga? Sisi
wa kizazi cha Azimio tulikuwa wadogo sana katika
miaka kumi ya mwanzo ya uhuru, na hata
utekelezaji wa Azimio la Arusha. Nimezaliwa Ilala,
Dar es Salaam, Machi 11, 1966.
Ndio, kuna mema mengi tuliyoyaona, lakini
tukitafakari sasa, kuna mabaya mengi pia
tuliyoyashuhudia. Tuna wajibu wa kusimulia mema
na mabaya hayo kwa manufaa ya Watanzania wa
kizazi cha sasa na vizazi vijavyo.
Kati ya kumbukumbu zangu mbaya za wakati huo
ni jinsi tulivyowaona wazazi wetu wakiishi kwa
hofu. Waliogopa kushutumu mamlaka hadharani
na kwa sauti. Waliishutumu Serikali na hata
kiongozi mkuu wa nchi kwa kunong’ona.
Wazazi wetu walimwogopa hata mjumbe wa
nyumba kumi. Ni ukweli kuwa kwa wakati ule,
Serikali na chama tawala havikuwa na uvumilivu
wa sauti za upinzani.
Na siku zote mamlaka bila upinzani huzaa kiburi
na majigambo. Huzaa hali ya kutokujali na kukosa
usikivu. Taratibu, huzaa hali ya kujisikia u-bwana
mkubwa. Hali hii ikiachwa ikaendelea, basi,
husababisha madhara makubwa kwa nchi. Huleta
hasara kubwa kwa nchi, kiuchumi na kijamii.
Juma la jana nilimalizia kwa kuandika kuwa makala
haya ni jaribio la kuvunja ukimya wa juu ya nini
kilitokea takribani miaka 50 iliyopita. Ni mmoja tu
wa mfano wa jinsi umma ulivyofichwa ukweli wa
juu ya nini hasa kilitokea kikasababisha mfarakano
wa waliopata kuwa viongozi wa mstari wa mbele
kwenye harakati za kuanzishwa kwa TANU na
kudai uhuru wa Tanganyika; Julius Kambarage
Nyerere na Oscar Salathiel Kambona.
Kuna aliyesoma makala yangu ya juma la jana na
kuniuliza; ” Maggid, hivi wewe huogopi?” Ni kweli,
kama ningeandika haya mwaka 1976 nilipokuwa
mtoto wa umri wa miaka kumi tu, basi, vyombo
vya dola vingenishukia mithili ya mwewe
anayekishukia kifaranga cha kuku. Sio tu mimi
ningeswekwa rumande ya watoto, bali hata mama
na baba yangu wangetikiswa na dola kwa ’
dhambi’ ya kumzaa mtoto mwenye fikra za ’
kipinzanipinzani ’ na ’ kihainihaini’.
Na hapa ndipo kwenye moja ya mapungufu
makubwa ya waliojenga msingi wa taifa letu;
kuchukia wenye kufikiri tofauti na watawala. Na
zaidi kuwachukia wenye ’ akili’ ya kufikiri na
kuutumia vema welewa wao.
Si tunajua kuwa utotoni tulisikia kuna maadui wa
nchi wa aina mbili; maadui wa nje na wa ndani.
Wapinzani ama wenye kufikiri tofauti ndimo
walimowekwa wanaoitwa ’maadui wa ndani!’
Niseme tu, mfulilizo wa makala haya ni moja ya
makala zangu muhimu tangu nianze kushika
kalamu na kuandika makala magazetini. Na
naandika nikiwa sina hata chembe ya hofu. Ni kwa
sababu moja kuu; kuwa yanahusu historia yetu na
mustakabali wa nchi yetu. Sote tuna wajibu wa
kuandika historia yetu.
Hii ni nchi yetu. Hatuna sababu za kuionea aibu
historia yetu, na badala yake tujivunie kuwa tuna
historia. Na ni unyonge na utumwa kusubiri
wasomi kutoka Marekani na Ulaya waje kutafiti na
kutuandikia historia yetu. Historia yako isimulie
mwenyewe.
Hivyo basi, tuna wajibu wa kuifanya kazi hiyo.
Historia itusaidie kutukumbusha machungu na
furaha ya tuliyoyapitia kama taifa. Si kwa kuandika
tu, hata kwa kusimulia machache
tuliyoyashuhudia.
Niliahidi kuchambua zaidi juu ya marafiki hawa
watatu; Kambona, Nyerere na Kawawa. Nitafanya
hivyo sasa.
Naam. Julius na Oscar walikuwa viongozi vijana
sana katika Tanganyika huru ya wakati huo.
Ikumbukwe wakati tukipata uhuru, Nyerere
alikuwa na miaka 39 na Oscar alikuwa na miaka
36. Hawa walikuwa ni vijana waliokabidhiwa
dhamana kubwa ya kuiongoza nchi kubwa ya
Tanganyika. Naamini walikuwa ni wenye dhamira
njema kwa taifa hili; Julius, Oscar, Rashid na
wenzao wengine katika TANU.
Ukweli unabaki kuwa Oscar Kambona hakuikimbia
nchi yake kwa kashfa ya kuiba fedha za Serikali au
ufisadi mwingine. Na kwa utafiti mdogo tu
niliofanya, nilichobaini ni ukweli kuwa marafiki
hawa wawili; Oscar na Julius walikuwa na
mgongano wa tofauti ya kimaono ya kisiasa
yaliyoathiri hata urafiki wao.
Maana; haiyumkini Kambona aliyeaminiwa na
Nyerere akaja kuwa Katibu Mkuu wa kwanza wa
TANU, akawa Waziri wa kwanza wa Elimu wa
Tanganyika huru, akaja kuwa Waziri wa Mambo ya
Ndani na hata kwa wakati mmoja kushika wizara
mbili - Waziri wa Ulinzi na Waziri wa Mambo ya
Nje. Kwamba aje tena baadae kutuhumiwa
uhaini, na hata kushukiwa uraia wake!
Ndio, kwangu mimi ya Kambona na Nyerere
ilihusu zaidi mgongano wa tofauti za kimaono ya
kisiasa . Na ukiingia kwa undani kwenye maandiko
na simulizi utaupata ushahidi wa haya.
Na kwa hakika, ili siasa ya nchi istawi, basi,
inahitaji uwepo wa migongano ya kifikra. Hivyo
basi, siasa ni migongano ya kifikra yenye kuhitaji
majadiliano endelevu.
Tunaona kuwa migongano ya kifikra kati ya Oscar
na Julius ilianza kuonekana dhahiri katika ziara
mbili walizozifanya kwa pamoja katika mataifa
mawili tofauti. Ziara ya Marekani mwaka 1963 na
ziara ya Uchina mwaka 1965. Na hapo katikati
kuna jambo lililosababisha uwepo wa mahusiano
ya mashaka kati ya Julius na Oscar. Ni uasi wa
jeshi wa Janauri 20, 1964.
Uasi ule ulisababisha Nyerere na Kawawa waende
mafichoni. Inasimuliwa walijihifadhi eneo la
Kigamboni. Mjini alibaki Oscar Kambona
aliyeshiriki kikamilifu kuwatuliza wanajeshi wale.
Kimsingi, katika kipindi kile cha maasi, Kambona,
kama angetaka, alikuwa na fursa ya kutwaa
mamlaka ya nchi akisaidiwa na jeshi. Inasemwa
kuwa akiwa Waziri wa Ulinzi, Kambona alikubalika
sana jeshini.
Baada ya ziara ya Marekani akiwa na Oscar
Kambona mwaka 1963 ambako Rais John
Kennedy alimsifia sana Nyerere kwa kuonyesha
uwezo wa kiuongozi, miaka miwili baadae, mwaka
1965, Nyerere na msafara wake akiwamo Oscar
Kambona, walikwenda China kwa mara ya kwanza
na kulakiwa na Mwenyekiti Mao Tse Tung.
Nyerere akiwa kwenye gari la wazi na mwenyeji
wake Mao, alishangiliwa na Wachina wapatao
milioni moja waliojipanga barabarani.
Pale Ilala tulikoishi, nakumbuka nikiwa na umri wa
miaka sita tu, usiku mmoja pale viwanja vya shule
ya msingi Boma tuliangalia sinema ya ziara ya
Julius Nyerere Uchina .
Nyerere aliiona China na alivutiwa sana. ”What we
have seen in China is relevant to us”, nimemsikia
Nyerere akiongea hayo kwenye kipande cha
filamu ya zamani kilichopo mtandaoni .
Alimaanisha walichokiona China kinaweza
kikafanyika kwetu.
Na Julius alianza kwa kubadilisha hata staili yake
ya mavazi, yakafanana na ya Mwenyekiti Mao, na
wengine katika TANU wakamwiga. Ni nini
kilitokea kwenye Mkutano wa TANU wa Januari,
1967 na kabla ya hapo? Mkutano huo ulisababisha
kumalizika kabisa kwa urafiki wa Nyerere na
Kambona. Fuatilia toleo lijalo.

Tunasubiri toleo lijalo. Mbona haliji hapa?
 
Kifo cha sokoine nyerere alihusika asilimia 100 . Huyu mzee hakutaka mtu wa kutofautiana naye chochote . Alikuwa dikteta mmbaya sana.

eeeeeeeeeeeee!! Na kifo cha ..... nani alihusika kama syo benja
 
Soma kitabu kinachoitwa The Dar Mutiny of 1964 cha Tony Laurence
Soma Southern African Political History: A Chronology of Key Political Events from Independence to Mid-1997 kazi ya Jacqueline Audrey Kalley
Soma chapisho la Godfrey Mwakikagile, Nyerere and Africa: End of an Era
  • Godfrey Mwakikagile, chapter 13, "Coup Attempts Against President Julius Nyerere and Reflections on Coup Leader Oscar Kambona by Andrew Nyerere," in his bookNyerere and Africa: End of an Era, 2nd Edition (Las Vegas, Nevada: Protea Publishing Co., 2005), pp. 359 – 377.
 
Marehemu Oscar Kambona alizaliwa mwaka 1925 katika kijiji cha Kwambe kilichopo mwambao mwa ziwa Nyasa, karibu na Mbamba-bay, wilaya ya Mbinga, Mkoa wa Ruvuma. Alikuwa mtoto wa marehemu Rev. David Kambona na Bibi Miriam Kambona.

Rev. Kambona alikuwa ni miongoni mwa waafrika wa kwanza kupata upadre katika kanisa la Anglikana la Tanganyika. Wakati Oscar Kambona akiwa mdogo, baba yake alikuwa akimweleza kuhusu ndoto zake juu ya uhuru wa nchi yake, hivyo Oscar alikuwa akiwa na hamu sana ya kuitumikia nchi yake.

Oscar alipata elimu ya msingi nyumbani kwao, chini ya mwembe (ambao bado upo), katika kijiji chao kwa kuwatumia wazazi wake wote wawili na mjomba wake, ambao wote walikuwa walimu. Baada ya hapo alipelekwa shule ya kati ya Mt. Barnabas, Liuli, na baadaye shule ya Sekondari ya Alliance, ambako alilipiwa ada na Askofu mzungu wa Anglikana kwa vile baba yake hakuweza kumudu kulipa ada ya paundi 30 kwa mwaka.

Oscar alikuwa akisimulia jinsi alivyoweza kumshawishi Askofu huyo amlipie ada kwa kusema sala ya Baba yetu kwa kizungu. Oscar alichaguliwa kwenda ‘Tabora Boy’s Senior Government School’, ambako alionana na Julius Nyerere kwa mara ya kwanza; wakati huo Nyerere alikuwa anafundisha katika shule ya kikatoliki.

Baada ya kumaliza masomo ya sekondari alienda katika shule yake iliyopita ya Alliance kama mwalimu na baadae alichaguliwa kuwa ‘Schoolmaster’. Ilikuwa katika mkutano wa kitaifa wa walimu, mnamo mwaka 1954, ambapo Kambona na Nyerere walikutana tena.

Kambona alikuwa tayari kukitumikia chama cha TANU ambacho kilikuwa kimeanzishwa muda si mrefu, lakini Nyerere akasema wasingeweza kumwajiri kwa vile chama kilikuwa hakina fedha.

Kambona akasema chama hakikuwa na fedha kwa vile hakikuwa na ‘organising secretary, na ndipo alipoamua kufanya kazi hiyo ili kujenga chama, bila ya malipo’. Aliishi kwa kutegemea akiba aliyojitunzia kwa kufanya kazi miezi 6.

Katika kipindi hiki Kambona alisafiri sehemu mbalimbali za nchi na kuonana na machifu na wazee wa vijiji ili kusajili wanachama. Katika miezi 6 alifanikiwa kusajili wanachama 10,000, na hadi kufikia mwaka mmoja alikuwa amepata wanachama hai 100,000. Kambona alitumia michango aliyopata kufungua akaunti ya kwanza ya TANU.

alienda Butiama kumshawishi Nyerere achukuwe uongozi wa chama moja kwa moja. Baada ya miaka mitatu Kambona aliamua kwenda kusomea sheria katika Chuo cha Middle Temple, nchini Uingereza mwaka 1957 kwa ufadhili wa Gavana.

Akiwa London Kambona alikuwa kiongozi wa chama cha wanafunzi wa Tanganyika na Mwenyekiti wa tawi la TANU la London. Ni wakati huo ambapo Kambona alipata fursa ya kukutana kwa mara ya kwanza na watu mashuhuri kama George Padmore, mwanaharakati wa umoja wa Afrika, ambaye alimshawishi ahudhurie mkutano wa mwaka 1958 wa waafrika wote(All Africa’s Peoples Conference), uliofanyika nchini Ghana muda mfupi baada ya kupata Uhuru.

Akiwa Ghana Kambona alipata nafasi ya kukutana na mwanaharakati mwingine maarufu wa siasa za Afrikla, Kwame Nkurumah. Akiwa uingereza Kambona alikuwa mwaafrika wa kwanza kutangaza taarifa ya habari kwa Kiswahili katika idhaa ya kiswahili ya BBC.

Aliporudi nchini Tanganyika, mwaka 1959, TANU ilikuwa imeshaweka bayana madai yake ya kupewa serikali ya madaraka, vinginevyo TANU ilikuwa tayari kuanzisha mapambano kama ilivyokuwa kwa Mau Mau ya Kenya. Wakiwa London wakisubiri kupewa madaraka ya ndani, Nyerere na Kambona walijadili hatua mbalimbali ambazo zingechukuliwa ili kuepuka kutoweka kwa amani.

Wakati akizungumza na waandishi wa habari mjini Londoni 1991, Kambona alikumbuka matukio kama hivi, ‘’Bwana Nyerere alikuwa akiishi nami katika chumba kidogo nilichopewa chuoni.

Tulijadiliana ni namna gani angeweza kurudi nyumani na kuonana na wafuasi wake bila kupewa serikali ya madaraka. Baadae nilifanikiwa kumshauri kuwa wakati atapozungumza na vyombo vya habari katika the East African Arch aseme kuwa walowezi wa kizungu ambao wapo Tanganyika wana hekima zaidi katika kanda ya Afrika Mashariki.

Alikubali kusema hivyo endapo na yeye Kambona angekubali kukatisha masomo yake ya sheria huko London na kurudi Tanganyika ili ampe nguvu na kumuunga mkono katika kikao cha kamati kuu ya TANU wakati akitetea tamko lake la wenye hekima zaidi.

Katika uchaguzi wa kwanza TANU ilishinda viti vyote isipokuwa kimoja. TANU iliunda serikali ya mambo ya ndani chini ya Nyerere ambaye alikuwa Waziri kiongozi wa kwanza.

Na katika harakati hizo za matayarisho ya serikali ya ndani, Kambona alimwoa Flora Moriyo wakati wakiwa kwenye msafara wa harakati za kukamilisha matayarisho ya uhuru na serikali ya Uingereza. Harusi ilifungwa katika kanisa la Mt. Paul, London, na Nyerere ndiye alikuwa msimamizi. Kambona aliteuliwa kuwa waziri wa Elimu.

Baadaye alishika nyadhifa za waziri wa Mambo ya Ndani, Mambo ya nchi za nje na Ulinzi na Tawala za Mikoa. Pia alikuwa mwenyekiti wa kwanza wa Kamati ya Ukombozi ya Umoja wa Nchi Huru za Afrika na mwenyekiti wa utayarishaji wa AOU charter.

Mwaka 1964, Kambona alifanya kazi kubwa katika kuunganisha Zanzibar na Tanganyika, akiwa pamoja na Raisi Nyerere, Raisi Karume na Waziri Kiongizi Hanga. Hii ilikuwa ni baada ya mapinduzi ya Zanzibar.

Wakati wa wanajeshi wa kikosi cha Calito walipoasi mwaka 1964 Kambona alikuwa msuluhishi mkuu kati ya serikali na wanajeshi hao. Nyerere na Kawawa walienda mafichoni Kigamboni. Baada ya siku tatu za majadiliano Kambona aliafiki kuongeza kasi ya kuwawezesha waafrika kushika hatamu jeshini.

Katika mahojiano na gazeti la Daily Telegraph la London Kambona alisema, ‘baada ya kuwatuliza wanajeshi nilikwenda kuwatafuta viongozi wengine na kuwarudisha mjini kwa kutumia Land Rover yangu’. Hatimaye maasi hayo yalidhibitiwa kabisa na majeshi ya Uingereza na Nyerere alimsifu Kambona bushara na uaminifu wake.

Tofauti kati ya Nyerere na Kambona zilianza kujitokeza baada ya maasi ya wanajeshi. Nyerere alitaka kuanzisha mfumo wa chama kimoja nchini ili kuimarisha usalama. Kambona alipinga hoja hiyo kwa maelezo kwamba mfumo huo ungezorotesha uhuru wa watu na maendeleo ya demokrasia.

Hata hivyo, Kambona alishindwa bungeni; alikataa kusaini muswada (bill). Mwaka 1967, baada ya safari ya China ya mwaka 1965, Nyerere akiwa amependezwa na mfumo wa kikomonist wa Mao, alitaka kuanzisha mfumo kama huo kwa jina la ujamaa.

Dhana ya msingi ya mfumo wa ujamaa ilikuwa ni kuwahamishia watu katika vijiji vya ujamaa na kutaifisha viwanda ana mali. Kambona hakukubaliana na utaratibu huo kwa maelezo kwamba ungeongeza umaskini na udhibiti wa serikali kwa watu.

Alijiuzulu kutoka katika serikali na Chama na hatimaye yeye na familia yake walikimbilia Kenya na kisha Uingereza ambako walipatiwa uhifadhi wa kisiasa. Mara baada ya kuondoka mali za Kambona zilichukuliwa.

Ndugu zake wawili, waliwekwa kizuizini bila ya kufikishwa mahakamani na kufungwa kwa zaidi ya miaka kumi. Wanafamilia wengine walinyanyaswa na kuwekwa kizuizini. Wengine kati yao walibambikiziwa kesi za uhaini, wakafikishwa mahakamani na kisha kufungwa na serikali.

Kati yao walikuwa Bibi Titi ambaye alipigania uhuru pamoja ana Nyerere na alikuwa kiongozi wa jumuia ya kina mama. Alikuwepo pia Michael Kamaliza ambaye alikuwa mwanaharakati wa chama cha wafanyakazi, mwanachama wa TANU na waziri.

Wengine ni pamoja na Gray Mattaka, John ana Eliya Chipaka na Prisca Chiombola. Kambona alituhumiwa kuwa kiongozi wa wahaini wakati akiwa London na alihukumiwa bila kuwapo. Watuhumiwa hatimaye walikata rufaa katika mahakama kuu ya Afrika Mashariki na wakaachiwa huru.

Hata hivyo, baadae walikamatwa na serikali na kufungwa tena. Kambona alituhumiwa kuwa aliiba pesa nyingi sana zikiwa ni mali ya umma, kitu ambacho Kambona alikataa katika taarifa yake na waandishi wa habari Septemba 6 huko London 1967.

Tuhuma hizo zilisema kuwa ‘’ Kambona amekutwa na pesa nyingi sana kama karanga alipopekuliwa katika Uwanja wa ndege Embakasi Nairobi’’ Hata hivyo Kambona katika taarifa yake kwa waandishi wa habari alikanusha kuhusika na tuhuma hizi na badala yake akaipa serikali ya Tanzania kuiomba serikali ya Kenya kutoa ukweli juu ya jambo hilo- jambo halikufanyika.

Akiwa Londoni Kambona aliishi maisha ya shida na dhiki. Katika mwaka 1982 ndugu zake Kambona na Otini Kambona walifunguliwa kutoka kizuizini baada ya juhudi za waziri mkuu wa New Zealand Robert Muldoon. Katika mwaka 1990 Kambona akiwa na matumaini makubwa ya mabadiliko ya kisiasa katika Tanzania hususani mabadiliko ya demokrasia, aliunda chama kiitwacho Tanzania Democratic Alliance.

Wakati vyama vingi vilipoanzishwa Tanzania 1992 Kambona aliomba kurudi Tanzania. Serikali ya Tanzania ilimkatalia katakata na kudai kuwa Kambona hakuwa Mtanzania. Kambona badala yake aliomba Serikali ya Uingereza kumpa pasi ya kusafiria kurudi Tanzania. Hata hivyo Serikali ya Tanzania ilitamka kwamba pamoja na kupata pasi hiyo itamweka ndani pindi atakapoingia Tanzania.

Pamoja na msimamo huo wa Serikali, Kambona alitua kwenye ardhi ya Tanzania tarehe 5 september 1992. Hakuna mamlaka iliyomkamata bwana Kambona bali alipewa miezi mitatu awe amekamilisha utata wa uraia wake. Baada ya kurudi, Tanzania aliona kuwa harakati za kuelekea kwenye demokrasia ya kweli zilikuwa zikienda kwa mwendo wa kinyonga.

Hata hivyo Kambona hakuweza kujihusisha kwa kiasi kikubwa na siasa kutokana na matatizo ya kiafya hususani shinikizo la damu. Hatimaye Oscar Kambona alifariki akiwa katika matibabu mjini London mwezi Juni 1997.

Mdogo wake Otini Kambona naye alifariki katika kipindi hichohicho kutokana na magonjwa ya moyo. Wote wawili walizikwa Tanzania, na serikali ya Tanzania iligharimia gharama zote za usafirishaji miili ya marehemu ndugu hawa.

Oscar Kambona ameacha mke na watoto wawili. Mtoto wao wa kwanza Mosi Kambona aliuawa mjini London katika mazingira ya kutatanisha. Roho ya Oscar Kambona na ndugu na jamaa wote waliotangulia MWENYEZI MUNGU aziweke pema peponi, Amin.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom