Ukweli ni mchungu na Ukweli ni usemwe...

Source07

Senior Member
Oct 5, 2018
196
352
Kwenu wanabodi!

Tangu Rais avunje mkataba wa ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo kwa kile kinachodaiwa kuwa ni mkataba mbovu ambao tungeishia kuona tunaliuza Taifa kwa wachina basipo kujua Lakin basi kuna ukweli ambao unafichwa,unafichwa kwa kile kinachoitwa Uzalendo wa Mh.Rais!

Hapana huu ukweli nilazima usemwe hatakama unauma,ukweli wenyewe mpaka tumefikia hatua yakuingia hiyo mikataba mibovu yote nikutokana na Serikali za CCM!

Kwanini mnaacha kusema kua Serikali za Ccm ndio zimefanya hayo yote Bali mnaishia kumpongeza Rais kwakitu ambacho wakati kinapitishwa alikua miongoni mwa wale waliokipitisha??.

Hapana nitusema waziwazi CCM inalihujumu Taifa!..Ningekua mstari wa mbele kumpongeza Rais kama hiyo mikataba iliingiwa na Serikali za Upinzani!..lakin la hasha ni CCM wenyewe kwann tuwapongeze?

Je, nimangapi yapo nyuma ya pazia tusioyajua yenye madudu kama haya?kwahili La Bandari bado mnaimani na ujenzi wa SGR?

Bado mnaimani na ujenzi Stiglers Gorge?Bado mnaimani na ununuzi wa Mandege tena kwa Cash? Bado mnaimani na ujenzi wa uwanja wa ndege kule Chato?

Yapo mengi yakutafakari kuliko kupongeza hili tatizo walio lisababisha wenyewe..!

Wakipaza Sauti wapinzani kuhoji utasikia wametumwa na MABEBERU,wakitokea watu kuhoji wanatekwa na kuambiwa sio watanzania au ndio kusema ni collective Responsibility kwamba wakti ni Waziri tena wa Ujenzi aliamua kukaa kimya nakulipitisha hili kwavile hakua na nguvu zaidi ya Bosi wake JK?

Hapana nimeshindwa kuelewa kabsa.

Nawasilisha Hoja!
 
Hueleweki, kwahiyo ulitaka Rais aache Kama ilivyo kwa kua nae ni ccm?
Wewe laumu, sisi tunapongeza hatua hiyo aliochukua rais atokanae na ccm
Hapana lengo nikutaka kuwepo sasa na Uwazi nsiyo kusubiri Rais ajae atuonyeshe madudu ya mtangulizi wake then na sisi tufarahie...kingine hili nilakujifunza kua Serikali za CCM siyo zakuaminiwa..
 
Si kila jambo huwekwa hadharani, hata hizo serikali zilizoendelea za UK, America and his allies zinaendeshwa kwa usiri, usiri hauepukiki katika kuendesha serikali, kinachotakiwa ni kwa viongozi kutanguliza maslahi ya nchi kwanza kabla ya kitu chochote kile
 
Wakati hiyo miradi ya wizi ikipitishwa lugha ilikuwa ni hiyo hiyo kuweka maslahi ya umma mbele. Hilo ndio lilichangia rais wa sasa kukaa Kimya. Leo tunashangaa anaposema huo mradi haukuwa na maslahi kwa umma wakati alikaa kimya! Je tutaamini vipi hii miradi ya ujenzi anayofanya sasa kwa mikopo ni ya maslahi ya umma na sio kusaka political millage?
 
WaTZ inafaa tuingizwe kwenye historia kama taifa la watu wa aina yake;
- Tunaambiwa Ccm ni ile ile.
- Kupitia ccm tunaambiwa tumeibiwa sana havielezeki.
- Tuliingizwa mikataba ya kijinga mmno.
- Tutaisoma namba.
- Tumenyimwa katiba mpya ingeyozuia madudu mengi.
Lakini bado tunaitetea na kuipigia vigelegele na tunaichagua kwa kishindo tena siyo na wajinga pekee bali hata wasomi.
Hii ndiyo TZ ya hayati mwl. Nyerere.
 
Si kila jambo huwekwa hadharani, hata hizo serikali zilizoendelea za UK, America and his allies zinaendeshwa kwa usiri, usiri hauepukiki katika kuendesha serikali, kinachotakiwa ni kwa viongozi kutanguliza maslahi ya nchi kwanza kabla ya kitu chochote kile
wewe ni mwongo tena umeitaja UK unaijua vizuri system ya hiyo au unataka kufurahisha genge la ma ccm wenzio hamnazo Serikari ingie mkataba halafu ufichwe no.10 usipelekwe bungeni thubutuuuu acha uongo wewe.
 
kwa mfumo wa CCM JPM asingeweza kunyanyua mdomo na kumpinga mwenyekiti wake kama vile tu akina kabudi leo wanavyo sifia kila kitu anachokifanya! kwahiyo tatizo ni CCM! hawana uoga wa kuwajibishwa na wananchi, ndio maana ni muhimu sana kuuvunja huo mwiko na kuwapa upinzani nchi ili CCM ijifunze.
 
Sasa kama kweli unaelewa maana ya Collective responsibility kuna haja gan yakumshambulia Magufuli? Sio kila linalopitishwa na Baraza la Mawaziri kila Waziri anakubaliana nalo, wengine wanapinga lkn nguvu ya wengi ikishinda wakitoka kikaon lao moja, otherwise nna wasiwasi kama unaelewa maana ya Collective Responsibility
 
WaTZ inafaa tuingizwe kwenye historia kama taifa la watu wa aina yake;
- Tunaambiwa Ccm ni ile ile.
- Kupitia ccm tunaambiwa tumeibiwa sana havielezeki.
- Tuliingizwa mikataba ya kijinga mmno.
- Tutaisoma namba.
- Tumenyimwa katiba mpya ingeyozuia madudu mengi.
Lakini bado tunaitetea na kuipigia vigelegele na tunaichagua kwa kishindo tena siyo na wajinga pekee bali hata wasomi.
Hii ndiyo TZ ya hayati mwl. Nyerere.
Hahaa.. watz tupelekwe kwenye 'Museum of Human History', tuwe katika maonesho, kama binadam wenye akili ndogo sana..
 
Kwenu wanabodi!

Tangu Rais avunje mkataba wa ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo kwa kile kinachodaiwa kuwa ni mkataba mbovu ambao tungeishia kuona tunaliuza Taifa kwa wachina basipo kujua Lakin basi kuna ukweli ambao unafichwa,unafichwa kwa kile kinachoitwa Uzalendo wa Mh.Rais!

Hapana huu ukweli nilazima usemwe hatakama unauma,ukweli wenyewe mpaka tumefikia hatua yakuingia hiyo mikataba mibovu yote nikutokana na Serikali za CCM!

Kwanini mnaacha kusema kua Serikali za Ccm ndio zimefanya hayo yote Bali mnaishia kumpongeza Rais kwakitu ambacho wakati kinapitishwa alikua miongoni mwa wale waliokipitisha??.

Hapana nitusema waziwazi CCM inalihujumu Taifa!..Ningekua mstari wa mbele kumpongeza Rais kama hiyo mikataba iliingiwa na Serikali za Upinzani!..lakin la hasha ni CCM wenyewe kwann tuwapongeze?

Je, nimangapi yapo nyuma ya pazia tusioyajua yenye madudu kama haya?kwahili La Bandari bado mnaimani na ujenzi wa SGR?

Bado mnaimani na ujenzi Stiglers Gorge?Bado mnaimani na ununuzi wa Mandege tena kwa Cash? Bado mnaimani na ujenzi wa uwanja wa ndege kule Chato?

Yapo mengi yakutafakari kuliko kupongeza hili tatizo walio lisababisha wenyewe..!

Wakipaza Sauti wapinzani kuhoji utasikia wametumwa na MABEBERU,wakitokea watu kuhoji wanatekwa na kuambiwa sio watanzania au ndio kusema ni collective Responsibility kwamba wakti ni Waziri tena wa Ujenzi aliamua kukaa kimya nakulipitisha hili kwavile hakua na nguvu zaidi ya Bosi wake JK?

Hapana nimeshindwa kuelewa kabsa.

Nawasilisha Hoja!

Kama hoja yako ni hii utapata shida sana

CCM inabadilika kama kinyonga na ndio silaha ya wao kukaa madarakani milele yote nchi hii

kama JPM anasema hayo ndani ya CCM hauoni ni jema sana??? kama angekaa kimya kwa mfano ungefanya nini??

wewe ni dhaifu, huna unaloweza kufanya!!! waachie CCM wakuburuze utakavyo

Nyerer kamsema ma kumfokea Rais mwinyi akiwa mdarakani!!!!!

At least furahia hii demokrasia ndani ya CCM!!!
 
Yes, madudu yote haya ni CCM, na CCM ni li zimwi linaloitafuna nchi yetu miaka nenda, miaka rudi, lakini hili ndilo zimwi likujualo, halikuli likakwisha, lazima litakubakiza.

Kwavile kuna mazimwi wengi, Watanzania tumemua kuendelea kulichagua, zimwi likujualo.

Na uchaguzi wa serikali za mtaa unakuja mwaka huu na uchaguzi mkuu mwakani, kazi ni moja tuu, unachukua, unaweka, waa...!.
P
 
Back
Top Bottom