Ukweli ni kwamba, wote tunachepuka

Ukweli ni kwamba, wote tunachepuka

kama ni ukweli,basi ukimwi haupo,haíwezekani gesti zinajaa watu wanafanya zinàa kila siku halafu tusiwe tumekufa kwa ukimwi,no way
 
NNA WIVU SANA NA MKE WANGU
IMEFIKA HATUA KILA BAADA YA LISAA MOJA NAMPIGIA SIMU KUJUA KAMA YUPO NYUMBANI

JE NI NJIA SAHIHI?
IF NOT NIPENI MBINU

N:B NNA WIVU MPK NAHISI KUPAGAWA
 
Kabla ya kuoa/ kuolewa umekua ukilala na wanaume/ wanawake kwa odadi kubwa tu. Ni Nini kinakuzuia kuendelea na njia hiyo baada ya ndoa?
 
Wanandoa wote wanachepuka, mimi mmoja wapo, mwenzangu sijui, sijawahi kumdaka ila simuamini.

Suala la usaliti kwenye ndoa ni kwa wote, japo katika 100% wanawake nawapa 30% wanaume 70%.

Kimbembe ni pale mwanamke anapodakwa, hakuna msamaha, ila mwanaume akidakwa yanazungumzika.

Nafikiri hili ni janga kubwa sana kwa sasa, kama sisi tu wazazi, viongozi wa dini tunachepuka, vipi vizazi vyetu tunaviandaa aje?

Ni nasaa zipi tutawapa watoto wetu, juu ya masuala ya ndoa? Kataa ndoa wanahaki ya kukataa ndoa, ni kina nani wanawashawishi kuyaishi maisha ya ndoa?

Hawa kataa ndoa ndio wanaochepuka na wake/waume za watu, utamwambia nani aoe wakati kuna madudu wanayaona?

Wazazi, viongozi wa dini, kuna kazi kubwa hapa, huko mbele msishangae ndoa zisiwepo kabisa, watu wanatiana mimba kila mtu alee kivyake.
SIku zote mtu akiwa anafanya jambo huwa anaamini kila mtu anafanya hivyo, au anapaswa kufanya hivyo.

Anahisi kama hufanyi kam yeye basi wewe lofa fulani hivi. Wewe kuwa mchepukaji sio evidence ya kuprove assumption yako.
 
Back
Top Bottom