Ukweli ni kwamba sizipendi shule za binafsi

Ukweli ni kwamba sizipendi shule za binafsi

Barbarosa

JF-Expert Member
Joined
Apr 16, 2015
Posts
22,583
Reaction score
27,838
Huwa nakereka sana pindi nionapo picha kwa mfano watoto wa Shule za binafsi wakitembelea Bunge letu, sipendi kabisa sema sina uwezo wa kuwazuia

Ningefarijika sana kama Watoto wetu wa Shule za Kata tu ndo wangeruhusiwa kufika Bungeni kwa gharama ya Seriklai, hao wa Shule za binafsi wakitaka walipie, binafsi hizi Shule ukiondoa zile za Wazazi na taasisi za kidini, zisifagilii kabisa yaani
 
Lakini zina msaada kwa serikali kwani zilizopo za serikali hazitoshi
 
Wengi hawazipendi hizo shule mkuu, kwanza gharama kubwa. Lakini ubovu wa shule za umma ndio umesukuma na kuchochea uwepo wa hizo shule.

Serikali ikiboresha kiwango cha elimu na kuhakikisha maslahi ya watumishi yapo sawa, shule binafsi nyingi zitakosa wateja.

Lakini nafikiri uhuru na fursa ya kutembelea bunge ipo kwa shule zote. Ni jambo la kujiandaa tu na mipango ya shule husika.
 
Mwisho wa siku zinawahudumia watanzania kwa manufaa ya taifa....sema hata jiwe hapendi sekta binafsi sijui ugonjwa huu umeanza lini, halafu shule kubwa za serikali nyingi zilikuwa za binafsi ( dini)
 
Huwa nakereka sana pindi nionapo Picha kwa mfano watoto wa Shule za binafsi wakitembelea Bunge letu, sipendi kabisa sema sina uwezo wa kuwazia, ningefarijika sana kama Watoto wetu wa Shule za Kata tu wangeruhusiwa kufika Bungeni kwa gharama ya Seriklai, hao wa Shule za binafsi wakitaka walipie, binafsi hizi Shule ukiondoa zile za Wazazi na taasisi za kidini, zisifagilii kabisa yaani, ...
Acha roho mbaya kwanza
 
watoto wa shule za kata hawa utawajua tu!
 
Huwa nakereka sana pindi nionapo Picha kwa mfano watoto wa Shule za binafsi wakitembelea Bunge letu, sipendi kabisa sema sina uwezo wa kuwazuia, ningefarijika sana kama Watoto wetu wa Shule za Kata tu ndo wangeruhusiwa kufika Bungeni kwa gharama ya Seriklai, hao wa Shule za binafsi wakitaka walipie, binafsi hizi Shule ukiondoa zile za Wazazi na taasisi za kidini, zisifagilii kabisa yaani, ...

Msidanganye watu. Mnataka watoto wetu wasome shule za kata kusudi muendelee kuwatawala milele! Janja yenu tunaijua. We will do whatever it takes to acquire best education for our kids. So that they bit you guys at your game. Ukitaka uendelee kumtawala mwananchi na asijitambue..... mnyime ELIMU BORA. Hata hao akina Mwigulu wanaovaa bendera shingoni kila siku..wakitudanganya na uzalendo uchwara.......kawaulize wanae wanasoma wapi. Usisahau kuleta jibu hapa.
 
Sawa hilo sina shida nalo wasomeshini watoto wenu mnakotaka lkn ninachotaka ni Serikali yetu itoe upendeleo maalumu kwa Shule zetu za Kata kwenye kila kitu, kuanzia mikopo mpaka ajira!
 
WATOTO WETU WANASOMA SHULE ZA BINAFSI ULAYA NA NCHI NYINGINE ZA DUNIA YA KWANZA AU PALE IST DSM. TUKISHINDWA SANA BASI WANASOMA PALE MAPENE BOYS/GIRLS AU MARIAN AU KAIZEREGE, ORODHA NDEFU. SASA KAMA JANGWANI INASHIKA MKIA UNADHANI MIMI MBUNGE NITAPELEKA MTOTO PALE? NAUMWA?
 
Sawa hilo sina shida nalo wasomeshini watoto wenu mnakotaka lkn ninachotaka ni Serikali yetu itoe upendeleo maalumu kwa Shule zetu za Kata kwenye kila kitu, kuanzia mikopo mpaka ajira!
TUENDAKO AJIRA ITAKUWA BASED ON COMPETENCE, SBB SERIKALINI HAKUTAKUWA NA NAFASI KIVILE, HIVYO SOKO LA SEKTA BINAFSI NDIO LITAPOKEA KILICHO BORA. USISAHAU TEKNOLOJIA INA CHUKUA NAFASI ZAIDI TUENDAKO.
 
TUENDAKO AJIRA ITAKUWA BASED ON COMPETENCE, SBB SERIKALINI HAKUTAKUWA NA NAFASI KIVILE, HIVYO SOKO LA SEKTA BINAFSI NDIO LITAPOKEA KILICHO BORA. USISAHAU TEKNOLOJIA INA CHUKUA NAFASI ZAIDI TUENDAKO.

Ningekuwa mimi ndo Raisi wa nchi ningeweka vizuizi na vihunzi virefu zaidi kwa watoto waliosoma Shule binafsi (ukiondoa wazazi na taasisi za Kidini) kwenye kila kitu hata ajira kwa watu binafsi pia kama Serikali unaweza kuweka vihunzi vikawa virefu zaidi klk kwa wale watoto wa Shule za Kata!
 
Zingine zina saidia na Ndio zinazofua Vyuma.
 
ata mimi sizipendi shule za magari ya njano, lakini sujui ni kwanini wanapewa kipaumbele sana kwenye uwakilishi wakielimu
kuna watoto kwenye shule za kata na vipaji wapo smart sana lakini sijawai kuona wakitembea tembea bungeni huko, sijui kwanini
 
Siwezi peleka mtoto wangu shule ya serikali, nimepitia huko kuanzia darasa la kwanza hadi chuo... Taaabu niliyoipata siwezi ruhusu wanangu wawe hivyo pia, I will do whatever it takes to make sure my kids get a good and quality education
 
Back
Top Bottom