Ukweli ndo huu: Kama mimba ni kero, wekeni vijiti

motonkafu

JF-Expert Member
Dec 2, 2015
1,019
705
Kama Mimba ni Kero, Wekeni Vijiti

Nimeamka na hasira leo baada ya www.bbcswahii. com katika kipindi chao cha Amka na BBC asubui ya leo tarehe 28/06/2016 kutangaza kuwa vitendo vya utoaji mimba vimekithiri nchini Tanzania ambapo inakadiriwa wanawake na wasichana zaidi ya laki nne wanatoa mimba kwa mwaka hivyo kwa maana halisi taifa linaingia hasara ya kupoteza binadamu laki nne kila mwaka. Na sauti ya msichana mmoja inasikika katika kipindi hicho akikiri kuwa alishauriwa na wenzake kutoa mimba baada kubakwa kwa kumeza majani ya chai, rangi za nguo na mitishamba mingine lakini ikashindikana.

Sasa ni vizuri wazazi, walezi, viongozi, waelimishaji rika, washika dau na wananchi wote kwa ujumla tukalielewa hili kwamba huu mchezo watu wanaupenda na wanafanya sio wanawake sio wanaume, sio wasichana sio wavulana hata wazee wamo katika hili tusijivike upofu wakati tunaona, tukitaka tuwaondoshe wanawake na wasichana katika dhambi hii ya kuua bila kukusudia tuwe wawazi tu tuwambie ukweli ama waweke vijiti, wachome sindano ikiwezekana wameze vidonge vya kuzuia mimba kila siku kabla hawajakutana na wapenzi, vimada na michepuko yao manaake ukweli ni kwamba hawa watu kutumia kondom wameshindwa ama pengine kwa kuzidiwa na utamu wa mchezo, au chuki binafsi dhidi ya kifaa hiki kilichotengenezwa mahususi kabisa kuzuia shahawa za mwanaume zisikutane na za mwanamke wakati wa kurushana roho na kuepusha hatari ya kutungwa mimba zisizotarajiwa. Na kuhesabu karenda ndo hawawezi kabisa wamama na dada zetu na hii ikichangiwa na uzembe wa watanzania wengi katika kutunza kumbukumbu za kichwani au za maandishi.

Hakuna mzazi, mlezi anaependa binti yake apate mimba wakati anagharamia mamilioni ya ada shuleni, chuoni japokuwa wengine wanasoma bure lakini napo wanafukuzwa shule na mimi nikishuhudia wanafunzi watatu ninaowafahamu wakifukuzwa shule kwa kubeba mimba ndani ya kipindi cha kati ya miezi miwili ama mitatu huku waliowatunga hizo mimba kutokomea kusikojulikana. Hata serikali inachukia sana na inaahidi kuwatafuta watungaji hao wa mimba mpaka wapatikane lakini kuna msemo wa waswahili unakera hapa 'maji yakimwagika hayazoleki' sasa kwa nini tusizuie mapema.

Sasa wazazi na walezi kwa nini tusijitoe mhanga wa kuwatia vijiti hawa watoto ili tusahau kesi za mimba, tusahau wasichana kukatishwa masomo, na tuwapunguzie wazazi presha. Tusijifanye waoga katika hili na serikali iandae mpango wa kuwatia vijiti wanafunzi wote mashuleni wenye uwezo wa kubeba mimba manaake adhabu zinazotolewa ama hazitoshi au hazifanyiwi kazi kwasababu tatizo bado lipo. Hapa naungana na mbunge /nimemsahau jina/ ambae juzi alisema miaka thelathini haitoshi, fimbo kumi na tano hazitoshi ni bora mtunga mimba ya mwanafunzi alipe milioni kumi na tano kama hana afilisiwe mali ikiwemo nyumba ili alipwe fidia mtoto aliekatishwa masomo.

Najua wanawake na wasichana wengine watakuja na utetezi wa kusema njia za uzazi wa mpango za kisasa zina madhara mengi ikiwemo kubadilisha mzunguko wa hedhi hivyo kumuudhi mtumiaji, kunenepesha mwili, kuchelewa kupata mimba utakapohitaji na usumbufu wa kumuona daktari mara kwa mara kuomba ushauri wa kuchoma sindano lakini hizo kero ni ndogo sana ukilinganisha na maumivu ya kuchokonolewa na machuma, kutupa watoto, kufukuzwa shule, nyumbani ama kuvunja ndoa.

Nchi za wenzetu wamedhibiti haya matatizo kwa kuwa ni wawazi kwa mabinti zao, dada zao, na wanawake wao kuwashauri watumie njia za uzazi wa mpango ili kuzuia fedheha hii.

Makala hii fupi imeandikwa tarehe 28/6/2016
 
Tatizo hatupendi kuukubali ukweli na hatupendi kukubali kwamba tumeacha misingi sahihi ya maisha.

Misingi ya mababu zetu, misingi ya maandiko matakatifu. Sijui ni udhaifu Wa haya maandiko kutokuendana na wakati au kutokubaliana na ukweli na hali halisi??

Jamii na wazazi tunapaswa kuwafundisha vijana namna zote kukabiliana na hili

Namna ya kiimani kwamba kutiii amri kumi ikiwemo ile ya sita kuishi katika hofu ya mungu na vile vile tusiwe na ugumu Wa kuwapa namna ya kidunia kupambana na hili kutumia njia za uzazi Wa mpango.
Ugumu Wa mioyo yetu kutokana na vifungo vya màandiko na utamaduni ndio chanzo cha haya yote.
 
Hili swala la utoaji mimba ni swala nyeti sana katika mustakabali mzima wa mwenendo wa jamii yetu. Hizi mimba zinatolewa kwasababu wasichana wanaelewa hawana uwezo wa kutunza watoto na zilipatikana bahati mbaya. Zikiachwa mimba hizi kunauwezekano mkubwa wa kuwa na watoto wengi wa mitaani.

Hapo mwanzo vijana walikuwa wanaolewa wakiwa wadogo, zile chemical changes za ujana zinamkuta msichana akiwa kwa mume wake. Kutokana na maendeleo ya binadamu vijana wa umri wa kuolewa wanakuwa bado wako masomoni.

Elimu ya uzazi itolewe na wazazi kwa watoto wao, mashuleni pia katika nyumba za ibada. Kuwe na vituo vya afya vinavyoweza kuwasaidia wasichana kupata kinga za mimba kama wameanza mapenzi wakiwa shule.

Serikali ijenge mazingira ya kuendelea na elimu kwa wale waliopata mimba wakiwa mashuleni hii itasaidia kupungua kwa utoaji mimba.

Inachochekesha kila mwanaume anataka kuoa binti fresh ambae hajatoa mimba na hao hao ndio wanavizia visichana vya shule.
 
Wazazi siku hizi wako busy sana kiasi ambacho hakuna anaye pata mda wa kukaa na watoto kuwaeleza njia zilizo sahihi kufuata..Baba anatoka kazini anapita Bar anarudi nyumbani saa 4 na ndiyo routine hiyo mama yeye anafika hme saa 11 ndiyo anaanza kuandaa msosi hadi saa 12 kamaliza yuko busy na simu kwenye magroup ya wsap na facebook hataki hata kelele za watu utadhani anafuatilia BBC kumbe habari za wema na diamond.
 
Nakubaliana na wewe Mkuu, ili kukabiliana na hili tatizo ni vyema elimu ya afya na uzazi wa mpango ikatolewa vya kutosha ili kupunguza tatizo.Lakini mwanafunzi/binti ambao wamekwisha jua kuwa wamekwisha fungwa uzazi kwa vijiti au vyovyote huwa wanakuwa Malaya sana si wanajua hawawezi kushika mimba. Me nafikiri wawe wanaachwa hivyo hivyo ili wawe waangalifu na kuchukua tahadhari
 
Wazazi siku hizi wako busy sana kiasi ambacho hakuna anaye pata mda wa kukaa na watoto kuwaeleza njia zilizo sahihi kufuata..Baba anatoka kazini anapita Bar anarudi nyumbani saa 4 na ndiyo routine hiyo mama yeye anafika hme saa 11 ndiyo anaanza kuandaa msosi hadi saa 12 kamaliza yuko busy na simu kwenye magroup ya wsap na facebook hataki hata kelele za watu utadhani anafuatilia BBC kumbe habari za wema na diamond.
Tuanze na wewe..utamwambiaje mwanao kuhusu hizo mimba
 
Swala la utoaji mimba kiukweli asilimia kubwa ni hawa mabinti zetu, na hii sio kingine ni utandawazi jamani. We utamwelekeza lakini yeye anajua kuliko wewe mzazi, na hapo ndo ugumu unaanzia huwezi kumchunga binti muda wote jamani, kama ni mtoto wa kusikia atakusikiliza mzazi lakini kuna hawa wengine jamani wazazi wanaongea mpaka lakini hawasikii wala hawaambiwi na ukweli hata sie tunajua wapo wa aina hiyo. Na kampani hizi ndo zinachangia kwa kiasi kikubw watoto kuharibika jamani, yaani ni kila mtu sasa kujivika suala la kulea awe mwanao au la, awe ndugu au la. Tunakutana nao mitaani huko jamani, kila mmoja awajibike na sio mzazi peke yake na hapo ndipo tunakosea. Utakuta katoto ka form one kamerusha picha Facebook huko nusu uchi mibabu inamsifia yeye anaona saaafi, wakati huo mzazi wake hata habari hana, sasa wewe uliyeona kwa nini usikemee mara moja?? Mabadiliko yanaanza na sisi wenyewe.
 
Back
Top Bottom