DnS8elpmis
New Member
- Jul 26, 2022
- 3
- 1
Ukweli ni kwamba
Hakuna kisicho wezekana,
Ukweli ni kwamba,
Kila mbuzi, atakula kwa urefu,
Wa kamba yake.
Ukweli ni kwamba,
Asiyesikia la mkuu,
Huvunjika guu,
Ukweli ni kwamba mabadiliko,
Daima hukutana na upinzani.
Ukweli ni kwamba,
Ng'ombe wa maskini hazai,
Ukweli ni kwamba,
Umaskini ni tabia, sio hali.
Ukweli ni kwamba,
Matatizo tumeumbiwa binadamu,
Ukweli ni kwamba,
Dhahabu ya mmoja, ni uchafu kwa mwingine.
Ukweli ni kwamba,
Utavuna ulichokipanda,
Ukweli ni kwamba,
Heri moja ya leo, kuliko kumi ya kesho.
Ukweli ni kwamba,
Mwenye macho haambiwi tazama,
Ukweli ni kwamba,
Usitukane mamba,
Kabla hujavuka mto.
Ukweli ni kwamba,
Siku hazilingani,
Ukweli ni kwamba,
Hakuna jipya chini ya jua.
Ukweli ni kwamba,
Nyota njema huonekana asubuhi,
Ukweli ni kwamba,
Hujafa, hujaumbika.
Ukweli ni kwamba,
Akufukuzaye hakwambii toka,
Ukweli ni kwamba,
Moyo wa mtu, ni usiku wa giza totoro.
Ukweli ni kwamba,
Subira, yavuta heri,
Ukweli ni kwamba,
Ngoja ngoja huumiza matumbo.
Ukweli ni kwamba,
Haraka! Haraka! Haina baraka,
Ukweli ni kwamba,
Chelewa! Chelewa! Utakuta mwana si wako.
Inategemea umesimama wapi.
Hakuna kisicho wezekana,
Ukweli ni kwamba,
Kila mbuzi, atakula kwa urefu,
Wa kamba yake.
Ukweli ni kwamba,
Asiyesikia la mkuu,
Huvunjika guu,
Ukweli ni kwamba mabadiliko,
Daima hukutana na upinzani.
Ukweli ni kwamba,
Ng'ombe wa maskini hazai,
Ukweli ni kwamba,
Umaskini ni tabia, sio hali.
Ukweli ni kwamba,
Matatizo tumeumbiwa binadamu,
Ukweli ni kwamba,
Dhahabu ya mmoja, ni uchafu kwa mwingine.
Ukweli ni kwamba,
Utavuna ulichokipanda,
Ukweli ni kwamba,
Heri moja ya leo, kuliko kumi ya kesho.
Ukweli ni kwamba,
Mwenye macho haambiwi tazama,
Ukweli ni kwamba,
Usitukane mamba,
Kabla hujavuka mto.
Ukweli ni kwamba,
Siku hazilingani,
Ukweli ni kwamba,
Hakuna jipya chini ya jua.
Ukweli ni kwamba,
Nyota njema huonekana asubuhi,
Ukweli ni kwamba,
Hujafa, hujaumbika.
Ukweli ni kwamba,
Akufukuzaye hakwambii toka,
Ukweli ni kwamba,
Moyo wa mtu, ni usiku wa giza totoro.
Ukweli ni kwamba,
Subira, yavuta heri,
Ukweli ni kwamba,
Ngoja ngoja huumiza matumbo.
Ukweli ni kwamba,
Haraka! Haraka! Haina baraka,
Ukweli ni kwamba,
Chelewa! Chelewa! Utakuta mwana si wako.
Inategemea umesimama wapi.
