Ukweli mchungu nilio ukubali ndo huu

Ukweli mchungu nilio ukubali ndo huu

Sheffer95

JF-Expert Member
Joined
Mar 16, 2020
Posts
274
Reaction score
771
Hapa karibuni nilileta thread inayosema " Hivi wanaume wenzangu mlifanyaje"
ukweli niliokuja kuujua ni kwamba kumbe yule mwanamke niliyetaka kumfanya mchepuko anafahamiana na mke wangu.

Na kwakifupi ana muheshimu sana kwasababu huko nyuma kidogo mke wangu aliwahi msaidia kum connect mahali akapata kazi nzuri sana kama mdogo wake, bahati mbaya sana yule binti akiwa kazini akaanza kutoka na bosi wa pale ambae mkewe na mke wangu walisoma pamoja Chuo kikuuu na walikuwa marafiki

Hivyo akafukuzwa kazi na mambo ya kuanza kudanga yakaanzia hapo na alizalishwa na mtu haeleweki.

Na kumbe kunikataa kote huko ni kwasababu, ana muheshimu sana mke wangu na pia hataki kum disappoint mara nyingine baada ya ile ya kwanza kumgombanisha na rafiki yake.

Na anasema aliapa ni heri awakubali wanaume wengine wote sio mm kwasababu hawezi kurejesha wema kwa ubaya.

Anyways, nimeamua kuheshimu maamuzi yake lakini nimemwambia asiishi kama mtu aliyekata tamaa.

Nimemwambia kumsaidia kama kuna biashara kafikiria kuifanya basi aniambie nimchangie mtaji afanye aache kutoka na vijana wa hovyo ambao hafananii kuwa nao.
 
Ikimbieni zinaa.....Shalom watu wa Mungu!
 
Bosi wa pale mkewe ni mkewangu tukueleweje we na bosi wa mkewako mnashare .kingine huruma sio malezi ye kakuomba umsaidie au ndiyo kujikweza tu
 
Hapa karibuni nilileta thread inayosema " Hivi wanaume wenzangu mlifanyaje"
ukweli niliokuja kuujua ni kwamba kumbe yule mwanamke niliyetaka kumfanya mchepuko anafahamiana na mke wangu.

Na kwakifupi ana muheshimu sana kwasababu huko nyuma kidogo mke wangu aliwahi msaidia kum connect mahali akapata kazi nzuri sana kama mdogo wake, bahati mbaya sana yule binti akiwa kazini akaanza kutoka na bosi wa pale ambae mkewe ni mke wangu walisoma pamoja Chuo kikuuu.

Hivyo akafukuzwa kazi na mambo ya kuanza kudanga yakaanzia hapo na alizalishwa na mtu haeleweki.

Na kumbe kunikataa kote huko ni kwasababu, ana muheshimu sana mke wangu na pia hataki kum disappoint mara nyingine baada ya ile ya kwanza kumgombanisha na rafiki yake.

Na anasema aliapa ni heri awakubali wanaume wengine wote sio mm kwasababu hawezi kurejesha wema kwa ubaya.

Anyways, nimeamua kuheshimu maamuzi yake lakini nimemwambia asiishi kama mtu aliyekata tamaa.

Nimemwambia kumsaidia kama kuna biashara kafikiria kuifanya basi aniambie nimchangie mtaji afanye aache kutoka na vijana wa hovyo ambao hafananii kuwa nao.
naona umemaliza kwa kusema vijana wa hovyo ambao hafanani nao ila umesahau kujiita mtu mzima hovyo ambaye hutulii na mkeo kazi kupepesa macho.
 
Back
Top Bottom