Muwindaji
JF-Expert Member
- Feb 28, 2015
- 245
- 206
Kimsingi, Dola inakua na mihimili mitatu, yaani Bunge, Serikali na Mahakama..
Kwa vile Ibara ya 8 ya katiba ya Jamhuri ya Tanzania 1977(Kama ilivyorekebishwa mara kwa mara) inasema mamlaka ya nchi yapo chini ya wananchi, Bunge ni mhimili muhimu sana kwasababu unawakilisha Sauti ya mamlaka halisi ya wananchi...
Moja kati ya kazi muhimu ya Bunge ni kuisimamia na kuikosoa Serikali ili ihakikishe inaweka maslahi ya wananchi mstari wa mbele...
Katika kulinda Uhuru na Haki za Bunge kufanya kazi yake vizuri, Bunge linajisimamia na linakua Bajeti yake huru(Kama ni msaada utakua ni kidogo sana kutoka kwa serikali)..
Bunge ni chombo huru..
Miezi kadhaa iliyopita, tulisikia TBC ikitangaza kwamba, inasitisha kurusha matangazo ya moja kwa moja kutoka bungeni(Live) kutokana na kile wanachokiita ukosefu wa pesa ya kurushia matangazo hayo, Tukumbuke kua TBC ni stesheni ya serikali, Mhimili mwingine kabisa wa dola, mhimili ambao Bunge lina kazi ya kuusimamia na kuukosoa...
Bila kujali kwamba maamuzi hayo ya serikali yalikua ni ya kisiasa au la, kuna maswali kadhaa ya kujiuliza;
1. Je, Bunge lenye bajeti yake inayojitegemea linashindwaje kutenga bajeti ya kuanzisha kituo cha kurushia matangazo yake moja kwa moja bila kutegemea favor kutoka kwa serikali?
2. Bunge ni mhimili ambao waliomo ni moja kati ya watu wanaopokea mishara na posho nono za kutisha, wabunge(kama kweli wanataka wananchi wao tuone wanavyofanya kazi zao vema) wanashindwaje kukata posho hizo na kuanzisha utaratibu wa kuanzisha kituo?
3. Kwa nature ya kazi za bunge(kuisimamia) serikali, walikua wanategemea nini kama sio hiki kinachoendelea?
4. Bunge linaendeshwa kwa kodi zetu, na serikali inaendeshwa kwa kodi zetu, Bunge kutegemea fedha za serikali halioni kua lina-parasite kodi za wananchi kote kote?
5. Bunge halioni kua kuendelea kuitegemea serikali kwenye matangazo ya live litashindwa kuiwajibisha serikali vizuri?
Wananchi Hatuungi mkono kitendo cha serikali kwa upande mmoja, lakini kwa upande mwingine, tunaunga mkono kwasababu Bunge lilinde uhuru wake kwa kuweza kujitegemea, (ni mfano wa baba anapomfukuza nyumbani mwanawe wa kiume aliyefika umri wa kujitegemea akapambane atengeneze maisha yake.)
Vile vile tukija kwenye kile wanachokiita uvunjifu wa Haki ya kupata Habari ni kweli inawezekana serikali wamevunja Haki hiyo, lakini Haki hiyo ni moja kati ya Haki ambazo utekelezaji wake unategemea rasilimali za nchi husika, Serikali inaweza kabisa ikajitetea kua imeshindwa kufanya hivyo kwasababu ya ufinyu wa bajeti yake!
Suluhisho pendekezwa:
Bunge lianzishe kituo chake cha kurushia matangazo ya moja kwa moja, kama zilivyo nchi zingine, mfano Uingereza.. Parliamentlive.tv - Commons... na liache kulia lia. Bunge lijitegemee ili liisimamie serikali vizuri.