Ukweli mchungu kuhusiana na mradi wa Stiegler's Gorge

Tatizo watu tunaingiza siasa kwenye taaluma.

Tatizo kubwa kwenye Tathimini za mazingira (Environmental Impact Assessment) zime base kwenye European Standards ambazo ni ngumu kwa nchi za kiafrika kuendana nazo.

Ikiwa Nchi za Africa zinataka kupiga hatua ni ngumu kufanya mifumo yake ifanane na ile ya ulaya kwa mara moja lazima ianzie chini na baadae ndo vitawezakana.

Tathmini ya mazingira (EIA) iliyofanywa kwenye mradi wa umeme wa stiglers gorge haukuzuia mradi kufanyika badala yake walitowa njia za kupunguza( minimize) au kuondoa ( mitigation measures) za madhara ya kimazingira ila njia zenyewe mbadala za kukabiliana nazo walitoa kama zile za nchi za ulaya ambao ikaonekana mradi utakuwa wa gharama kubwa zaidi kuliko budget iliyokuwepo.

Hakuna mradi wenye athari kubwa za kimazingira duniani kama mradi wa kuzalisha umeme kwa kutumia vinu vya nyuklia lakini ndo nchi zote zilizoendelea duniani utumia,hii ni kwakuwa zinaweza kugharamia njia za kupunguza na kutoa athari za kimazingira.

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Naona unabishana ili ulipwe fadhila.. Huyo Prof. alikuwa wa kwenu kabisa... Na aliwasiliana ripoti mliyoipenda... Please usiite report yake kuwa ni "nonsensical report"... Unadhalilisha mamlaka ya uteuzi!!
Una mapungufu! Nimekuomba EIA ni ya nani ukaleta taarifa ya OECD na UNESCO hiyo ndo EIA?
Tunajadili ubovu wa EIA na jinsi serikali ilivyoikataa, wewe unasema profesa ni wenu. Sisi akina nani. Nakwambia ni nonsensical report, unahamia bhla! bhla!

Sema tulijue jopo lilofanya EIA. Au unadhani huwa ni ripoti ya mtu mmoja? Yawezekana hawakuwa hata na sifa za kufanya EIA ya aina hiyo na bado kuwa watu munataka ripoti kama hiyo itumike. Shit happens!
 
Tatizo watu tunaingiza siasa kwenye taaluma.

Tatizo kubwa kwenye Tathimini za mazingira (Environmental Impact Assessment) zime base kwenye European Standards ambazo ni ngumu kwa nchi za kiafrika kuendana nazo.

Ikiwa Nchi za Africa zinataka kupiga hatua ni ngumu kufanya mifumo yake ifanane na ile ya ulaya kwa mara moja lazima ianzie chini na baadae ndo vitawezakana.

Tathmini ya mazingira (EIA) iliyofanywa kwenye mradi wa umeme wa stiglers gorge haukuzuia mradi kufanyika badala yake walitowa njia za kupunguza( minimize) au kuondoa ( mitigation measures) za madhara ya kimazingira ila njia zenyewe mbadala za kukabiliana nazo walitoa kama zile za nchi za ulaya ambao ikaonekana mradi utakuwa wa gharama kubwa zaidi kuliko budget iliyokuwepo.

Hakuna mradi wenye athari kubwa za kimazingira duniani kama mradi wa kuzalisha umeme kwa kutumia vinu vya nyuklia lakini ndo nchi zote zilizoendelea duniani utumia,hii ni kwakuwa zinaweza kugharamia njia za kupunguza na kutoa athari za kimazingira.

Sent from my iPhone using JamiiForums
Uko safi! Kuna watu hapa wanajidai kuyajua mazingira wakati hata hawajui ubovu wa EIA. Hawajui hata faida zake wao wanadhani EIA ina kazi ya kupambana na uharibifu wa mazingira. Waandikaji wetu wa EIA wenyewe nao ni kupata kipato tu, utaalamu ni mdogo ukilinganisha na mahitaji yao ya kifedha. Ripoti nyingi pale NEMC ni copy-paste kutoka kwenye internet. Professionalism ni zero!
 
Acha kupotosha watu wewe. Uharibifu gani wa mazingira uliofanywa pale.
Kemea hao ndugu zako wanaokata magogo hapo kijijini kwako kwa kuchoma mkaaa.
Kwa kifupi hakuna best project anayoifanya Magu Kama hiyo. Kati ya zote hiyo kwangu it's number one
uoto wa asili umeharibiwa, tatizo lako wewe na MATAGA wenzako mnajiona ni wazalendo sana hasamkivaa fulana za kijani na vibendera vya tanzania, upuuzi tu
 
Ukiwa na resources za kutosha, unaweza sasa kutumia nguvu ya kifedha kutoka resource inayositawi kukuza inayodorora. Hii study ya huyu profesa ni insha kama insha zingine. Miradi itembee, umaskini umichosha nchi
 
Kufanya kosa si kosa, bali kurudia kosa. Anasema wazungu walimaliza misitu yao na madhara wanayapata. Leo wanakushauri usirudie walichokifanya, unaona hawana akili. Ama kweli ujinga ni mzigo.
Tatizo wabongo wengi mnadandia Mambo kwa miheuko.
Wakati dunia inaubwa sehemu kubwa ya makazi yetu yalikuwa ni misitu waishiyo wanyama. Hao uko majuu washamaliza mapori yote, wanaongoza kwa air pollution. Wamefyeka misitu kikubwa ili waweke makazi ya watu. Leo hii sisi kufanya hili la kimaendeleo limekuwa nongwa?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kaitafute siwezi kukutafunia wewe siyo mtoto ila athari za kimazingira ni kubwa kuliko huo umeme wakujipendekeza wa bei cheee..... omba mola wako akupe siku nyingi zakuishi haya ninayokuambia utakuja kuyaona kama siyo kusikia wenzetu wenye elimu kubwa walituambia acheni hii ni hatari,nyie kwa ubishi ikaundwa kamati na mtukufu ili kujiridhisha majibu yakaja yaleyale katika report ya mabeberu ulitegemea kama ni mradi wa kipigaji kazi isifanyike? Mkiambiwa ooh..... mabeberu hawataki kuona tunaendelea mambo yakitaamu mnaingiza siasa kwa ajili ya matumbo ya watu wachache siyo? endelea kunufaika na mradi.
Mbona hukunisoma mkuu wangu 'The fact files'!

Unayo hiyo ripoti mkuu wangu. Kama unayo tafadhali, iweke nasi tuisome, na baada ya hapo tutakuwa na nafasi nzuri ya kuukataa mradi kwa uharibifu wake, au kuunga mkono kwa manufaa tunayodhani utaliletea taifa.

Sasa wewe mara unaniwekea lebo, ambayo andiko langu limeelezea wazi kuwa bila ripoti hiyo, sio sawa kuhukumu?

Tuwekee hiyo ripoti ya wataalam. Uwezo wa kuichambua tunao, na hapo ndipo tutakapoamua ni upande upi tuuunge mkono.
Hayo ya 'kunufaika' unayokimbilia ni dalili za kutokuwa na hoja.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kaitafute siwezi kukutafunia wewe siyo mtoto ila athari za kimazingira ni kubwa kuliko huo umeme wakujipendekeza wa bei cheee..... omba mola wako akupe siku nyingi zakuishi haya ninayokuambia utakuja kuyaona kama siyo kusikia wenzetu wenye elimu kubwa walituambia acheni hii ni hatari,nyie kwa ubishi ikaundwa kamati na mtukufu ili kujiridhisha majibu yakaja yaleyale katika report ya mabeberu ulitegemea kama ni mradi wa kipigaji kazi isifanyike? Mkiambiwa ooh..... mabeberu hawataki kuona tunaendelea mambo yakitaamu mnaingiza siasa kwa ajili ya matumbo ya watu wachache siyo? endelea kunufaika na mradi.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu 'The Fact Files',
Mimi najua kutafuta taarifa kama hizo, ni rahisi sana kwangu kuzipata, lakini sihitaji kufanya hivyo kwa sababu kadhaa:
1. Wewe umejitangaza mwenyew hapa kwamba ni "Thefact files"; unaelewa maana ya hilo? Kwa hiyo kama nilikuomba uweke ushahidi wowote usitake sasa kuruka kimanga. Kwa kufanya hivyo unajionyesha wewe ni mbabaishaji tu!
2. Kama umenisoma kwa utulivu katika bandiko hilo uliloni'quote' kijinga kijinga hapa, ungekuwa mwelewa wa haya mambo ungeelewa kuwa mimi sipingi kishamba umhimu wa kutunza mazingira yetu. Ninaelewa sana umhimu wa mazingira na naweza kukueleza kwa uhakika kabisa kwamba huna chochote unachoweza kunifundisha juu kulinda mazingira yetu.
3. Tofauti kubwa iliyopo kati yako na mimi kuhusu uelewa wa mazingira ni mkubwa, kwa sababu wewe unaonekana kuyaimba mazingira kama kasuku. Yaani huna tena akilini mwako uwezo wa kupima, kulinganisha na kuona uzito wa athari na uwezekano wa kuwepo njia za kuzipunguza au kuzizuia kabisa athari hizo ili taifa lifaidike na kinachozalishwa hapo (umeme wa nafuu zaidi). Wewe unachojua ni mipasho tu kama hiyo hapo juu ulivyoiweka.
4. Uingereza na nchi mbalimbali zilizoendelea, walichafua sana mazingira kabla ya kupata maendeleo waliyonayo leo.
Sitasema kamwe hapa kwamba na sisi inatupasa kuchafua mazingira ili mradi tupate maendeleo. Lakini leo hii, zipo njia za kutumia raslimali kama hayo maporomoko ya maji, na kama kuna athari zinazotokana na matumizi hayo njia zipo za kuzuia yasiwe makubwa.

Hao wakuu wanaotupigia kelele kuhusu miradi yetu hii wao wanaona njia moja tu, kusitisha miradi kama hiyo.
Hii miaka zaidi ya hamsini tangu tupate uhuru wa kwenda shule, kusoma na kujitahidi tuweze kupata akili za kuamua kipi ni kizuri kwetu au kibaya, kwa nini bado tusiwe na huo uwezo hadi tubaki tukiimba nyimbo wanazotufundisha hao wakubwa wanaotutupia vijisenti kdhaa ili kutupumbaza akili?.

Mkuu, 'The Fact Files', liishi jina lako kama lilivyo. Unajiaibisha kwa jibu kama hilo uliloweka hapo juu kunijibu mimi.
 
Back
Top Bottom