Ukweli mchungu: Kama wazazi wako hawakuwekeza kipindi ukiwa mtoto nyakati hizi utaziona ngumu sana

Kifaru86

JF-Expert Member
Apr 22, 2017
1,734
3,802
Katika maisha lazima tukubaliane wazazi wetu ambao tangu tukiwa watoto walijisahau hawakuwekeza nyakati hizi utaziona ngumu kwa sababu

1. Kama wazazi hawakufanikiwa kumiliki assets kama vile nyumba,viwanja,mashamba nyakati zile vitu vilikuwa bei rahisi basi kipindi hiki haya yote upambane uwafanyie haya yote

2. Kama hawakujengea mazingira ya kujiajiri au kuajiriwa basi nyakati hizi utaziona ngumu kwani kila kitu ili ufanye kinaitaji rasimali

3. Kama hawakufanikiwa kukutengenezea mazingira ikitokea umesoma na haujajiriwa nini unachotakiwa kukifanya

4. Kama hawakufanikiwa kujiwekea akiba ya badae wataishi vipi basi ni jukumu lako kuwasimamia maswala ya fedha kila siku kuwatumia

Haya tuendeleee kama una kuongezea
 
Mimi naishi na mama yangu hapa du yaani hata haka ka mshahara wangu anatamani akapokee yeye eti kisa alinihangaikia na ugomvi hapa home hauishi either na mke wangu au watoto wangu au house girl,yaani ni tabu mpaka nimekataa tamaa ya maisha
 
Hio no. 1 ni uongo tu kusema vitu vilikua bei rahisi,hata wewe miaka 20 ijayo watoto wako watakuuliza baba mbona hukujenga nyumba wkt huo ilikua ni gharama ndogo tu mil 30,mbona hukununua viwanja wkt vilikua bei ndogo mil 10 tu ungepata kiwanja lkn jiulize kama wkt huu hio pesa ni ndogo?
 
Hakuna wakati vitu vilikuwa rahisi, linganisha bei ya viwanja na mishahara ya wakati huo. Kwa kifupi sema kama wazee hawakuwa na malengo.

Wewe mwenyewe unajichanganya hapo.

Hawakuaje na Malengo wkt umesema mwenyewe mishahara ya kipindi hicho ni kiduchu.
 
Hio no. 1 ni uongo tu kusema vitu vilikua bei rahisi,hata wewe miaka 20 ijayo watoto wako watakuuliza baba mbona hukujenga nyumba wkt huo ilikua ni gharama ndogo tu mil 30,mbona hukununua viwanja wkt vilikua bei ndogo mil 10 tu ungepata kiwanja lkn jiulize kama wkt huu hio pesa ni ndogo?
Kuna wakati broo let's the truth speak
Yaani ukweli ubakie kuwa ukweliiiiii

Kuna storii zingine unakuta mzazi wako anakusimulia Mara ohooo miaka ya zamani tegeta ilikuwa pori au kimara kulikuwa pori serikali ulikuwa inatuforce tukae ukoo tukawa tunapakataa tukipewa tunauza ila saivi kumebadilika watu wamejenga lazima ujiulize hapo
 
Yaani wewe ni makalio. Kwa hiyo unadhani kuwahudumia wazazi ni hisani? Wangekuacha ukafa utapiamlo huku wao wakiwekeza mali zao za kula uzeeni?
Mkuu kuwahudumia wazazi ni hisani,mkuu wasingeweza kuniacha nife kwa sababu wamenizaa kwa starehe zao,sikuomba wanizae,kwa hiyo hivyo hivyo walivyohangaika kunileta duniani ndo hivyo hivyo walivyokuwa na wajibu wa kunitibu na kunisomesha.hata Mimi nina primary responsibility ya kuwa hudumia watoto wangu ambao nimewaleta duniani kwa starehe zangu.na niwajibu wangu kuwaandalia maisha yao ya baadae huku na Mimi nikijiwekea ka akiba ka uzeeni,wanangu si mgodi wangu maana nao watakuwa na responsibility zao zitakazotokana na starehe zao.hope umenielewa
 
Katika maisha lazima tukubaliane wazazi wetu ambao tangu tukiwa watoto walijisahau hawakuwekeza nyakati hizi utaziona ngumu kwa sababu

1.kama wazazi hawakufanikiwa kumiliki assets kama vile nyumba,viwanja,mashamba nyakati zile vitu vilikuwa bei rahisi basi kipindi hiki haya yote upambane uwafanyie haya yote

2.kama hawakujengea mazingira ya kujiajiri au kuajiriwa basi nyakati hizi utaziona ngumu kwani kila kitu ili ufanye kinaitaji rasimali

3.kama hawakufanikiwa kukutengenezea mazingira ikitokea umesoma na haujajiriwa nini unachotakiwa kukifanya

4.kama hawakufanikiwa kujiwekea akiba ya badae wataishi vipi basi ni jukumu lako kuwasimamia maswala ya fedha kila siku kuwatumia

Haya tuendeleee kama una kuongezea
Na wewe mkuu wakati huu ndio wa kuwekeza kwa watoto wako,ukilemaa tu na wewe inakuwa yaleyale...
 
Kibongo bongo mzazi akikusomesha sijui unataka nini tena alafu ukute ni mtoto wa kiume.
Mzazi anaweza akawa amekusomesha umesoma kwa bidiii ukamaliza degree yako vizuli tuu,

Shida inakuja ulitegemea kuajiriwa na ajira zimegonga mwamba alafu ukijiangalia huna mtaji wa kibiashara, huna pakuanzia huna wa kukushika mkono unadhani mtu wa mwisho kumkimbilia hapo ni nani kama sio kumrudiaaa baba.

Sasa hapo inatagemea baba yako alijipangajeeee
 
35 Reactions
Reply
Back
Top Bottom