Ukweli mchungu: Chanzo cha anguko la ndoa 1&2

Nyenyere

JF-Expert Member
Sep 9, 2010
14,769
10,650
Wakuu, amani ipitayo fahamu zote iwe nanyi. Ni muda kitambo umepita pasipo kupeleka mada jukwaani kwa sababu sikupata muda wa kutosha kuandaa makala ndefu yenye hoja fikirishi. Leo naleta kwenu hoja kuntu tuweze kujadili pamoja.

Wakuu, nimekuwa nikisema, na leo hii nasisitiza tena kwamba msingi mkuu wa ndoa imara ni wazazi. Kwamba kijana ama binti aliyelelewa katika maadili bora na wazazi wake ana nafasi kubwa ya kuwa mwanandoa bora kabisa. Yale unayotenda leo ni jumla ya mambo yote yaliyoujaza moyo wako.

Maisha ya kitaa
Baada ya wazazi kukimbia jukumu lao la msingi kwenye ndoa (malezi ya watoto), dunia iliingilia kati kujaza pengo hili. Vijana wake kwa waume wamejikuta wakilelewa na dunia tangu utoto wao. Huko hujifunza tabia tofauti kutoka tamaduni tofauti. Apatacho mtoto kutoka kwa wazazi wake ni sentensi mbili tatu tu za maonyo na makaripio jioni awapo nyumbani kabla ya kwenda kulala. Lakini mwalimu mkuu ni marafiki anaoshinda nao.

Sasa mambo haya huwa na matokeo hasi lijapo suala la ndoa. Sio rahisi kutambua hili kwa sababu ni maisha ambayo yamefanywa kuwa sehemu ya jamii na kukubalika. Mfano mdogo tu ni tabia ya kwenda "club" ama diisco. Nyingine ni tabia ya partying. Haya yaweza kuonekana kuwa ni maisha ya kawaida katika jamii, lakini tunasahau kuwa yamelenga jamii ya kawaida pia!!

Kwa kawaida taasisi ya ndoa si taasisi ya kawaida, inahusisha maamuzi magumu sana, tena huenda ndio maamuzi magumu zaidi mwanadamu aweza kufanya maishani mwake!! Nasema si taasisi ya kawaida kwa sababu kuingia kwenye ndoa ni kuamua "kujitenga na ulimwengu wa kawaidana kutengeneza ulimwengu wako. Kuna mtu aliwahi kusema, " love is blind, therefore marriage is an institution for the blind! Kuna ukweli katika usemi huu, kwa sababu kuingua kwenye ndoa ni sawa na kutoboa macho yako na ukawa huoni kingine chenye uzuri zaidi ya yule uliyemwona mara ya mwisho hata ukaamua kuwa uishi naye siku zako zote hapa duniani.

Ni sawa kabisa na yule kipofu ambaye alibahatika kufunguliwa macho kwa sekunde kadhaa, lakini akabahatika kumwona punda pekee aliyekuwa mbele yake, kisha macho yakafungwa tena akaendelea kuwa kipofu. Sasa ikawa kila akisikia watu wanasifia kitu, mfano gari nzuri, yeye huwauliza, "hilo gari ni zuri kama punda?" Hakuwa na kingine cha kulinganisha nacho katika ulimwengu huu kwa sababu yeye anaishi kwenye ulimwengu tofauti.

Hivi ndivyo inavyopaswa kuwa kwa wanandoa, kwamba mume awe na sura ya mkewe tu akili mwake, mke kadhalika. Hata asikiapo sauti za pembeni kwamba yuko mwanamke ana chura hatari awe na ujasiri wa kuhoji, ana chura kama mke wangu? Nje ya hapo ni kuzolewa na kila upepo uvumao, ni kama boti isiyo na nahodha. Kuingia kwenye ndoa ni kuamua kuwa starehe za dunia hii ni upuuzi na kwamba umegundua maana halisi ya maisha katika huyo unayefunga naye ndoa.

Maisha ndani ya ndoa
Kama nilivyotangulia kusema, uimara wa ndoa hutegemea makuzi ya wanandoa waliyopata kutoka kwa wazazi. Ndoa haifundishwi mtaani ama katika semina, tena ndoa ya kweli haifundishwi kanisani wala msikitini. Ndiposa tukasema, asiyefunzwa na mamaye hufunzwa na ulimwengu. Kijana asiyefunzwa na wazazi, atakapoingia kwenye ndoa mapigo makuu huambatana naye kama gharama ya kukwepa shule muhimu kabisa ambayo ni msingi mkuu wa ndoa. Miezi michache baada ya ndoa huanza magumi na mateke, vikao vya suluhu, kutafuta faraja nje ya ndoa n.k.

Nikirejea mifano niliyotoa huko kabla, kijana anayekulia maisha ya kwenda disco, partying n.k. ataujaza moyo wake mambo hayo. Ni rahisi mno kujidanga kwamba akiingia kwenye ndoa ataacha, lakini ukweli ni kuwa kawaida ni kama mazoea. Tabia iliyojengwa kwa miaka 25 si rahisi kuivunja kwa semina ya wiki moja!

Itaendelea..........

SEHEMU YA PILI

Inaendelea...

Kijana katika maisha yake yote kabla ya ndoa amepitia kwenye mafunzo mbalimbali kwa "]vitendo, halafu leo hii miaka 25 baadaye anapotaka kuingia kwenye ndoa tutarajie abadilike baada ya semina ya wiki moja, semina iliyojaa maneno tupu ya hamasa? Tuache kudanganyana na kuharibu vizazi vijavyo!!

Kwa mfano: kijana akioa binti ambaye maisha yake yote nje ya ndoa alizoea kwenda club ama disco, siku akiingia ndani ya ndoa atatulia kwa wiki kadhaa ili " azoee mazingira, waliopita JKT wanaelewa kutoa mtero. Hofu ya ndoa huisha mara, halafu mwili huyakataa kabisa maisha ya ndoa kwa sababu sivyo ulivyojengwa. Hamu ya kwenda outing na marafiki, kutamani kwenda kwenye disco, matamasha kama fiesta n.k. hurejea, tena mara hii kwa kasi kubwa mno. Nasema kasi kubwa kwa sababu, ni asili ya mwanadamu kuwaka tamaa ya kufanya kile azuiliwacho.

Kama ilivyo kwa mtoto, ukimkanya kuchezea kisu, atatafuta gap tu wakati haupo, atakishika na kukichezea ili abaini mwenyewe kuna nini mpaka umzuie. Akifikia ujana utamwonya kuhusu kujihusisha na pombe, sigara, mapenzi n.k. Lakini bado tu, ukimpa nafasi atatumia kujaribu ili afanye maamuzi mwenyewe kama kweli vitendo hivyo ni kama unavyomweleza?

Niruhusuni nitolee mfano mmoja kwenye biblia;

Adam aliumbwa akakabidhiwa aitunze bustani. Eva akaumbwa amsaidie Adam kuitunza. Kwa hiyo Eva alikuwa chini ya uangalizi wa Adam, lakini katika namna ya kustaajabisha, pale Adam alipomwacha Eva apate uhuru wa kuwa pele yake bustanini, historia ya mwanadamu ilibadilika. Akaamua kujaribu kula "tunda" ili aamue mwenyewe kama alichosema Mungu ni kweli ama la. Kwa ushawishi wa nyoka, huku akiamini hakuna amwonaye, akala. Akamwendea na mumewe akamshawishi kwamba anakosa starehe nzuri mno, naye kwa sababu alimpenda mno mkewe akachagua kumsikiliza.. Akala tunda. Wote wawili wakaingia matatani.

Sasa hata leo nyoka yuko kazini. Mke huyu awapo kwenye ndoa mara ataanza kusikiliza zaidi sauti za nje kwa marafiki zake kwa sababu ndio kawaida ya maisha yake. Ghafla ndoa itageuka kuwa mzigo mzito ambao unajaribu kumwondoa kwenye "uhalisia wake, yaani maisha aliyozoea. Hapo ndipo huanza majuto na malalamiko yasiyokoma ndani ya ndoa.

Kufuatia pengo hili la malezi ya awali, ndipo wajanja wa mjini wametengeneza program kwa jina la " semina za ndoa" kwa madai ya kuwaandaa vijana kuyakabili maisha ya ndoa kwa amani. Sasa ukitumia akili kidogo tu utagundua kuwa haiwezekani kamwe kupata amani ya ndoa kwa kanuni za kibinadamu, kwa mafundisho ya maneno matupu. Amani sio maneno bali ni matendo, iwe kwenye siasa, uchumi au ndoa!! Hatuhubiri amani, bali ni matendo yetu yanayoihubiri amani ya kweli. Mengine yote nje ya hapo ni porojo na kudanganyana tu.

Semina za ndoa

Kumbe semina za ndoa zimekuja ili kujaza pengo hili la malezi kwa materials ambayo sio original, ndio maana utasikia upuuzi wa mafunzo ya kisasa mfano;
Mwanamume ukitaka atulie mnyonye dudu yake, au mwanamke umnyonye tupu. Tena wengine huenda mbali kudai "kuta nne za chumba zinaficha siri nzito, mumeo akitaka nyuma mpe tu asijeporwa na wajanja!" Eti ni siri yenu wawili!!

Haya ndio mafundisho: kama mwenza wako anapenda kwenda club inabidi mpeleke mwenyewe. Usipofanya hivyo wapo watakaompeleka kwa sababu ni hitajio la mwili wake. Bahati mbaya sana ni kuwa si mahitaji yote huwekwa hadharani kwa hofu ya matakwa ya taasisi ya ndoa. Kwa mfano mume apendaye kunyonywa uume wake ndipo aridhike, au mke ambaye amejizoesha kunyonywa uke ndipo apate mzuka wa ngono aweza kumtaka mwenza wake ama asimtake amtendee hayo. Mwanamke akiomba kunyonywa na mumewe huingia katika hatari kubwa ya kusababisha mgogoro wa ndoa kwani kiasili hiyo ni dalili ya mke malaya ingawa nje ya ndoa imekubalika kuwa ni jambo la kawaida. Pia mume aweza kuwa ameharibika akili kiasi kwamba bila kumwingilia mwanamke nyuma basi hasikii raha ya mapenzi. Lakini ni vigumu mno kwake kuanzisha mada hiyo kwani yaweza kabisa kuiweka kwenye hatihati ndoa yake. Hii ni tabia ya wanaume malaya wasiothamini utu wao na wengine, lakini katika jamii nje ya ndoa inazoeleka sasa kuwa ni kawaida tu. Leo hii hakuna anayeshangaa mwanamke kutoa nyuma, bali jamii itamstaajabia mwanamke kumwacha mwanamume kwa sababu ya kulinda utu wake.

Sasa mambo haya nilisema ni ya kawaida kwa jamii ya kawaida, lakini ndani ya ndoa sio ya kawaida kwa sababu ndoa ni taasisi isiyo ya kawaida. Kama ndoa sio taasisi ya kawaida, tuseme nini basi kuhusu ndoa? Ndoa ni nini?

Jibu jepesi sana ni kuwa ndoa ni taasisi yenye dhumuni la kuwakomboa wanandoa kutoka utumwa wa ulimwengu huu na kuwaweka huru kwa kuwaingiza kwenye ulimwengu mwingine. Ndoa si utumwa kama ambavyo imeanza kuzoeleka katika zama hizi. Ndoa ni taasisi inayokuweka huru kabisa na hivyo huwi mtumwa tena!!...

Itaendelea....
 
Ahsante sana kaka... Hapa unatueleza kwakina kabisa ni kwa namna gani tunaweza kuondokana na migogoro iliyoshamiri katika ndoa nyingi hivi sasa .Nimefurahishwa na vile umeegemea zaidi katika kutafuta suluhisho..Amani ipitayo Amani zote iendelee kujazwa ndani ya moyo wako wakati wote..Elimu unayoitoa inanguvu mno Mkuu..
 
Amina
 
NONDO adimu kama hizi huwezi kuta zinawachangiaji wengi
Ubarikiwe mkuu kwa somo jema kwa vijana!

Haya ni moja ya masomo muhimu sana ambayo vijana wanapaswa kujifunza kwa uyakinifu!
Absolutely, Nadhani Solution ni kwa wazazi Kuwajibika ipasavyo na si vinginevyo
Mwanadamu ni kama mti, matunzo mazuri na uangalizi mzuri huleta mavuno mazuri na kinyume chake huwa tofauti;

Endelea na somo mwalimu
Ni kweli wakuu, tunajaribu kushirikishana kile tunachojaaliwa. Suluhu pekee ni wazazi kusimama kwenye zamu zao kama ulivyosema hapo mkuu.
 
Na Mimi nitoe rahi kwa vijana.
Ukitaka udumu na mke wako wa ndoa, uliyemuoa kwa dhati ya moyo wako.
"Usimlale Nyuma"
 
Back
Top Bottom