Ukweli kuhusu Zitto Kabwe foundation

Ukweli kuhusu Zitto Kabwe foundation

I doubt; mkopo gani hauna riba wala dhamana kwani hao ni wajomba zako? Kama umepata hiyo hela hiyo ni ile mambo ya pyaramid schemes. Wa mwanzo mnapewa halafu mnatangazia watu wakija wengi wanaingizwa mkenge. Mkopo gani hauna riba wala dhamana yoyote. Kama hao zzk foundation wana hela za kugawa bure inafaa watangazie watu! Kwanza zitto mwenyewe kashesema haijui hiyo foundation lakini bado matapeli hawakati tamaa.

Ni wahuni tu Kaka. Walihack akaunti ya Facebook ya huyo Dada kisha wakapost hivyo.
TUWENI MAKINI TU
 
Collateral yake ni nini? Mbona naona kama taarifa kama haijajitosheleza? Hivi kweli uaply loan online na kupata hapo hapo. What physical evidence do u pit inplace ku assure kuwa utalipa mkopo kwa wakati?

Nilitaka kuuliza swali kama hili hili. Ukisepa na mkopo wao watakupataje ikiwa mmepeana online?
 
Ni wahuni tu Kaka. Walihacok akaunti ya Facebook ya huyo Dada kisha wakapost hivyo.
TUWENI MAKINI TU

We unatuzuga tu hapa haunnekani hata kama mtu aliepata mil tatu out of elfu 83 we unapiga soga tu.
Unacheza na mil tatu za bure saivi umgekuwa kwenye consumption zone.
 
Ndugu wadau,

Nimeona hii kitu kwamba Zitto Kabwe Foundation inatoa mikopo isiyo na riba kwa online banking.

Mwenye ufahamu wa hii kitu atujuze tuchangamkie tenda isipokuwa isiwe DECI.

Link ni hii hapa: http://zittokabwetz.wapka.mobi/
 
Sifa kuu za wanachama tunaohitaji katika maombi ya kujiunga ili upatiwe mkopo nikama ifuatavyo:-

(a) UWE NI MTANZANIA

(b) UWE UMETIMIZA MIAKA 18 NA ZAIDI

(c) UWE NA AKILI TIMAMU

(d) UWE NA MOJA KATI YA VITAMBULISHO HIVI CHA KAZI, SEREKALI ZA MITAA, LESENI YA BIASHARA, KITAMBULISHO CHA CHUO, BANK au KITAMBULISHO CHA KUPIGIA KURA na kiwe na namba ya utambulisho.

KAMA UNAZO SIFA HIZO UNARUHUSIWA KUJIUNGA NA TUTAKUPATIA MKOPO WA PESA.

my take
watu wake kule Kigoma wananuka umaskini,angeshunghulika nao kwanza,,don't jump the gun!!
 
Zito ni member hapa JF ni vyema akaja kulisemea hili mapema. Isijekuwa watu wanapiga dili kupitia jina lake.
Cc: Zitto Kabwe
 
Zitto huyu Zitto kupewa mkopo usio na riba sharti ni kuwa mwanachama tu? au anataka kutakatisha pesa jamani?
 
inawezekana wadau mi nauliza ni kweli wapo
TAFADHARI USIJARIBU KUJIUNGA NA KULIPIA KAMA HUNA UHAKIKA SABABU JAMAA HAWANA ANUANI YA OFISI YOYOTE TANZANIA
 
Nimependa hio zawadi ya kuomba mkopo na kukubaliwa.
Mkuu mtoa mada huja eddit kweli maana duh, kwahio hizo 45min usha lamba zote hizo au ndo tayar.
 
jamaa angu mmoja nilimuuliza kuhusiana na hii kitu mwezi ulopita,akanijibu hii tasisi ipo kweli,na akadai jamaa yake ameshakopeshwa,na akanisisitiza kwa kuwa mueshimiwa ujaga mara moja moja ofisini kwetu nkimuona basi nimuulize kama siamini,bado sijaonana nae,na niliambiwa au nicheki na lady jay dee yupo kwenye hii taasisi pia ili niamini zaidi.Leo ntajitahidi kufatilia uwepo wa hii kitu kujiridhisha
 
kweli maisha yamekua magumu...wanabuni mbinu nyingi kuwaibia watu..
 
Leo nimeona Post ya Rafiki yangu facebook ikisema hivi;-


NAHITAJI USHAURI WENU GUYS. BE SERIOUS.

Juzi nilikua napitia Ukurasa wa Vodacom Tanzania nikakuta wameweka Tangazo lao la M-PESA lenye hiyo picha wakihamasisha watanzania wajiunge na Taasisi ya Utoaji mikopo iitwayo ZITTO KABWE FOUNDATION ambayo Vodacom wameingia nao mkataba. Hii Taasisi inatoa mikopo bila RIBA.

Nilisoma tangazo lao na kupuuzia nikawa najua ni matapeli hao wametengeneza page feki ya Vodacom nikaipotezea, sasa jana asubuhi nikakuta tena Tangazo katika ukurasa wa ukweli wa msanii Lady Jaydee nae kapewa dili la kufanya matangazo kuhusiana ma jaws ZITTO KABWE FOUNDATION pia sikua na uhakika nayo.

Usiku wa jana huo huo nikaona sasa Tangazo rasmi katika TV ilikua TBC1 walirusha Live hilo Tangazo katika Taarifa ya Habari za kibiashara wakatoa mpaka website ya Online mtu anaweza kujiunga na akapatiwa mkopo wa pesa na atarudisha mkopo wa pesa bila kua na RIBA halafu marejesho yao mazuri hawambani mkopaji.

Nikasema ngoja nijaribu kujiunga nione je? Niukweli wanatoa mikopo?? Nikafungua website yao jana usiku http zittokabwe-foundation.wapka.mobi nikasoma maelezo yote! Kuna fomu nikaikuta nikaijaza, nilipoijaza fomu nikapokea ujumbe kua nimefanikiwa kujiunga natakiwa kulipia ada ya Uanachama Tshs. 83,000 (ELFU THEMANINI NATATU ) ili maombi yangu ya mkopo yaweze kuidhinishwa nipatiwe mkopo. Nikawa naogopa kulipia nisije kutapeliwa bure!

Sasa leo Asubuhi kuna jamaa yangu kumbe nayeye ameshawahi kujiunga na wakampatia kweli mkopo nikamuelezea akanitoa hofu! Nikaona kwani elfu83 na kitu gani?? Ngoja nijaribu nikawatumia elfu83 katika M-PESA wakanitumia ujumbe kua wameipokea pesa nisubirie ndani ya dakika30Nikasubiria, kweli wakanitumia mkopo kupitia M-PESA asubuhi hii ya leo muda si mrefu, niliomba mkopo wa Tshs. 3,000,000 (Million 3) hapo nilipo siamini friends.

#USHAURI : Nifungue mradi gani nina hizi Million Tatu, kwani nilikua sijajipangay nilifanya kama najaribu tu sikua na imani kama ntapata kweli huu mkopo nimejaribu wamenipa! Sijajua biashara ipi ambayo inalipa sana?? Please nisaidieni Mawazo yenu nawaomba! Utani tuweke kando nipo serious katika suala hili nahitaji ushauri wenu.

Nikajaribu kumuuliza kama Ni kweli akanipa taarifa kuwa Ni kweli na ametumiwa hizo pesa (millioni 3).
Mwenye taarifa nayo mwingine atupe uthibitisho.

[TABLE="class: outer_border, width: 750, align: left"]
[TR]
[TD]"Narudia tena, sihusiki na mfuko wa mikopo unaotangazwa kupitia Mitandaoni. Sijaanzisha ZittoKabwe foundation. Siendeshi taasisi ya mikopo na wala sina biashara yeyote ile ndani au nje ya nchi. Hivyo puuzeni watu wanaotangaza mikopo kwa jina Langu. Nimejulisha vyombo vya dola suala hili ili kukamata matapeli wanaotumia jina Langu kuibia watu."
Zitto
[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
Humpati mtu hapa,ulnataka kutudanganya tutume 83000 mkaanzie weekend hutupati ngooo
 
Back
Top Bottom