Ukweli kuhusu Zitto Kabwe foundation

Mchoraji Cyper255

JF-Expert Member
Nov 21, 2012
1,758
6,087
Leo nimeona Post ya Rafiki yangu facebook ikisema hivi;-


NAHITAJI USHAURI WENU GUYS. BE SERIOUS.

Juzi nilikua napitia Ukurasa wa Vodacom Tanzania nikakuta wameweka Tangazo lao la M-PESA lenye hiyo picha wakihamasisha watanzania wajiunge na Taasisi ya Utoaji mikopo iitwayo ZITTO KABWE FOUNDATION ambayo Vodacom wameingia nao mkataba. Hii Taasisi inatoa mikopo bila RIBA.

Nilisoma tangazo lao na kupuuzia nikawa najua ni matapeli hao wametengeneza page feki ya Vodacom nikaipotezea, sasa jana asubuhi nikakuta tena Tangazo katika ukurasa wa ukweli wa msanii Lady Jaydee nae kapewa dili la kufanya matangazo kuhusiana ma jaws ZITTO KABWE FOUNDATION pia sikua na uhakika nayo.

Usiku wa jana huo huo nikaona sasa Tangazo rasmi katika TV ilikua TBC1 walirusha Live hilo Tangazo katika Taarifa ya Habari za kibiashara wakatoa mpaka website ya Online mtu anaweza kujiunga na akapatiwa mkopo wa pesa na atarudisha mkopo wa pesa bila kua na RIBA halafu marejesho yao mazuri hawambani mkopaji.

Nikasema ngoja nijaribu kujiunga nione je? Niukweli wanatoa mikopo?? Nikafungua website yao jana usiku http zittokabwe-foundation.wapka.mobi nikasoma maelezo yote! Kuna fomu nikaikuta nikaijaza, nilipoijaza fomu nikapokea ujumbe kua nimefanikiwa kujiunga natakiwa kulipia ada ya Uanachama Tshs. 83,000 (ELFU THEMANINI NATATU ) ili maombi yangu ya mkopo yaweze kuidhinishwa nipatiwe mkopo. Nikawa naogopa kulipia nisije kutapeliwa bure!

Sasa leo Asubuhi kuna jamaa yangu kumbe nayeye ameshawahi kujiunga na wakampatia kweli mkopo nikamuelezea akanitoa hofu! Nikaona kwani elfu83 na kitu gani?? Ngoja nijaribu nikawatumia elfu83 katika M-PESA wakanitumia ujumbe kua wameipokea pesa nisubirie ndani ya dakika30Nikasubiria, kweli wakanitumia mkopo kupitia M-PESA asubuhi hii ya leo muda si mrefu, niliomba mkopo wa Tshs. 3,000,000 (Million 3) hapo nilipo siamini friends.

#USHAURI : Nifungue mradi gani nina hizi Million Tatu, kwani nilikua sijajipangay nilifanya kama najaribu tu sikua na imani kama ntapata kweli huu mkopo nimejaribu wamenipa! Sijajua biashara ipi ambayo inalipa sana?? Please nisaidieni Mawazo yenu nawaomba! Utani tuweke kando nipo serious katika suala hili nahitaji ushauri wenu.

Nikajaribu kumuuliza kama Ni kweli akanipa taarifa kuwa Ni kweli na ametumiwa hizo pesa (millioni 3).
Mwenye taarifa nayo mwingine atupe uthibitisho.

=====================

UPDATES;

Majibu ya Zitto

"Narudia tena, sihusiki na mfuko wa mikopo unaotangazwa kupitia Mitandaoni. Sijaanzisha ZittoKabwe foundation. Siendeshi taasisi ya mikopo na wala sina biashara yeyote ile ndani au nje ya nchi. Hivyo puuzeni watu wanaotangaza mikopo kwa jina Langu. Nimejulisha vyombo vya dola suala hili ili kukamata matapeli wanaotumia jina Langu kuibia watu."
Zitto
 
Collateral yake ni nini? Mbona naona kama taarifa kama haijajitosheleza? Hivi kweli uaply loan online na kupata hapo hapo. What physical evidence do u pit inplace ku assure kuwa utalipa mkopo kwa wakati?
 
Siamini system inaonekana wapo watakaokosa hiyo siyo charitable organization na wala sio lazima anaetuma hiyo ada ya kujiunga apate mkopo.

Hivyo inaonesha mtu anaweza kupata loan by chance na akikosa hana right ya kuhoji.

Vipi kuhusu collateral kwa security ya mkopo na assurance ya mkopeshaji coz nashangaa process yote online.

Au wanategemea usajili wa line za simu na status ya line yako?
 
...#USHAURI : Nifungue mradi gani nina hizi Million Tatu, kwani nilikua sijajipangay nilifanya kama najaribu tu sikua na imani kama ntapata kweli huu mkopo nimejaribu wamenipa! ...
Nakushauri urudishe mkopo, kwa kuwa ulichukua bila kujipanga, usije ukafanya biashara bila maandalizi yoyote ukapata hasara ushindwe kurudisha mkopo!
 
mh! maisha magumu kweli kweli na kila cku utapeli unaongezeka yaani hadi tufike..........cjui.
 
collateral yake ni nini? Mbona naona kama taarifa kama haijajitosheleza? Hivi kweli uaply loan online na kupata hapo hapo. What physical evidence do u pit inplace ku assure kuwa utalipa mkopo kwa wakati?

hapo ndo napata mashaka na mimi. Nimemuuliza hilo swali akaniambia niingie kwenye hiyo link.
 
Masharti ya mkopo tafadhali au mpaka upate turn over sasa haina defined time ni mkopo wa aina gani huu Jamani!!
 
Hii kitu mwaka jana aillikana naona imerudi tena, matapeli hawa nashangaa kwan nini Tz systerm haiko makini kumlinda mlaji shame on us!
 
"Narudia tena, sihusiki na mfuko wa mikopo unaotangazwa kupitia Mitandaoni. Sijaanzisha ZittoKabwe foundation. Siendeshi taasisi ya mikopo na wala sina biashara yeyote ile ndani au nje ya nchi. Hivyo puuzeni watu wanaotangaza mikopo kwa jina Langu. Nimejulisha vyombo vya dola suala hili ili kukamata matapeli wanaotumia jina Langu kuibia watu."


 
Ahahahaa!! Niliechat nae fb amenitumia huu ujumbe.
 

Attachments

  • 1392966995029.jpg
    1392966995029.jpg
    41 KB · Views: 155
I doubt; mkopo gani hauna riba wala dhamana kwani hao ni wajomba zako? Kama umepata hiyo hela hiyo ni ile mambo ya pyramid schemes. Wa mwanzo mnapewa halafu mnatangazia watu wakija wengi wanaingizwa mkenge. Mkopo gani hauna riba wala dhamana yoyote. Kama hao zzk foundation wana hela za kugawa bure inafaa watangazie watu! Kwanza zitto mwenyewe kashasema haijui hiyo foundation lakini bado matapeli hawakati tamaa.
 
Back
Top Bottom