Vodacom kwa hili la changamoto za M-Koba mnazingua Pakubwa sana

Gai da seboga

JF-Expert Member
Apr 19, 2019
482
969
Wasalam mabibi na mababu...

Kimsingi vodacom walivyokuja na swala la m-koba niliamini kuwa sasa wamekuja na mageuzi ya kisasa katika swala Zima la uendeshaji wa vikundi vya vikoba mbalimbali.

Kuna kikundi cha kikoba ambacho nipo na tuna kama miezi mitatu hivi sasa toka tuanze, Bana miezi ilopita kila kitu kilikuwa sawa sawia katika kuweka hisa, kulipa Adhabu, rejesho la mkopo mpaka katika kutoa mikopo.

Lakini tuna siku nne sasa hivi kila viongozi wakiidhinisha pesa ya mkopo kwa mwanachama pesa haitoki mwanzon wakisema wanashughulikia mifumo, sasa imefika hatua ya kukera mana kla siku tunaambiwa changamoto inashughulikiwa lkn hakuna suluhu yoyote ya maana, ukizingatia wanaotaka pesa ya mkopo wana dharura.

Hili sasa linakera na lishachosha kiasi kwamba wanachama sasa wanataka wavunje kikundi huko m-koba wafanye manually tuu mana imekera kupitilizaa sasa.

Vodacom mjitathimini juu ya huduma zenu, km hamkujipanga bora msingeanzsha hizi huduma...
 
Poleni sana kwa hilo lakini navyojua mnaweza kutoa pesa pia isitoke huwa ipo hivyo hapo ndipo tofauti kubwa huonekana kati ya mifumo ya bank na a/c za simu kama MPESA
 
Back
Top Bottom