Ukweli kuhusu wimbo wa Malaika

Jamani tusichanganyane.hizi nyimbo za Malaika zimekuwa nyingi sana
 
Huu wimbo ni wa mfalme kichaa GK (King Crazy GK)
 
Bado nafikiri jina la kumpa wa kiume ila lazima liwe la kiswahili, so far nina Amani au Heri naendelea kufikiri mengine.

Malaika ni jina nililonalo kichwani toka miaka mingi. Vp wewe mkuu?
Ila kina Angel wanakuwaga vicheche hao! Jiandae.
 
Maana wanajionaga kama malaika kweli sasa hapo ndio shida huanzia hapo mjomba utapiga mpaka utaua jiandae babu.
 
Mimi ninachofahamu ila sina uhakika nacho kwa asili mia mia moja ni kuwa wimbo huo uliimbwa/ulitungwa na jamaa mmoja mchaga alikuwa anapiga muziki kutumia gitaa la galatoni anaitwa Frank. walijulikana kama Frank na dada zake baada ya hapo ndipo Fadhili William akauiga.
 
Wimbo ulitungwa na mtanzania aliyekuwa anapiga kwenye bend moja uko nairobi ila alirudi tanzania kabla ajaimba kwenye bend yake, ile bend wakaupiga wimbo huo, na maria makeba aliusikia wimbo akiwa kenya akauliza wimbo katunga nani, akambiwa mtunzi ni mtanzania alirudi kwao tanzania, ndo akawaomba kurudia wimbo na akasema wimbo ni kutoka tanzania.
Hii habari nilimsikia mtunzi wa wimbo huu akiojiwa, alikuwa anaishi dubai sijui kama bado yupo hai?
 
Huu wimbo kwa mara ya kwanza ulitungiwa Kigoma Ujiji eneo moja linaitwa Buzebazeba, aliutunga kijana mmoja wa Kiswahili mwenye asili ya Kikongomani lakini alikuwa na asili ya Zanzibar kwa kuwa mama alikuwa Mzanzibari na baba alikuwa Mkongomani,aliuimba akiwa anamuimbia dada mmoja ambae baba yake alikuwa mfanyabiashara maarufu wa Kinyakyusa ambae mpaka sasa anavuma bado na biashara mzee Mwakalindile.
Wimbo huu ni maarufu Kigoma kuliko sehemu nyingine yeyote Tanzania kwa kuwa ndiko chimbuko la wimbo huu
 
majengo mkoani kilimanjaro
na kwa mara ya kwanz aulirekodiwa kenya
 
Ila kina Angel wanakuwaga vicheche hao! Jiandae.

Mkuu ni Malaika sio Angel. Musa ni Musa tu hata aende Ulaya haitwi Moses.

Nitakua mkali kwa wote wataojifanya wazungu na kumuita Angel, ni mwiko mwanangu kuwa na jina la kizungu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…