Ndugu Wanabodi,
Tangu kutenguliwa kwa Mkurugenzi Mkuu wa TIC Bi Kairuki, kumekuwepo na mjadala mkubwa wenye kutoa hoja na uchambuzi wa aina mbalimbali wengine wakimtetea na wengine wakimponda,ilimradi kila mtu na fikra zake.
Katika mijadala yote, kwa bahati mbaya msingi wa maoni yaliyotolewa uliegemea kwenye taarifa za uwongo na potofu ambazo zimetolewa aidha kwa makusudi au kwa kutofahamu.
Mimi sitoingia kwenye mtego wa kuingia mjadala, bali nitakachofanya ni kuwasaidia wanaBodi kuwaelezea taarifa zipi zilizotolewa kwenye mitandao sio za kweli:
1) Sio kweli kwamba Bibi Kairuki alifuatwa na Rais Kikwete afrika ya kusini na kuombwa kurudi nchini kuja kufanya kazi TIC na akaahidiwa kiwango chochote kile cha mshahara.
Ukweli ni kwamba mwaka 2012, nafasi ya Mkurugenzi Mkuu wa TIC ilitangazwa baada ya aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa taasisi hiyo Bw Ole Naiko kumaliza kipindi chake cha Uongozi.
Awamu ya kwanza ya Usaili wa nafasi hiyo ya Mkurugenzi wa TIC ilifanywa na Kampuni ya KPMG kwa niaba ya Bodi ya TIC. Na awamu ya pili ya usaili ilifanywa na Bodi yenyewe ya TIC. Bibi Kairuki alisailiwa kwenye awamu zote mbili na kushinda usaili huo.
Kwa mujibu wa Sheria ya Tanzania Investment Act ya mwaka 1997 kifungu cha 10, Mkurugenzi wa TIC anateuliwa na Rais, hivyo baada ya kufaulu usaili jina la Bi Kairuki lilipelekwa kwa Rais ili amteue kama Sheria ya TIC inavyoelekeza.
Kwa mantiki hiyo taarifa zilizotolewa kwamba Bi Kairuki alitafutwa na Rais aje kusaidia TIC na kwamba alikuwa analipwa usd 18,000 na JK akamuahidi atamlipa alafu baadaye wakageuka hazina chembe hata moja ya ukweli.
Pia ipo dhana kwamba Bi Kairuki alipata kazi ya TIC kwasababu amesomea nje. Huo nao ni upotoshaji,Bi Kairuki amesomea shahada yake ya kwanza katika chuo kikuu cha Dar es Salaam na Stashahada amesomea nje ya nchi.
2) Suala la mshahara wa Mkurugenzi wa TIC linatamkwa na Sheria ya Tanzania Investment Act ya mwaka 1997 kifungu cha 10 (b)..kinachoipa Bodi ya TIC jukumu la kumpangia mshahara Mkurugenzi Mkuu wa Kituo hicho. Tafsiri ya sheria ile haisemi suala la mshahara ni la majadiliano.
3) Taarifa zilizoandikwa na baadhi ya magazeti na mitandaoni kwamba Bi Kairuki alikuwa anajilipa posho ya Tshs 25Milioni ni za uwongo na ziliwahi kupikwa na kuandikwa kwenye magazeti huko nyuma (to be specific) gazeti la Raia Mwema mwaka jana. uchunguzi ulifanyika, hesabu za TIC zilikaguliwa na kuthibitisha taarifa zile hazina chembe hata moja ya ukweli. Wapikaji wa taarifa hizo wanajulikana na sababu zao zinafahamika.
Wanabodi,
Tuepuke kuendesha mijadala kwa kutumia taarifa ambazo hazijathibitishwa. Kwa wanahabari ni vema wakafanya kazi yao kwa weledi. Maadili ya fani ya Habari yanawataka kuipokea taarifa iliyotolewa na Serikali na kuitoa kwa umma kama ilivyotoka. Kitendo cha kutia chumvi na kukoleza taarifa kwa habari za uwongo sio sahihi. Kwa mtu mwenye kutaka kupata ufafanuzi kuhusu taarifa iliyotolewa, vipo vyombo vinavyohuika vinavyoweza kutoa maelezo sahihi kuhusu suala hii. Navyo ni Wizara ya Viwanda na Biashara na Bodi ya TIC.