Mfukutuzi
JF-Expert Member
- Feb 15, 2015
- 239
- 175
Uchambuzi Wangu:
Nawashangaa sana baadhi ya Watanzania, wamekalia Lowassa Lowassa, wakati yeye na wenzake wamechukua tu tenda (consultancy) ya kukitangaza Chama (kutumia kivuli cha kutangaza nia na kutafuta wadhamini kuanza kampeni mapema kwa ajili ya chama).
Wengi wao wameahidiwa vyeo Serikali ijayo, na kwa wafanyabiashara kama Lowassa, wameahidiwa misamaha ya kodi na uhuru wa biashara zao. Kusoma shida, hata picha? Amka Mtanzania, jifunze kusoma katikati ya mistari!
Lowassa anafeli katika vigezo vingi mno; ikiwemo afya, makundi, kashfa za ufisadi, na vinginevyo vingi, hata yeye anajua. Anyway, sina lengo la kufika huko, ila majina ya wagombea halisi na wanayoisumbua CCM ni haya. Hesabu zote zinaangukia kwa hawa na sababu nimekuwekea;-
1. Charles Makongoro Nyerere (Historia inambeba)
2. Mohamed Gharib Bilal (Mzanzibari)
3. Mizengo Kayanza Pinda (Waziri Mkuu, ni kawaida kwa mawaziri wakuu)
4. Dr Asharose Migiro (Mwanamke)
5. Jaji Augustino Ramadhani (Mzanzibari/ Ukristo-Uislam)
6. Prof. Mark Mwandosya (Uzoefu)
7. Dr. Salim Ahmed Salim [kama atachukua fomu] - (Hana kashfa/ uzoefu/ Mzanzibari)
Watu watauliza mbona wengine maarufu na hujawataja? Membe ameshaonyesha hana uwezo mkubwa wa ushawishi na pia anakabiliwa na tatizo la Makundi. Magufuli hawawezi kumteua, ni mchapakazi na yuko serious na kazi hivyo atawaharibia mambo yao. Hawawezi kumwacha kwenye kinyang'anyiro, wamemwandalia nafasi nyingine kubwa ila si urais.
Ila pamoja na hayo yote, mgombea wa CCM mwaka huu ni lazima atakuwa Mzanzibari maana hivi karibuni marais kutoka bara wamefululiza sana, na CCM wanataka kuwabembeleza Wazanzibar wabaki kwenye Muungano.
Na huu ndio utabiri wangu. Nimemaliza. Tujadili nchi tuachane na vyama, na kama huamini hili, subiri Julai 10, top 5 ya kupigiwa kura inatoka kwenye list hii, angalia nyuma ya pazia Mtanzania.
By Mr. ZigZag (Mzalendo halisi)