Siku za hivi karibuni imewahi kuandikwa juu ya madai ya udini, ukabila, ukanda, ubabe katika Chuo Kikuu cha Dodoma. Mimi kama Mtanzania mwenye uchungu na taifa langu niliamua kuzifanyia kazi tuhuma hizo nzito. Niliamua kufanya hivyo kwa kuwa natambua athari za udini, ukabila, na ubaguzi wa aina nyingine katika jamii. Nchi nyingi zimejikuta katika mapambano ya kumwaga damu kutokana na aina mbalimbali za ubaguzi. Katika kuzifanyia kazi tuhuma hizo nilifanya uchunguzi na kubaini yafuatayo:-
Udini Uongozi wa UDOM
Chancellor: H. E. Benjamin W. Mkapa (catholic)
Vice Chancellor: Prof. Idris Kikula (Muslim)
Chairman of Council: Hon. Dr. M. G. Bilal (Muslim)
Deputy Vice Chancellor (Academic): Prof. L. Kinabo (catholic)
Deputy Vice Chancellor ( Administration) Prof. S. Mlacha ( Muslim)
Viongozi wengine wa ngazi za juu UDOM
Principal - College of Education: Prof. K.M. Osaki (catholic)
2 Deans of Schools in the College are all Christians
Principal - College of Humanities: Prof. C. M. Rubagumya (Christian)

Principal- College of Informatics: Prof. N. Mvungi (Christian - Protestant)

Dean of Student (Christian)
Dean, School of Natural Science (Christian)
Dean, School of Medicine (Christian)
Dean, School of Nursing ( Christian)
Source: (UDOM Prospectus and Website)
Wafanyakazi - Wanataaluma - Christians 96%
- Muslim 4%
Wafanyakazi Waendeshaji - Christians 86%
- Muslim 14%
Wanafunzi - Christians 92%
- Muslim 8%
(Source UDOM Website, newpapers, announcements of student admission)
Inashangaza sana kuona mtu mzima mwenye akili zake timamu kuzusha kwamba UDOM ni Chuo cha Waislam kwa kuwa kuna viongozi watatu Waislam bila kuyafanyia kazi madai yake. Bila shaka watu hao na wapambe wao hawalitakii mema Taifa letu.
Waungwana, kutokana na uchungu nilionao juu ya jambo hili bado nitaendelea kufanya utafiti kuhusu muundo wa uongozi katika vyuo na taasisi nyingine za umma na kumwaga data hapa uwanjani kwa madhumuni ya kuwasuta wote wasiotaka mwananchi wa dini au kabila fulani apewe madaraka hata kama ana uwezo. Ukweli ni kwamba viongozi wa UDOM hawakuteuliwa kwa sababu ya dini zao bali uwezo wao ambao kwa kiasi kikubwa unajidhihirisha kwa jinsi ulivyofaulu kubadilisha mandhari ya vilima vya Chimwaga na vitongoji vyake, pamoja na ramani ya nchi yetu katika dunia ya elimu ya juu. Ujenzi wa UDOM umesaidia sana kuinua kiwango cha elimu kwa vijana wanaomaliza kidato cha sita. Vijana wa wakulima na masikini wengine wa Tanzania ambao sasa wanasoma UDOM wangeishia kuwa wapiga debe kwenye vituo vya daladala kwa kukosa sehemu za kujiendeleza. Wanaobeza na wabeze, lakini mimi naifagilia nchi yangu na serikali yake kwa ujenzi wa UDOM bila kujali itikadi za Chama. Wanaosoma UDOM ni Watanzania haijalishi ni wanachama wa CHADEMA, CUF, TLP, CCM, NCCR, au ANR.
Watanzania tuamke, tuache kutumiwa kwa madai ya udini, ukabila, jinsia, kanda nk. Tusipokuwa makini tutajikuta kama majirani zetu.
Naamini JF ni kijiwe cha watu wenye busara, ni vizuri kikatumika kutoa taarifa zilizofanyiwa kazi. Nitasikitika sana endapo JF itageuzwa kuwa kijiwe cha majungu