Ukweli kuhusu Tundu Lissu; Anapenda watu, ni mtetezi wa haki

Anatetea watu pamoja na mafisadi na wakwepa kodi!

Mkuu tafuta mkakati mwingine bora wa kuwaaminisha Watanzania kuwa serikali yako inapambana na mafisadi na wakwepa kodi sugu. That's already a stale song. Kwa mtu yeyote mwenye mantiki kichwani anaelewa kuwa hapa Tanzania ni vigumu sana kwa mafisadi na wakwepa kodi kushamiri kama ilivyokuwa na ilivyo leo hii bila "urafiki" na Ikulu yenyewe. IT IS MISSION IMPOSSIBLE.

Nenda nchi kama Ethiopia uone kama ujinga tulio nao wa viongozi wa taifa kufisidi rasilimali za taifa unaweza kushamiri. Wako tayari hata kwa vita ya wenyewe kwa wenyewe kuliko kuachia kundi la watu lihujumu nchi jumla kupitia Ikulu kama ilivyo hapa kwetu.

Ndio maana serikali yako ya CCM imekosa "moral authority" ya kumkamata na kumshtaki mtu kama Lowassa kwa "ufisadi mkuu" mnaodai kafanya. Mmebakia kumbwekea pembeni kama vijibwa vioga. Mnahangaika kutaifisha mashamba ya Sumaye na kuharibu greenhouse ya Mbowe kwa kelele nyingi huku architect mwenyewe wa ufisadi mkuu (joka lenye makengeza) kawakalia bungeni tuli akiwasanifu tu. Hana shida ya kimshahara wala posho uchwarra za ubunge. Na hakuna mwenye ubavu si serikalini si ndani ya CCM wa kumnyooshea hata kidole.

Kubwa zaidi, ma-director wa ufisadi mkuu wanajimiminia whisk zao kwa raha zao baada ya kustaafu wakijua hakuna lofa wala mpumbavu yeyote mwenye jeuri ya kuwaletea fyokofyoko. Naona sasa imebakia kazi ya kumbwekea "harmless" Lissu. Shame!
 
Mtembelee Rugemalila na Seth kwenye wing yao lupango. Waambie wakutambulishe kwa wala bure wenzao.

Kinachowakuta hao ni manyanyaso na sio kupambana na ufisadi. Walitakiwa wapindishwe mahakani huko ndio kwenye ukweki. Akina Masamaki serekali ilisema haina nia ya kesi, mahakama ya mafisadi haina wateja. Sasa hapo huoni unachezewa siasa nyepesi na chafu?
 
..anayo mapungufu kama wanadamu wengine.

..lakini hakuna ubishi kwamba ni miongoni mwa watetezi wakubwa wa HAKI ktk nchi hii.
 
..hapa chini ni mahojiano ya Vicent Mughwai kuhusu familia yao na haswa Kaka yake Tundu.

..maelezo ya Vincent yanasaidia yanatoa mwanga kuhusu alikotokea Tundu Lissu na kwanini yuko hivyo alivyo.


Wewe ni nabii wa Mungu aliye Hai!
 
Back
Top Bottom