Ukweli Kuhusu Tetesi Za Nafasi Za Professionals JWTZ...!!!!

Ukweli Kuhusu Tetesi Za Nafasi Za Professionals JWTZ...!!!!

donlucchese

JF-Expert Member
Joined
Mar 23, 2011
Posts
17,258
Reaction score
22,139
Wakuu,
Naomba leo nilienda pale makao makuu ya jeshi Upanga kufatilia kuhusu hizi tetesi za nafasi za professionals kutoka.

Uzuri kuna Major mmoja ninafahamiana nae ambaye akani-link direct mpaka kwa mkurugenzi wa Army recruitment. Naomba nimnukuu,
"Taarifa hizi zilizozagaa kuhusu nafasi za professionals kutoka si za ukweli na za uzushi mtupu. Tumepata taarifa kwamba wengine wametapeliwa hadi fedha kwa ahadi ya kupatiwa nafasi za kujiunga na jeshi. Jumamosi tutatoa tamko rasmi kwenye vyombo vya habari kukanusha taarifa hizi za uongo. Jeshi lina taratibu zake na nafasi zikitoka hazifanywi siri bali hutangazwa katika vyombo vya habari"
mwisho wa kunukuu.

Hivyo wakuu wenzangu let's be patient tusubiri wakizitangaza wenyewe.

Pamoja.
 
Mkuu, umefanya jambo kubwa sana na kuleta marejesho hapa jukwaani inaonesha jinsi gani una nia njema na moyo mwema kwa jamii.
 
Mkuu, umefanya jambo kubwa sana na kuleta marejesho hapa jukwaani inaonesha jinsi gani una nia njema na moyo mwema kwa jamii.

Tuko pamoja mkuu, maana hata mimi nilikua najiuliza sasa kama nafasi za professional zimetoka je utajuaje ni profession gani inahitajika? Maana huwa wanatangaza mpaka kwenye magazeti labda nafasi za madaktari kadhaa, walimu kadhaa etc. Sasa utaombaje wakati hujajua ni nafasi gani zinahitajika kwa wakati huo? Tusubiri tu watutangazie mkuu.
 
wewe subiri utangaziwe tu mkuu na usishangae siku ukasikia wenzako wapo kunduch ukaanza kutafuta source wakat ts too late, ushaur hz vtu ni kmyakmya mkuu
 
Umefanya jambo la busara sana ndugu yetu na tunakushukuru sana kwa hilo bila shaka hata zikija kutoka rasmi utatujuza mapema kabla hata hatujachungulia magazetini..
 
Tuko pamoja wakuu, achaneni na maneno ya kimya kimya, jeshi halinaga siri. wakihitaji profession fulani watatangaza na tutatuma maombi.
 
mkuu umefanya jambo la msingi sana na ni mfano wakuigwa kama intelligent person wito wangu kwa wahusika wa aya mambo wasiwe wasili sana especially wizara ya ulinzi na jeshi lakujenga taifa pindi zinapokuwa zinazagaa taharifa kama izi wawe wepesi kulitolea maelezo so mpaka watu waanze kutapeliwa kiukweli vijana wengi kitaa atuna ajira na asilimia kubwa ni ujuma katika kupata izi ajira ni ay tu wa jf
 
Uko sawa kabisa mkuu,
 
Da kama zile za nmb uongo pia nimekomaa kutuma kwa ems ela yangu imeenda bule tafadhalin jaman mnaoweka post bila kuwa na taarifa kamila
 
Ww acha mambo ya njaa mtoatangazo alikurupuka watu wamejishikisha kwenye kaz zao uanze kuwarubun acha izooo
 
Back
Top Bottom