Mimi nina huo ugonjwa wa Usonji sipendi watu kabisa muda mrefu nashinda ndani, Darasani km mwalimu hayupo siwezi kaa natoka nje na kutafuta sehemu iliyojificha hata km kwenye Dampo kuepuka fujo na kelele, najua kuchora vizuri, sidhani km nitakuja kuoa kwasababu naogopa matukio ya kimapenzi nanayoyashuhudia na kuyasoma, nakiri shuleni sikua vizuri ila nikitaka somo fulani nifaulu nafaulu kwa kiwango cha juu saana na linakua ni moja tu, Mtaani wananiita Archimedes napendelea Nature, wanyama sipendi binaadamu na wala sio muongeaji nikitaka kuongea kwa nguvu na haraka naishia kigugumizi na kulia.
Hebu nisaidie ni aina gani hii ya binaadamu, nimeshindwa kufanya kazi ktk sehemu mbalimbali nilizo ajiriwa kikubwa ni ukimya wangu na kupenda kujitenga