Ukweli kuhusu sanaa ya utapeli na Akili za binadamu

Ukweli kuhusu sanaa ya utapeli na Akili za binadamu

Humble African

JF-Expert Member
Joined
Jul 28, 2013
Posts
4,781
Reaction score
14,439
Duniani tumo binadamu wa aina tatu kiakili na wote tunaishi pamoja in harmony na tumegawanyika katika makundi makuu matatu kiutendaji na utekelezaji wa akili zetu.

Kundi la kwanza ni wale Magenius.. Hawa mabwana wana IQ kubwa kuliko binadamu wa kawaida wana score around (160 - 300) wana uwezo mkubwa sana wa kuchakata taarifa vichwani mwao na kufumbua mafumbo magumu kuliko ila bahati mbaya zaidi hawa asilimia 90% yao ni wagonjwa wa ugonjwa wa usonji( Autism). Ugonjwa wa akili huu, ugonjwa huu wa usonji mara nyingi huwapata wakiwa watoto wa mwaka na nusu na kuendelea. Dalili zao huwa wanapenda kukaa peke yao, hawapendi kelele, wanachelewa kuongea, wana hisia Kali sana za kunusa na kusikia na wako very bright kwenye kitu kimoja pekee. Na pia huwa wanaongea kidogo sana..they "small talk" they are not good conversationalist. Sio waongeaji wazuri sana.

Nilifuatilia zaidi na kuyajua mengi juu ya Autism baada ya mpwa wangu kugundulika ana ugonjwa huu wa usonji akiwa na miaka 3..huyu dogo ana miaka 10 tu kwa sasa mnaweza kuwa mmekaa nje akawambia mtoto analia na kweli after a second dogo analia ndani...then mmekaa nje anakwambia maharage yanaungua..na kweli mnasikia harufu ya maharahe kuungua jikoni punde baada ya yeye kusema. Wako very sensitive. Ni wakimya na pia very loner..wanapenda kukaa wenyewe tu na huwa wanaconcetrates na kitu kimoja tu mawazoni mwao huyu dogo shuleni ni mtupu but he is very artistic genius and creative, unaweza ukatembea nae mjini then mkirudi home anadrawing kit yake ya kuchorea tu anachora mji mzima mlimopita kwa usahihi bila kurejea popote pale hadi huwa navurugwa ufahamu ukizingatia Mimi hata kuchora kagari tu siwezi. Nikagundua dogo is genius sababu ya ugonjwa wake wa usonji.

Nikarejea historia ya Michelangelo na Vincent Von Gosh hawa wote walikuwa artistic genius..huyu Van Gosh alikuwa anaweza kuuchora hadi upepo unaovuma..hakyamungu! This is insanely genius..ukingalia kwenye picha zake za starry starry night utaona kazi zake but alikuwa mwehu na michoro hii aliichora akiwa kwenye chumba cha vichaa alipojipiga risasi na kufariki akiwa mpweke sana. Michaelangelo huyu ni balaa yeye hata simzungumzii maana anahitaji Uzi wake kabisa ili tumtendee haki. Tukipata muda tutamjadili.

Albert Einstein Mwanamahesabu na mwanafikizia ambae amebadilisha maisha ya binadamu anaaminika kuwa the most influential scientist of the 20th century, amechangia mengi kwenye aerospace engineering, astrophysics, mathematic, spirituality e.t.c alifanya kazi kubwa ya sisi kuishi hivi Leo kwa theory yake of relativity ya E=MC sqaure ndio theory iliofagia njia ya kutengeneza mabomu ya nyuklia Leo hii. Akiwa na miaka 10 usonji ukiwa umemuandama hakuweza kuongea vizuri wala kuwa na marafiki akiwa na IQ kubwa kabisa aliweza kufaulu somo moja tu la hisabati tu shuleni yaliyobaki alifeli vibaya sana. Alipofikisha miaka 16 alikuwa anaitwa chuoni kusolve complex mathematics equations zilizowashinda maproffesor na akiwa na miaka 25 hakukubaliwa na vyuo vingi maana kwenye mtihani wa kujiunga na chuo alifaulu somo moja pekee mathematics kwa asilimia 100. Watu hawa huwa wanakuwa na ugonjwa wa Usonji unaowafanya kufikiri kitu kimoja tu deeply kutokana na nerve circuit zao zilivyoundwa kwenye brain. Magenius maarufu Waliothibitika kuwa na Autism ni Albert Einstein, Charles Darwin, Sir Issac Newton, Michelangelo, Aristotle, Tesla e.t.c Wengi wao wana muandiko mbaya sana maana mikono yao haiwawezi kuendana na kasi ya ubongo unavyofikiri, hivyo wanajikuta wanaandika fasta na rough ili kukimbizana na kasi ya ubongo wao unachokifikiria.

Tunahitimisha kwa kukubaliana na mwanafalsa maarufu wa ugiriki ya kale kwamba any genius is accompanied with some sense of madness.. Magenius wengi ni vichaa na hii inapigiliwa msumari na kauli hii "too much of anything is harmful " akili ikizidi kipimo muhusika anakuwa hayuko normal na hivyo anakuwa psychiatric Case hivyo ni ngumu sana kichaa kukutapeli maana ni mgonjwa wa akili maana ana complex things kichwani ambazo hata yeye hawezi na hana lugha ya kuzielezea kwa watu wakamwelewa kirahisi atawezaje kukushawishi uingie mkenge!? Jibu ni hawezi kukutapeli maana hata hawana good socializing ability kama wengine. lakini hapa sasa ndipo linapoibuka kundi la watu wengine wanaitwa "intelligent people" watu hatari sana hawa.

Hawa intelligent people bongo zao ziko katikakati kiakili wana uwezo wa kupata maneno sahihi ya kuelezea zile complex ides za genius..hawa uandika hata zile manual zinavoelezea namna ya kutumia vitu mbalimbali vilivyoundwa na magenius kwa lugha rahisi na nyepesi maana wanayo maneno sahihi na ya kueleweka kirahisi, hawa wanaandika kimkakati hoja zao na kuweza kushawishi watu kirahisi sana kama alivyosema Fid Q msanii wa hip hop kwamba "neno zuri huwa halina ukweli na neno baya ndio lenye ukweli " hawa intelligents siku zote Daima dumu wana maneno sahihi na matamu ya kukufanya uuone ukweli au usiuone.. Aina ya watu hawa ni Adolph Hitler, Barack Obama, Hemingway, e.t.c na Kwenye hili kundi wanakaa matapeli pia Kariba ya brother wa Forex n.k sijawahi kuona katika maisha yangu tapeli asie jua kupachika maneno sahihi na matamu kwenye maandishi au maneno yake. Sijawahi kumuona! Mtaji wao ni maneno yake matamu.

Then group la mwisho ni "normal people" au tunafahamika zaidi kama watapeliwa Ahahaha. Sisi tunafit Kwenye social world maana tunaenda clockwise na jamii yetu na bongo zetu hazijisumbui kuchakata taarifa zaidi wala kuconcertrates na kitu kimoja we are carefree hatuna tofauti na simu za Motorola za zamani mwanga ukizima zinazima moja kwa moja hadi ndani tofauti na intelligents ambao wao ni simu janja(smartphone) zenyewe screen ikizima na kuwa nyeusi ujue imezima kinafiki internal background inaprocess more informations kifupi hazilali bongo zao tofauti na normal people sisi ambao ni kundi kubwa akili zetu ni za kawaida sana na ndio akili za binadamu wenye afya na wazima kiakili maana hatuoverload brain zetu na sisi sio wagonjwa wa akili kama hao wawili hapo juu wanaosumbukiwa na Autism na Bipolar disorder.

Tujitahidi tujue mechanism za matapeli na tuwaepuke mapema before its too late.

Na je unadhani wewe unafit group gani hapo juu? Kwanini unahisi group ulilochagua linakufaa? Tupe sababu?
 

Attachments

  • images.jpeg
    images.jpeg
    22.8 KB · Views: 228
huyu Van Gosh alikuwa anaweza kuuchora hadi upepo unaovuma..hakyamungu!
Hili jipya kwangu, nitafuatilia kiongozi. Je kuna movie yeyote inayomhusu huyu jamaa.
hivyo ni ngumu sana kichaa kukutapeli maana ni mgonjwa wa akili maana ana complex things kichwani ambazo hata yeye hawezi na hana lugha ya kuzielezea kwa watu wakamwelewa kirahisi atawezaje kukushawishi uingie mkenge!?
Nakupata vyema
alivyosema Fid Q msanii wa hip hop kwamba "neno zuri huwa halina ukweli na neno baya ndio lenye ukweli "
Naendelea kuwaza kwa sauti, Je ni wimbo upi wa Fiq Q? niutafute.
Kwenye hili kundi wanakaa matapeli pia Kariba ya brother wa Forex n.k sijawahi kuona katika maisha yangu tapeli asie jua kupachika maneno sahihi na matamu kwenye maandishi au maneno yake. Sijawahi kumuona! Mtaji wao ni maneno yao matamu.
Naendelea kukusoma kiongozi
Tuwajue matapeli na tuwaepuke.

Na je unadhani wewe unafit group gani hapo juu? Kwanini unahisi hilo group linakufaa?
Kiongozi nawe una Talanta ya uandishi.

Salute kwako
 
Mwl.RCT huwa unanikosha sana ndugu yangu na comments zako? Ahahaha

Kuhusu Van Gosh kwanza tafuta ngoma moja Kali sana imeimbwa na baba yake Enrique Iglesias anaitwa Julio iglesias alimtungia ngoma huyu Vincent Van Gosh wimbo unaitwa Vincent au Starry Starry night...ni ngoma moja very soothing and emotional sana juu ya maisha ya Van gosh. Then pitia article zake mtandaoni utaenjoy.

Kuhusu nyimbo ya Fid Q nadhani inaweza kuwa ile sumu.

Kuhusu Talanta ya uhandishi sifikiri kama Niko vizuri sana..huwa namtizama bold kama Mwandishi mzuri wa makala.
 
Julio iglesias alimtungia ngoma huyu Vincent Van Gosh inaitwa Vincent au Starry Starry night.
Ahsante, Naziweka video kwa manufaa ya wengine pia

Lyrics - Julio Iglesias Vincent Starry-Starry Night

Starry starry night
Paint your palette blue and gray
Look out on a summer's day
With eyes that know the darkness in my soul
Shadows on the hills
Sketch the trees and the daffodils
Catch the breeze and the winter chills
In colors on the snowy linen land
Now I understand
What you tried to say to me
How you suffered for your sanity
How you tried to set them free
They would not listen they did not know how
Perhaps they'll listen now
Starry starry night
Flaming flowers that brightly blaze
Swirling clouds in violet haze
Reflect in Vincent's eyes of china blue
Colors changing hue
Morning fields of amber grain
Weathered faces lined in pain
Are soothed beneath the artist's loving hand
Now I understand
What you tried to say to me
How you suffered for your sanity
How you tried to set them free
They would not listen, they did not know how
Perhaps they'll listen now
For they could not love you
But still your love was true
And when no hope was left inside
On that starry starry night
You took your life as lovers often do
But I could have told you Vincent
This world was never meant for one as beautiful as you
Starry starry night
Portraits hung in empty halls
Frameless heads on nameless walls
With eyes that watch the world and can't forget
Like the strangers that you've met
The ragged men in ragged clothes
The silver thorn of bloody rose
Lie crushed and broken on the virgin snow
Now I think I know
What you tried to say to me
How you suffered for your sanity
How you tried to set them free
They did not listen, they're not listening still
Perhaps they never will
Kuhusu nyimbo ya Fid Q nadhani inaweza kuwa ile sumu.

Kuanzia Dakika ya 3.13
Ukiacha hisia zikuendeshe, kwa ujeuri utaishia kufeli
Sababu neno la ukweli sio zuri na neno zuri halina ukweli
Ntasahau vyote, milele ntamkumbuka aliyeniumba
Na daily ntakaa mkao wa pusha tu kama Umbwa
 
Safi sana mkuu! Nimependa ushapu na wepesi wako..hopefully wengi watafurahi hizi perfect work of art kutoka kwa manguli hawa wawili.

Ukiachilia mbali miziki Big G, mziki halisia una mengi sana ya kutufundisha. Ule mziki ambao hata Remmy Ongala aliwahi kuuliza asili yake ?

Tycoons.
 
we jamaa uko kundi la simu janja Hahahahaha hukawii kutupiga. (najaribu kuwa genious eti nachakata taarifa). kumbe bashite tu
Simu janja janja mwenyewe.. Ahahaha!

Relax Mimi normal mwenzako mzawa. Wale wahanga wale wa kupigwa za uso na simu janja? Au maandishi yamekaribia kunoga kama ya simu janja?

Nikija na project na Mimi after a while kimbia sana unless nitakuchakata...maana nishachakatwa tayari! Ahahaha.
 
Ni Kweli Mkuu. Kuna Novel Nilisoma Ya Jodi Picoult Inaitwa "House Rules" Inaelezea Autism Spectrum And Aspegers Syndrome. Kuna Dogo Ndani Ya Hii Novel Ni Autistic With Aspegers Syndrome. As You Said They Are Hypersensitive, Specialize In One Area Of Intelligence, Anti-Social, Fail To Read Social Cues. I Really Enjoyed The Book. Thanks For Your Thread. It's Literally True.
 
Wewe una jaribu kuwa mtu wa hapo kati lakini hujakidhi viwango. Maandishi haya yana uongo wa wazi hata mimi wa kundi la mwisho naweza kuona.
 
Back
Top Bottom