Mamaya
JF-Expert Member
- Jul 4, 2011
- 4,794
- 3,724
Madesa wewe ni researchers wa ukweli au magumashi.
Ni kama una lako jambo vile, maana usingekuwa nalo story ingebalance, now its a one sided story from a 'researcher' ....
Ntakubishia si kwa sababu nimefika Rwanda bali taarifa yako haikidhi mizania ya mtafiti, ingawa pia mie sio mtafiti.
Kwa mfano:
1. Watu kujua wizara ya elimu iko wapi researcher Madesa anahusisha na kuelimika kwao???? Zaidi ya nusu ya watu mliowauliza walikiwa hawajui wizara iko wapi.
Ilikuwaje watu karibu ya nusu (wanaopajua wizarani) mliowauliza na bado hamkufika wizara ya elimu. Kama sio urongooo!!
2. Reseacher unashangaa enrolment rate ya 97%. Ulipata kujua gross enrolment rate ya Tanzania miaka ya 70?? Ulipata kusikia UPE?? Je sasa enrolement ya Tz ni ngapi ktk MDGs??? Unakimbilia kutupa story za marekani (eti hata marekani haijafikia 97%) ambako sie tunaona kwenye Tv tu.
3. Unasema swala la laptop haliwezekani kwa vile hakuna umeme wakati kuna samsung za kutumia sola hata kampuni ya Tigo wanagawa siku hizi.
4. Ni kweli wanyarwanda hawajui kinachoendelea serikalini?? Je watanzania tunajua kinachoendelea serikalini na kama twajua imetusaidiaje???
Sasa badala ya kuleta matokeo ya utafiti wako unaleta story za mtaani, mara mia wanaotujuza viota vya maraha ndani ya Kigali kuliko taarifa ya msomi ambaye hakuelimika....watafiti kama wewe ndio mmejaa Ikulu yetu ndio maana mambo hayaendi.
Samahani kama nitakukwaza...........
anatakiwa angalau akasome kitabu cha cothari.