Ukweli kuhusu Rwanda na Kagame kwa ujumla (tofauti na wengi wajuavyo)

Kagame, Mseveni, J. Kabila(Polite Kanambe -Hili ndo jina lake halisi) wote hawa ni ndugu wa damu. Kagame anaendelea kwa ubabe na kupata vitu vingi bure toka DRC kwa mjomba wake Polite mfano Umeme anaotumia bure ni wa DRC alichukua madini mengi sana dhahabi na almasi wakati wa kumsaidia Kabila Laurent. Bado akataka amegewe na sehemu ya ardhi ya DRC Laurent akakataa - akammaliza na kumuweka huyo mpwa wake(Hakutoa hata majeshi yake hadi leo wako DRC) ambaye hadi sasa full ulinzi wake ni Watusi tu. Wacongo hilo wanalojua na ndo maana jamaa ni vigumu sana kuonekana hadharani japo ni Rais, ikitokea kuhutubia anafanya hivyo kwa njia ya TV na Radio. Je, kwa hali hiyo ya burebure na ka nchi kadogo sawa na mkoa mmoja hapa TZ kwa nini asiendelee!? NINAMSHANGAA!! Mimi ningelipa Mshahara kama Gadaffi........... Haya wabishi wa JF mnayajua hayoooo! kazi kwenu
 
Madesa, angalia upande mwingine wa shilingi uone jinsi wasomi wanavyoiona Rwanda:
The small African nation of Rwanda recently announced that it had cut poverty by 12% in six years, from 57% of its population to 45%. That equals roughly a million Rwandans emerging from poverty -- one of the most stunning drops in the world.
Laiti ungemwelewa mtoa mada, basi wala usingeleta hii hoja....hebu angalia hapo kwenye red...."Rwanda, recently annocuned....!" Hivi unapata shida gani hapo kufahamu kwamba huo si uhalisia bali ni serikali ndio ilitangaza?! Kama umemsoma vizuri mtoa mada, anasema kwamba baada ya kwenda kwa mtu wa USAID, huyo jamaa wa USAID akasema kwamba "analetewa tu data...!"
It's a remarkable achievement for Rwanda, which has emerged from civil war and a bloody ethnic genocide in the 1990s. How did it happen? The Times quizzed Paul Collier, director of the Center for the Study of African Economies at Oxford University, about the numbers.
Yaani remarkable achievement from wht the government announced!"
Are there any doubts that the drop is real?
No doubts; I know the economics professor
who did the data analysis, and he is highly experienced and painstaking, so it is genuine.
Hapa nashawishika kumwamini mtoa mada. Hoja yangu ni ile ile, kwamba mtoa mada alipokutana na mtu wa USAID, akaambiwa huyo mtu yeye uletewa tu data!! hapa tena, tunamuona Professor akisema " I know the economics professor who did the data analysis....!" Huyo Economic Professor ndie alifanya Data Analysis; so who collected the data?! How realiable were the collected/submitted data?! Don' you know the difference between Data Collection and Data Analysis?! Kwa Bahati , mie nimeshawahi kufanya yote hayo mawili na kwa ujumla wake; yaani, Data Collection, Data Analysis as well as Data Collection and Analysis! Hilo la pili ni kwamba, kuna mtu mwingine kabisa ambae amekusanya Data, tena si ajabu hata kumfahamu humfahamu na wewe unaishia tu kufanya data analysis!! Data Collector ndie anayeuona ukweli ambao si lazima auandike sawa na alivyouona!! Therefore, kama huyo bwana alifanya Data Analysis na si yeye aliyefanya Data Collection, then hapo hamna genuity yoyote coz' kwani we're not sure kama huyo Data Collector alifanya hiyo kazi professionally au alijifungia tu chumbani na kupika hizo data! Na hata anapomalizia " so it is genuine" inaonesha wazi kwamba haja-base kwenye scientific conclusion!!
My take: Ukiona wazungu wanakusifia sana, basi ujue hapo kuna tatizo. Rwanda wanasifiwa sana na wazungu kutokana na kuondoa urasimu....hata mimi nawasifia sana kwa hilo! Hata hivyo, lazima tukumbuke kwamba hivyo ndivyo watakavyo wazungu kwa nchi za wenzao...yaani waingie tu na kutoka kadri watakavyo lakini si wewe ufanye hivyo kwenye nchi zao! Ngoja leo serikali ya JK iondoe restrictions za kuingia nchini "kufanya uwekezaji!" Ngoja leo serikali ya JK iondoe Visa restriction kwa hao wanaojiita wawekezaji....ngoja leo pasiwe na restriction ktk upatikanaji wa ardhi....na mambo mengine kama hayo! I am telling you, within one months, itatangazwa kwamba TZ ndio sehemu bora kabisa duniani katika kufanya uwekezaji (katika kuiibia)!! Huyu JK leo anayeesemwa vibaya, atasifiwa kila mahali na wazungu! Ni nani asiyekumbuka jinsi Ben Mkapa alivyokuwa anasifiwa na wazungu hadi kupewa cheo cha Mwenyekiti Mwenza wa Utandawazi?! Hili lilifanyika baada ya kuwa Mkapa ameuza mashirika yote na kuruhusu wazungu wachukue kila tone la dhahabu kwa ujira mdogo!! YUle Morgan Tsivangrai (not sure wit spelling) wa Zimbabwe wakati akiwa kiongozi wa wafanyakazi alikuwa anapondwa sana na wazungu na kuambiwa si lolote si chochote na kwamba hajasoma!! Enzi hizo alikuwa mwiba mkali kwa wazungu kwavile ndio walikuwa wawekezaji wakubwa hususani kwenye kilimo! In short walikuwa hawampendi kabisa! Baadae wazungu hao hao wakaja kuwa rafiki mkubwa wa Morgan baada ya Morgan kuondoka kwenye uharakati na kumpinga Mugabe ambae aligeuka kuwa mwiba kwa wazungu! In short, ukiona kiongozi yeyote wa dunia ya tatu anasifiwa sana na wazungu basi fahamu kwamba hapo kuna tatizo! Wazungu kamwe hawatakuja kumsifia kiongozi yeyote anayeenda kinyume na matakwa yao hata kama anafanya hivyo kwa maslahi ya wananchi wake! Hivyo basi, ukweli unabaki pale pale kwamba Rwanda si lolote si chochote.Kama mwezi mmoja hivi uliopita nilikutana na dada mmoja Mnyarwanda ambae yeye mambo yake si mabaya! Alikuja Dar kwa mapumziko...niliongea nae mengi sana kuhusu Rwanda, ajabu ni kwamba yale tunayoyasikia kwenye vyombo vya habari ni tofauti kabisa na jinsi dada yule alivyonieleza!

NasDaz, mto mada nilimwelewa vizuri in the context kwamba Rwanda is being commended for whilst it should not be in the first place.
I'm still concerned with the authenticity of the report / research! Let the author come out with the genuine identity or rather the source and reference (as I did in my case) of his / her research, I quoted the L.A Times.
Rwanda si tu inasifiwa na wazungu, no. Inasifiwa pia na watu tunaoangalia mambo in perspective. Huwezi kunishawishi kwa vyovyote vile kwamba sisi tunafanya vizuri zaidi Rwanda wakati kule bei za consumables ziko chini kulinganisha na sisi. Ni mengi sana ambayo we are more worse in comparison.
NasDaz, it seems you're not in Tz otherwise you could'd realized that there is no visa restrictions at all here since foreingers do come in here with the tourist visa but do engage themselves in business, tena kubwa! Nenda Kariakoo uone hawa jama wa Kichina tena wako hadi uswahilini sasa hivi.
Ukweli unabaki pale pale tu kwamba tunapiga porojo na uswahili wakati Rwanda wanasonga mbele, wenzetu shirika la ndege ndo linanunua madege makubwa sisi hatuna hata ya kukodi sasa hivi, hawa jamaa kabla mauaji ya kimbali walikuwa wanatumia kifaransa lakini sasa hivi ni kizungu huko mashuleni. Sisi shule tunajenga za kata ambazo matunda yake tunayaona. AIBU.
 
aisee hivi huyu gen. laur nkunda yuko wapi eti?atakuwa anakula bata tu baada ya kazi nzito
Mkuu Gen Laurent (Louraa) Nkunda yupo nyumbani kwake Kigali anakula bata tu baada ya kukamatwa na serikali ya Kagame. Ila Brig. Gen. Jean Bosco Ntaganda bado yupo mashariki mwa DRC akiangalia maslahi ya Rwanda pamoja na kujinyakulia vito vya thamani.
 
Kikubwa hapa ni kuangalia mazuri ambayo kagame ka-achive kwan hakuna nchi africa kwa sasa isiyokuwa na puppets ambao wamewekwa na wazungu!
 
I have never doubted Madesa as far as these issue are concerned. His credibility to me is unquestionable. Aanayesema katumwa na Magamba hajui anachoonge.
 
I have never doubted Madesa as far as these issue are concerned. His credibility to me is unquestionable. Aanayesema katumwa na Magamba hajui anachoonge.

ni kweli mkuu. anayo yaongea ndio ukweli wenyewe. mwenyewe nimefika pale nyakarambi vijijini. hakika rwanda sio nchi ya kuishi. yaani utafikili wapo vitani bado. bunduki kubwa kubwa nje nje, beria za kumwaga, kila hatua mnasachiwa.
 
Mkuu mbona nawe unawajua hawa wazee? Duh huyu Ojukwu alimuingiza king hata Nyerere! Tutajadili tu haya masuala ya kijeshi hasa kuzungukia bara la Africa. Kuna wengine walikuwa ni wauaji tu ila kuna wengine walikuwa ni wapambanaji hasa. Kuna siku tutafanya hivyo ni kuhabarishana mengi.

Nimekufungulia thread hiyo ila naona mamodereta wameifuta pengine kwa sababu ya kulinda usalama wa taifa halafu nimegundua kwenye ule mjadala wa wanamapinduzi tulisahau kumjadili huyu Luteni wa Anga aliyevunja rekodi ya kufanya mapinduzi mara mbili na kufanikiwa mara zote Flight Lieutenant Jerry Rawlings – Ghana « Max Siollun's Website - hivi alibahatisha au vipi?
 
ukishaona rais wa nchi anavaa uniform za jeshi hilo ni tatizo-usitegemee kuwa na democracy kwenye volatile nation kama rwanda.
NGOJA NIJISIKILIZIE ZANGU WIMBO WA KWETU PAZURI MIMI....
 
umeongea mambo mengi sana na kutumia muda mwingi kumjibu mleta thread na hoja zake kwa kuniquote mimi,lakini ulichotakiwa ni kuniprove mimi wrong kwa nilichojaribu kukiaddress kuhusu kagame kuitawala Rwanda kwa mkono wa chuma,bahati mbaya sana hukufanya hivyo;nikuulize je unaona hali ya rwanda ya kagame iko sawa kwenye suala la uhuru wa kutoa maoni miongoni mwa raia?magazeti ya rwanda kwa mfano yako huru kuandika chochote kuhusu kagame na serikali yake kama tunavyoona hapa kwetu kwa magazeti kama mwanahalisi kuichambua serikali na rais kwa uhuru wa hali ya juu?je rwanda ipo mitandao ya kijamii ya aina ya jf ambayo mtu anaweza kuandika jambo lolote mradi asitukane matusi ya nguoni kuhusu rais na serikali kiujumla?je rwanda wapinzani wako huru kama hapa kwetu ambapo hatusikii mpinzani kuvamiwa na majambazi baada ya kuonekana tishio kwa serikali na rais?

Kuhusu hiyo picha hapo mpushi ni rwanda kama unaijua rwanda sawasawa na pia kama ulivyosema siku hizi sana ku-verify information nakubaliana na wewe kabisa kwani huo urahisi ndio ulioniwezesha mimi kuipata hiyo picha halisi ya mwanafunzi halisi wa shule ya msingi ya rwanda,sitaki kujiingiza kubishana kuhusu ubao anaotumia huyo mtoto,mwenye macho ataona kwa macho yake na kutafakari kwa akili yake na kuipa maneno anayoyajua hiyo picha....

Sina uhakika kama umezisoma posts zangu zote zinazohusiana na maada hii. Ukiisoma kwa mfano post yangu ya kwanza utaona kuwa hoja zake zote nilizipitia - nimeweka mpaka link zinazothibitisha nilichokisema. Tatizo lako ni kuwa selective on what I wrote hence ignoring/missing the big picture. Granted kuwa Rwanda demokrasia yao inaweza kuwa questioned depending on what is your definition of democracy, lakini angalia global position yao in good governance. "Picha Halisi" sio objective, "picha halisi" kwangu si lazima iwe "picha halisi" kwako/kwa mwingine. But my question still remains: Unatambuaje kuwa huyu ni ignorant wa laptop kwa kuangalia picha ya huyo mtu akifanya jambo lisilohusiana na matumizi ya laptop? Kwa nguo/viatu alivyovaa? Kwa kuwepo ndani ya darasa ambalo si state of art?

Hapo kwenye RED is precisely what I have been so far trying to point out. Ukifikiria kwa akili yako, lazima utapata conclusion fulani, just like anybody else. Will that subjective conclusion of yours - or anyone's conclusion for that matter - qualify to be termed as a FACT??? Kumbuka maada inasema UKWELI KUHUSU RWANDA etc etc etc - which suggests an irrefutable fact. Nisingekuwa na tatizo mtoa maada, wewe na wengine wooote kabisa mnaouona "ukweli" huu mngeuita "MAONI/MTAZAMO". Mnachokisema hapa ni at best circumstantial incidences (kwa mfano mpinzani wa serikali kuvamiwa na majambazi), kwani jambazi huchagua political affiliation/status ya mtu anaemfanyia ujambazi wake? What if it is true huyo/hao wapinzani walikuwa victim wa common criminality? Are you 100% certain kuwa wapinzani wanauliwa na Kagame?

Btw: The East African haliuzwi Rwanda? Haliko critical kwa Kagame? Sina ushahidi wa kuwepo au kutokuwepo kwa blogs za Wanyarwanda, lakini hata kama hazipo ina maana Wanyarwanda hawawezi ku-surf internet elsewhere na wakapata information ambazo serikali ya Kagame isingependa wazipate? Unataka kuniambia ukiwa Rwanda, BBC, CNN, Aljazeera n.k. hazipatikani?
 
one has to appreciate the power of HISTORY. Before you talk of rwanda i think one has to get its full history. I totally agree with what Kagame is doing, infact he is my role model.
 
Nimekufungulia thread hiyo ila naona mamodereta wameifuta pengine kwa sababu ya kulinda usalama wa taifa halafu nimegundua kwenye ule mjadala wa wanamapinduzi tulisahau kumjadili huyu Luteni wa Anga aliyevunja rekodi ya kufanya mapinduzi mara mbili na kufanikiwa mara zote Flight Lieutenant Jerry Rawlings – Ghana « Max Siollun's Website - hivi alibahatisha au vipi?

Mkuu uliandika nini hadi wafute? Angalia usiguse usalama wa nchi kwa kuwa kale kasheria usalama wa Taifa kanaweza kakakupeleka pabaya! Nadhani kama tunaongelea mambo ya hawa wakuu in general hawezi kufuta ila ukiingia kuongelea specifically kwa hawa wetu wa TZ wanaweza kufuta. Mkuu ujue hatuna utamaduni wa kutoa classfied information baada ya muda kuwa umepita ili ziwe for public consumption, hivyo siri huendelea kuwa siri.

Mkuu unanigusa hapo kwa Fl. Lft. Jerry Rawlings. Jamaa alikuwa akijiita Junior Jesus.
 
I googled and you-tubed and was surprised. Kila mtu ana discuss Rwanda, wazungu, wa-Asia, wa Tanzania, etc. Why does this country matter? Why do u waste your time, discuss yourseleves and other countries with serious problems such as Somalia, Burundi, etc. But they say Nobody Kicks a Dead Dog.
 
Ni rahisi sana mtu kumshambulia Kagame ikiwa umetoka nchi yenye Nidhamu ya woga amani na utulivu) kama Tanzania. Hata mimi leo ukiniuliza wizara ya Elimu iko wapi Dar kusema kweli sijui na sidhani kama niko pekee yangu. Kati ya wakazi millioni 5 wa dar nikna hakika asilimia 90 hawajui wizara ya elimu iko wapi kwa sababu hakuna ulazima wa kuijua.

Pili - Nimemsoma Madesa ambaye anaonyesha jinsi walivyokuwa wabovu ktk kufanya research kiasi kwamba karibu kila mtu aliyeko Rwanda kenda kupumzika. Badala ya ndugu yangu kumshangaa huyo mfanyakazi wa USAID kutojua maeneo yaliyokuwa na upungufu wa shule, wakati ni kazi yake na ndiye alotegemewa kujua inaonyesha wazi kwamba hawa ma TX wanaoletwa na NGOs huja kujirusha tu Afrika hawana msaada wowote.

Tatu - Swala la Mahutu na Watutsi, pengine mkuu wangu Madesa analifikiria hili ni swala dogo sana ambalo anaweza kulipatia ufumbuzi kirahisi.. Pengine utueleze wewe kama ungekuwa rais wa Taifa ambalo chuki baina yao ni ya wananchi wenyewe wanachukiana utaweza vipi kuiongoza nchi hiyo, lakini kumlaumu Kagame kwa kuweka ulinzi, kukataza watu kuzungumzia vita ama tofauti zao ili tu kuonyesha yeye ni dikteta haiwezi kutupa majibu. Wewe sema Kagame anatakiwa afanye nini? ikiwa hawa watu wako tayari kabisa kuuana tena umetupa na ushahidi wa chuki kubwa waliyokuwa nayo.

Rwanda ilikuwa torned na vita na sijui kaa uliwahi kufika Rwanda kabla au wakati wa Vita, Kwa sisi wakazi wa ukanda wa ziwa hadi Kigoma tunajua vizuri adha walizokuwa nazo hawa watu.. Wakimbizi wa Kihutu walikuja Tz toka miaka ya 60s wakifanya kazi za manamba ktk mashamba ya Pamba na ufugaji. Rwanda ilikuwa haitamaniki tena naweza sema Burundi ilikuwa mbele sana ya Rwanda. Nakumbuka vizuri sana kabla ya vita tulikuwa tukichenji Tsh 100 kwa Faranga 1,000 (franc) haya nambie leo hii imekuwaje Tsh iko chini ya Franc? - Tzsh 260 kwa Franc 100.

Tumeelezwa na takwimu kibao wala sii moja kwamba Tanzania ni nchi ya tatu duniani kupokea mikopo kwa ajili ya uchumi, leo mtu anakuja itolea mfano Rwanda ambayo ilikuwa vitani tena vibaya ktk historia ya dunia hii. Hata kama nusu inapata misaada mikubwa at least wao wanaitumia misaada hiyo uendeleza nchi sio kama sisi kila msaada huenda kujenga vitambi vya watu maana siku hizi hadi wanawake Tanzania wana vitambi.

Kama Udikteta unaweza kuijenga jamii na kuwafanya waishi kwa usalama zaidi basi ni bora mara mia kuliko demokrasia kwa watu ambao roho zao zina wingu kubwa la uhasidi...Demokrasia haiiwezi kusafisha nyoyo za watu bali ni njia rahisi sana ya kuwatenganisha, kuwagombanisha na kuwasambaratisha. Demokrasia sio dialog ni mfumo unaolenga watu wenye UMOJA kwanza na sio Taifa lililojitenga kwa marabaka, demokrasia ina sehemu zake haiwezi fanya kazi kila mahala.
 
Hawa watutsi si wa kuwaamini kabisa, maana stori ninazosikia kuwahusu zinatisha. Na haya ninayoyasikia kuhusu Kagame na Rwanda ndio yananizidishia uoga.
 
Mkuu uliandika nini hadi wafute? Angalia usiguse usalama wa nchi kwa kuwa kale kasheria usalama wa Taifa kanaweza kakakupeleka pabaya! Nadhani kama tunaongelea mambo ya hawa wakuu in general hawezi kufuta ila ukiingia kuongelea specifically kwa hawa wetu wa TZ wanaweza kufuta. Mkuu ujue hatuna utamaduni wa kutoa classfied information baada ya muda kuwa umepita ili ziwe for public consumption, hivyo siri huendelea kuwa siri.

Mkuu unanigusa hapo kwa Fl. Lft. Jerry Rawlings. Jamaa alikuwa akijiita Junior Jesus.

Nadhani mamods wamefanya pre-mptive measure, mambo ya kinga ni bora kuliko tiba hasa ukizingatia watu mngeanza kuchangia kwa undani mngetoa siri za wanajeshi wetu mahiri; mimi niliweka tu wasifu wa hao kina 'JJ'!
 
Huo ndio ulikuwa ugomvi wake na Ufaransa, mkoloni wa zamani wa Rwanda.
Ufaransa haijawahi kuitawala Rwanda. Rwanda, Burundi na Congo zilikuwa chini ya Ubelgiji. Wakati huo kifaransa kililkuwa ndio lgha rasmi ya ubelgiji na hivyo kwa nchi ilizozitawala!! Ufaransa ilikuwa ikilifunza jeshi la Rwanda wakati wa Habyarimana na huo ndio msigano wao.
 
Ukweli wa machache nnayo yajua mimi ni huu,

ELIMU:

Ule mradi wa laptop moja kwa kila mwanafunzi umefeli kwa sababu ya Rushwa na ilikuwa ni ndoto kutimia kwani zaidi ya nusu ya shule zao hazina umeme, walikuwa wana system kama ya kwetu kutoa mikopo lakini kuanzia mwaka jana serikali imejitoa kudhamini wanafunzi wa elimu ya juu hivyo basi wazazi wanatakiwa wawalipie watoto zao sual hilli limeleta mtafaruku mkubwa Rwanda ila kwa kuwa sheria zao haziruhusu maandamano hakuna aliyepinga hadharani,Wanyarwanda wengi hawajui chochote kinachoendelea kwenye serikali yao, ntafafanua,

Mwaka juzi nilikuwa Rwanda tukiwa tunafanya research ni kuhusu elimu chini ya NGO moja iliyokuwa inataka kujenga shule vijijini.
Maajabu ni kwamba zaidi ya nusu ya watu tuliowauliza watuelekeze wizara ya Elimu ilipo walikuwa hawajui ilipo na cha zaidi vijana wa Kigali wengi wao walitupoteza na kutupeleka mahali ambapo sio au wizara tofauti kabisa, mwisho wa siku kwa tabu sana na hapo napo tulipata ajabu la pili, tulikutana na naibu waziri wa elimu mama mmoja mrembo sana na tulichotaka kutoka kwake ni kutaka kujua ni wapi kuna uhaba wa shule ili tukajenge huko, mama yule akasema kwa yeye Rwanda ni moja hawezi akataja eneo kwani akisema kusini watu wa mashariki watakasirika?!! Mwisho wa siku akasema hajui ni maeneo gani twende ila akatushauri twende kwa wa kuu wa viijij au tewnde ubalozi wa Marekani kuna mtu wa USAID anaye husika na elimu huyo ana data zote za Rwanda, tukasema haya, swali la pili kwake likawa je ni asilimia ngapi ya wanafunzi wanaandikishwa shule kwa mwaka akasema 97% na hiyo 3% inayobaki ni ya watoto ambao wanamapungufu akimaanisha vilema, jamani hata nchi za ulaya na Marekani hawajafikia 97% huo ni uongo mtupu na hakujua kuwa zaidi ya mwezi mzima tulikuwa viunga vya Kigali tukiwahoji watoto wa mitaani ambo hawasomi, Jamani Rwanda si kama tusomavyo kuna omba omba wengi kama miji yetu watoto wa mitaani wapo kila kituo cha daladala wakisumbua abiria kuomba pesa.

Turudi ubalozi wa USA, huko tukakutana na huyo jamaa wa elimu, ofisa yule akasema yeye naye kusema ukweli hajawahi kutembelea kijiji chochote kile analetewa data tu hivyo basi tutafute njia nyingine ya kupata data hizo, nikajua labda ni mpango wa kutokutaka kutupa data lakini si kweli wale watu wanashinda ofisini tu hawajui nini kipo mtaani na hata Kagame nae yupo hivyo hivyo.

UHALISIA WA RWANDA:

Ni nchi mojawapo ambayo wananchi wake wanaishi kwa hofu vibaya mno, ukiwa Rwanda huruhusiwi kuongelea vita ya wahutu na watutsi eti serikali imekataza inataka isahau ila makabila haya mawili yana chuki ambayo si rahisi kusahauluka kuna siku nilikuwa kwenye daladala na rafiki yangu mmoja toka Kenya nikawa namuuliza maswali kuhusu Wahutu yule jamaa hakunijibu na abiria wote walinigeukia kutaka kujua nani kataja neno hilo ikanibidi niongee kiswahili ili kuonyesha mimi ni mgeni na nikasameheka kwa hilo,siku nyingine nikamuuliza msichana wa Kitutsi kama ipo siku anaweza akaolewa na Mhutu akasema hilo halitatokea kamwe kwa chuki aliyonayo na nikagundua kuwa hata NGO iliyonipeleka pale members wote ni watutsi!!! na wakasema kama wahutu walishawahi kuongoza NGO hiyo na hakukuwa na Mtutsi, pata picha, kila ikifika saa kumi jioni Kagame anapeleka majeshi mtaani eti kulinda amani mpaka kesho yake, utaona matruck ya jeshi ya kimwaga askari mitaani wakiwa kwenye mstari mmoja na mikononi wana AK47, fingers on the triger, staili hiyo Kigali inaitwa SINGLE FILE SYSTEM hasa na vijana.

Rwanda naweza kusema ni koloni la Marekani na nchi inayopumua kwa misaada ya USA hakuna nchi East & Central Africa yenye international NGOs kama ile, wananchi wengi wameajiliwa huko, kuna kampuni kubwa chache sana na makampuni hayo yanamilikiwa na wamarekani na hata maofisa wake wengi wamesomea huko akiwa yeye mmoja wapo na kwa taarifa yenu ni kuwa raisi na rafiki zake wanamiliki kampuni karibuni zote kubwa za Rwanda kupitia kampuni yao ambayo kazi yake ni kununua kampuni nyingine.hivyo basi ni miongoni mwa matajiri wakubwa kabisa nchini kwake.

Jamani Rwanda kumetapakaa umasikini mambo yote mnayosoma kutoka Rwandan media yote yamekuwa screened by the government, Rwanda hakuna freedom of media, na sidhani kama kuna private tv/radio zaidi ya mbili,kama moja ipo, ile nchi inaendeshwa na misaada zaidi ya 80%,kodi zao ziko juu zaidi ya kwetu, kuna stori nilipewa kuwa wahisani walikuja kukagua mradi wa barabara na serikali haikutekeleza hilo walichokifanya ni kufumua lami nzuri na kuweka nyingine ili kuonyesha pesa ilipoenda, mpaka mwaka juzi walimu walikuwa wanalipwa wastani wa 42$ kwa mwezi,mpo hapo?

Mpaka leo hakuna anayemjua mrithi wa Kagame ila kuna tetesi anaweza akawa mtoto wake ambaye yupo USA in one of the best millitary academy ambako amesomea baba yake, kama umeshawahi kusikia kule kuna upinzani wa kweli basi tujadili, ana kashfa ya kuwapoteza wapinzani wake na juzi juzi Uganda ililalamika kuwa anatuma majasusi wake nchini humo.

Kwakuwa muda umenitupa kwa leo naishia hapa, ila ukipatamuda vuka mpaka hata kwa wiki 1 tu ukajionee nilichosema ila jiandae kwa matumizi kwani chakula ni gharama nadhani mara tatu ya hapa na hapa sizungumzii kwenye hotel kubwa, asante.
What is your motive, TANZANIA tuna matatizo mengi mno rundo ambayo simply because hatuna raisi kama Kagame hayatatuliki, hebu sema, ulipenda hawa ndugu waliogundua tatizo lao na kutafuta mbinu za kulitatua washindwe? ndiyo hulka gani hiyo ya KiTanzania, wengi hatujui hata nchi yetu inaenda vipi, badala ya kuwaelimisha hawa unaenda ku-research Rwanda haya sema basi report yako imezungumza hayo, kanma sivyo ni kwa nini km siyo unafiki, uchoyo, wivu na hulka zote za kichawi? Hivi unajua matatizo ya Tanzania yote yanaeleweka lakini hakuna 'WILL' ya kuyatatua si raisi wala watendaji wake, sasa wewe unaleta upuuzi wako hapo, Rwanda at least wanjua matatizo yao na solutions wanazitengeneza, hivi wewe, do you really understand the meaning of GENOCID? Watu wamekufa kwa wingi pale, wewe because you're a spectator unaongea tu, as if ni jepesi sana hilo, nataka nikushauri kitu kimoja, fanya research hapa TZ, toa report hapa tutatue matatizo yetu hata kwa kutumia mifano ya nchi zenye kasi ya maendeleo km Rwanda, ni hivi majuzi tu Kagame alisema angepewa tu wizara ya miundombinu bongo nchi ingekuwa tajiri kama zilizoendelea that is a FACT. Wewe unatumia fedha za wapi sijui, naombea zisiwe kodi za waTz masikini kwenda kuishi Rwanda ati research RESEARCH MY LEG! kwa Matatizo tuliyo nayo hapa, ni uchawi kwenda kujaribu ku-troubleshoot nchi ambayo very soon itakuwa imeendelea, halafu raisi wetu anakataa kufananishwa na Rwanda ati ni nchi ndogo kwa population na eneo kuliko TZ wt about China?

Wewe unapoteza tu pesa zetu, BINAFSI NAKULAANI KABISA!
 
Back
Top Bottom