Ukweli kuhusu ndege za Serikali

Wapinzani mnapokosa mambo ya msingi ya kujadili mnakuwa vituko sana. kwa hiyo unalinganisha makampuni ya Bakhresa ambayo yanatafuta faida kubwa na taasisi za serikali ambazo ni kwa ajili ya kutoa huduma?

Kwa hiyo serikali inatoa 'huduma' ya usafiri wa anga au inatengeneza faida?
 
Kwa hiyo biashara ya ndege haina faida?

..unaweza kupata faida.

..lakini unatakiwa u-invest fedha nyingi sana.

..unatakiwa uwe na ndege nyingi za kuweza kuwa na " hub " ya kusambaza abiria maeneo mbalimbali.

..Rwanda, Kenya, Uganda, South Africa, wote wanaendesha mashirika yao kwa hasara.
 
Mtu akikuambia usivuke barabara bila kuangakia kulia na kushoto kabla, ukavuka bila kuangalia hivyo, ukagongwa na gari, akikuambia nilikuambia usivuke bila kuangalia kulia na kushoto kabla hapo maana yake amefurahia umegongwa?

Mbona unaunganisha vitu viwili ambavyo havina uhusiano wa moja kwa moja?

Kusema kwamba serikali imejiingiza katika very risky business bila mipango mizuri si kufurahia serikali kujiingiza hivyo.

Mimi nasikitika sana, ndiyo maana naandika hivi, tusirudie kujimwambafy kwenye mambo yaliyowashinda watu waliyoyaanzisha.

Wewe unafikiri serikali ya Marekani huko ndege zilipoanzia na wanapojua biashara hii kwa miaka mingi zaidi yetu ni wajinga walivyoamua kutokuwa na shirika la ndege la serikali?

Sent from my typewriter using Tapatalk
 
Wapinzani mnapokosa mambo ya msingi ya kujadili mnakuwa vituko sana. kwa hiyo unalinganisha makampuni ya Bakhresa ambayo yanatafuta faida kubwa na taasisi za serikali ambazo ni kwa ajili ya kutoa huduma?
Fanculo wewe, ndege ni huduma? Bibi yako anaweza kupanda bure?
 
Nawahakikishia huyu jamaa hayuko sawa kwenye ubongo.
Nahisi kuna fyuzi imechomoka baada ya zile risasa🤣🤣🤣 siyo bule.

Yani yeye hajui niwatarii wangapi wameletwa na hizo ndege, wamelipa kiasi gani pesa za kigeni kupitia utarii!

Makampuni na mahoteli yakitarii yameingiza pesa kiasi gani!

Yani jamaa hajui yte hayo.
Hopeless
 
Nina uhakika unawachukulia poa wote wanaoongoza sekta hii ya anga, unaongozwa na kukariri maisha kimazoea.

Hakuna aliyeingia kichwakichwa, ondokana na hizi mentality za miaka zote za kitanzania za kuona kuna watu wapo sehemu nyeti na hawajui wanalofanya.

Mashirika yote ya ndege katika kipindi cha corona yanapitia kipindi kigumu, cha ajabu mkuu umeamua kufanya yale yale ya uswahili wetu, kumsimanga mgonjwa wakati wa ugonjwa wake, kumbuka kuwa akipona atarudia katika uzima wa afya yake.
 
Shindwa kabisa

Wewe lazima ni mmoja katika genge linalohujumu uchumi wa nchi!! Hizo ndege mpya zikija zitatia hasara shirika kwani hakuna
Wateja wa kuzipanda!! Ndege hazitakiwi kukaa ardhini zinatakiwa kuwa angani!!
 
Kwa hiyo unabisha? Unasema shirika la ndege halitapata hasara?

Sent from my typewriter using Tapatalk
 
'Watarii', 'utarii' na 'huko mbereni' ndio nini hasa unakusudia kusema? Maana sio typing error kwani umerudiarudia.
Ukijijua wewe ni mjinga ficha ujinga wako usiuweke hadharani

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwahiyo miaka yote wapinza mlikuwa mnalakamika nini kuhusu nchi kuwa na ndege zake? Tulikuwa na Moja, sasa wangeongeza tunalalamika nini jamani? Au ndio siasa za maji taka hizo.......

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa hiyo unabisha? Unasema shirika la ndege halitapata hasara?

Sent from my typewriter using Tapatalk
Hasara wanapata wamiliki wa mashirika makubwa kuliko leru na bado yapo sokoni sembuse sisi.
Unakuwa na mawazo hasi mpaka unasahau ukweli kwamba mwaka huu unaweza kupata hasara na miaka miwili ijayo ukapata faida!.

Kama Bill Gates angekuwa mwoga wa hasara microsoft ingekufa miaka ile ya 1970 baada tu ya kuanzishwa.

Kama walioanzisha facebook wangekuwa waoga wa hasara ingekufa baada ya misukosuko ya mwaka juzi.

Ukiogopa hasara ya muda mfupi siku zote utabakia kuwa lofa tu.
 
Mkuu, uko poa Sana, unajua ukitaka uwe mkuu ni lazima usijaribu kuepuka mfumo wa maisha ulivyo

Elimu inatufundisha kukwepa magumu na changamoto, lakini maisha, yanatufundisha kukabiliana na kila kitu ndipo tutoboze, ulimwengu huu unawahitaji majasiri na sio waoga kama hao, Magu Chapa kazi, kwani haufanyi ili unufaike wewe, Bali vizazi vya mama Tanzania
 
Mkuu, hakuna mwisho kabla ya mwanzo, Anza na mwanzo wako ndipo uwe na mwisho

Utakuwa ni muujiza, ujikute tu uko kileleni bila ya kupanda mlima Kwanza,

Mfumo wa maisha ukiukwepa unakufa masikini hata kama umesoma namna gani,

Maisha hutufundisha kukabiliana na changamoto zote, Ila elimu hutufundisha kukwepa changamoto, kuwa na jicho la mwewe, shauri yako
 
Kufufua shirika la ndege sio lazima ununue madege yote hayo tena bila utaratibu wa manunuzi ya kinchi.

Nyie mkubali mlibaka manifest ya CHADEMA 2015 bila kujua mikakati iliyokuwa imepangwa ili kufufua shirika hilo hata kama walikuwa wanataka kununua ndege zisingekuwa madege yote hayo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hujajibu swali nililokuuliza na swali ulilojibu sijakuuliza.

Unaelewa maana ya methali ya Kiswahili inayosema "Usiige tembo kunya, utapasuka msamba"?

Facebook walioanzisha waliparamia biashara wasiyoiweza?

Unafananisha Shirika la Ndege Tanzania na Facebook?

Sent from my typewriter using Tapatalk
 
Na usipoanza kumuiga tembo kunya Kwa kuchana msamba Kidogokidogo kwa kujizoeza viungo vyako Kwanza, utafikaje kule kuona kawaida kunya kwake?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…