kadovela
JF-Expert Member
- Jan 31, 2016
- 471
- 679
sisi wanaume ni kama wadudu waitwao kumbikumbi. kumbikumbi kihasili makazi yao ni kwenye mashimo ndani ya vichuguu. licha ya kuwa ndani ya mashimo kwenye vichuguu kuna giza kubwa na mwanga hafifu lakini kumbikumbi wanapata chakula na maji ya kutosha, tulizo la uhakika na ulinzi mkali uliowazunguka wa mchwa wenye sumu kali kuwalinda dhidi ya wadudu wakali kama nyoka na kenge, lakini hulka ya kumbikumbi kupenda vitu vinavyonga'aa imewafanya kukumbia shimoni na kufuata mwanga nje na matokeo yake wanaangukia kwenye mikono ya wanadamu na kuishia kukalangwa na kuliwa kama karanga, wengine wanawala hata na ugali. karata nimeshamaliza kucheza karibuni tule kumbikumbi tushushie na myakaya. hawa kumbikumbi wengine wanawaita mbulika.