Mfahamu mnyama muhanga(aardvark)

BRAND

JF-Expert Member
Jun 2, 2013
295
249
1.jpg

Mhanga pia ujulikana kama ( muhanga) wingi ni wahanga ,majina yake mengine ni fundi-mchanga , kiharara, kukukifuku au loma ( Orycteropus afer jina la kisayansi ) kiingereza huitwa aardvark

Ni mnyama apatikanaye barani Afrika Kusini mwa jangwa la Sahara utampata zaid Afrika Kusini,Ethiopia Namibia na Zimbabwe,hapatikani visiwani popote au kwenye misitu yenye mvua nyingi na majimaji ingawaje ni hodari wa kuogelea.

Myrmecophaga tridactyla , ni spishi kubwa kushinda wahanga wote.
Wahanga wakubwa wanakua na pua ndefu na ndimi zao.
Mhanga ni mnyama anayewinda na kufanya kazi zake usiku. Ni mnyama wa pekee ambaye asilimia 99 ya chakula chake ni mchwa.

Mhanga katika maeneo mengine huitwa dubu wa Afrika alaye mchwa au mla mchwa.

Jina lake lilitokana na jina la Kiafrikana lililo na maana ya nguruwe wa ardhini au nguruwe wa mchangani kutokana na hali kwamba mhanga huchimbua ardhi kutafuta mchwa.

2.jpg

Jina lake la kisayansi nililotaja hapo juu
Orycteropus, linamaanisha mguu unaochimbua, na lile la afer , linamaanisha Afrika. Hata hivyo, mhanga, ingawa anajulikana kama nguruwe wa ardhini hana uhusiano wa karibu na nguruwe.Lakini ni mwenye kukaribiana kiumbo na nguruwe hata sura zao

Miguu ya mhanga si mirefu sana. Miguu ya nyuma ni mirefu kuliko ya mbele. Ingawa miguu ya nyuma ya mhanga ina kucha tano, miguu ya mbele ina kucha nne pekee.

Pua yake ndefu imefunikwa na manyoya mengi. Pua hii pia ina mifupa mingi zaidi ya mnyama yeyote yule. Hii ni kwa sababu ya kuweza kustahimili mng’ato wa adui anapochomeka pua hii tunduni kutafuta chakula.

Mhanga huchimbua vichuguu na kuvamia mchwa kwa kutumia ulimi wake mrefu wenye sentimita 30. Ulimi huu una mnato kutokana na mate yake ya gundi.
Mnato huu hunata mchwa kabla ya kubamizwa kinywani. Hata mng’ato wa wale mchwa wakubwa na wakali kama soldier termite si lolote si chochote kwa ulimi wa mhanga kwani ulimi huo una ngozi ngumu inayostahimili ming’ato hafifu kama hiyo. Kwa usiku mmoja, mhanga huweza kula zaidi ya mchwa 50,000 (amini usiamini).

Mhanga anaweza kuzurura kwa usiku mmoja hadi kufikia km 19 mpaka km 30 akitafuta mchwa

Mhanga huishi tunduni baada ya kuvamia mchwa wote. Wakati mwingine mhanga huvamiwa na wanyama wengine wanaokuja kutafuta mabaki ya mchwa au makao.

Mhanga hujihami kwa kuviringa na kutoa mapigo ya kucha zake kali kwa adui. Adui akiwa mkubwa na mkali mfano chui, mhanga huchimbua upenu na kuurusha mchanga nyuma aliko adui na kuumfumba macho kwa machanga pamoja na kufunika njia.
3.jpg
Wakati mwingine, mhanga aendapo kulala shimoni mwake hukutana na wanyama wengine mumo humo waliojificha au waliopata makazi mapya. Yeye hujitolea kukabiliana nao kwa kucha zake kali. Wakati mwingine, mhanga huuliwa na adui wakali hasa majoka makubwa pindi anapozama shimoni kutafuta mchwa .

Mhanga hujitolea kutafuta chakula licha ya hatari anayokumbana nayo. Pia, hujitolea kukabiliana na adui atakayekuja shimoni au atakayepatikana shimoni kiasi cha kupoteza maisha yake wakati mwingine .

Kwa jumla basi, kujitolea mhanga, ni kujitolea kufanya jambo gumu ambalo linaweza hata kusababisha kifo.
.
Msemo huu pia unaweza kumaanisha kujitoa kwa hali na mali ili kuweza kukidhi mahitaji ya maisha.
Hata mtu anayejinyima ili afikie faida fulani huwa amejitolea mhanga.

SIFA ZA PEKEE ZA MUHANGA

1:Huishi had miaka 23

2:Nngumu kumuona mchana

3:Maadui zake wakubwa ni simba, chui, fisi, mbwa mwitu, chatu na binadamu humfanya kitoweo

4:Anaweza kuchimba Shimo na kutokea upande wa pili anapomkimbia adui

5:Matunda pekee yanayoliwa na mhanga ni matango

6:Saa 2 had saa 6 ndio huona vizuri zaid ndio maana hapendi mwanga wala giza nene

7:Sio mkorofi

8:Huwa na uwezo wa kuzaliana baada ya miaka miwili

9:May had July ndio msimu wao wa kuzaliana

10:Hubeba mimba miezi 7

11:Mtoto huanza maisha yake baada ya miezi 6

12:Anakimbia kwa zig zag

13:Hapiti njia moja mara mbili huweza kukaa had wiki ndio apite tena

14:Anapotoka shimoni hutumia hadi dakika kumi akiwa nje ya shimo kucheki noma kabla hajaenda kuelekea mawindoni

15:Akikaribia kuzaa huchimba mashimo mengine jirani kwa ajiri ya dharura kukitokea uvamizi na kutengeneza matundu zaid ya kuchomokea

16:Hawaishi kwenye makundi makubwa

17:Huzaa mtoto mmoja mwenye kilo moja na point

18:Ndiye mnyama anaengoza kwa kukutana na kifo akiwa kwenye utafutaji kutokana na tabia yake ya kutokuwa muoga anapodhamiria jambo lake yeye tabia yake ni "liwalo na liwe lakini lazima mchwa nile"

19:Ni ngumu kuwaona zaidi ya mmoja mara chache sana wanaweza kuwa wengi au wawili,hawa ni "one man army" licha ya udogo wake.

MWISHO

Kuna makabila baadhi ya afrika magharibi wana muenzi muhanga kwa namna tofauti kutokana na ujasiri wake wa kutoogopa hatari yoyote makabila hayo ni Hausa, ayanda,logo na margbetu.

Bila kusahau mungu wa kimisri ya kale ana alama ya kichwa cha mhanga.

Idadi ya wahanga inasemekana inapungua duniani kutokana na usiri wa maisha yao inakuwa ngumu kutafuta namna ya kuwahifadhi kwani kuwaona ni hadi usiku mkali ni mara chache huonekana mchana na mahitaji yao ya chakula ni shida nyingine kuwatunza.
 
kuna imani kwamba ukikuta mahali amechimba porini kuna uwezekano wa kuwepo madini hizi imani zina ukweli wowote?
 
Nimependa ujasili wake
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom