Ukweli kuhusu mshahara wako

Ukweli kuhusu mshahara wako

Pyepyepye

JF-Expert Member
Joined
Jan 6, 2017
Posts
1,940
Reaction score
3,858
(1.) Mshahara wako hautakutajirisha. Maana bosi wako sio mpumbavu wa kiwango hicho.

(2.) Mshahara wako umepangwa ili kutosheleza mahitaji yako ya kila siku na hata ukizidi, hauwezi kukufaa kwa siku 100 zijazo. Sana sana hulautoshlezi kabisaaa.

(3.) Ikiwa kampuni yako inakupa thamani halisi ya huduma unayoitoa, ujue wanafanya kazi kwa hasara na hakuna wajiri mwehu kwa kiwango hicho.

(4.) Mara baada ya kupata ajira (HIRED), wakati wowote unaweza fukuzwa kazi (FIRED) au kustaafu (RETIRED), unaweza pia kujiuzulu wakati utapochoka (TIRED)

(5.) Mshahara ni rushwa unayopewa ili kusahau ndoto, familia, uhuru, kujiheshimu, thamani halisi ya elimu yako, maisha ya kijamii na malengo mengine binafsi.

(6.) Watoto wako hawataweza kurithi nafasi yako katika kampuni hiyo uliyoajiriwa. Ajira sio urithi. Amka kijana.

(7.) Kama mshahara wako hautoshi kulipa bili zako na mahitaji mengine mengi ya msingi na kukubakishia akiba. Yatosha sasa kujiandaa kwa umaskini baada ya kuacha kazi.

(8.) Ikiwa wewe ni mwajiriwa waza zaidi ya kula na kuvaa. Waza uzee, waza magonjwa yanayoweza kukufanya ukalala kitandani kwa muda mrefu ikiwemo kupooza. Utakapo patwa na haya utaweza tumia akiba yako na ikakufaa, je itatosha?

(9) Kuwa mfanyakazi ni sawa na kuwa mtumwa, kuwa mwajiriwa ni sawa na kuwa mke. Kwani unaishi kwa maelekezo ya bosi, wala huwezi kujiamulia tu bila ruhusa ya bosi.

(10.) Kwenye jarida la Forbes linalo ripoti watu matajir duniani, ulishawahi ona tajiri aliyeajiriwa?
Unalojambo la kuufanyia mshahara wako. Tumia mshahara wako kama ufunguo wa kukufikisha kwenye malengo yako.
 
ni kweli kabisa lakini sasa nifanye biashara gani?
 
Motivational speakers noma saana lkn cha ajabu wanaishi kwa hela za viingilio tu hapa town,hawanaga biashara nyingine yoyote ile
Umewachapa kwelikweli,kuongea kwingi hapo hana hata kamradi kakufuga kuku hata wawili
 
Hahah mkuu jamaa kwa kuponda mishahara ndo wenyewe hao.Waulize wenyewe ofisi zao wanauza Product/Service gani utabaki unashangaa tu.

Eti mshahara ni kama rushwa kwako,hahah
 
Kuna mmoja kama hawa akawa anajisifia kuwa aliacha kazi akajiajiri anatuponda kwelikweli anadai yeye ameshatoboa maisha ile anainuka suruali inabonge la kiraka na kiatu kimepinda upande,Mungu si athumani nikakutana nae kumbe anauza genge
 
Huu ni ukweli mtupu ila walengwa sijui kama wataufurahia, sana utakuwa umewaharibia siku zao kwa weekend yote hii na pia kila wapokeapo mshahara. Ni chungu lakini Tiba.
 
Motivational speakers noma saana lkn cha ajabu wanaishi kwa hela za viingilio tu hapa town,hawanaga biashara nyingine yoyote ile
Ulitaka waishi kwa pesa gani?Timu kubwa za ulaya zina pesa kwa sababu ya viingilio vya mashabiki
 
Hahah mkuu jamaa kwa kuponda mishahara ndo wenyewe hao.Waulize wenyewe ofisi zao wanauza Product/Service gani utabaki unashangaa tu.

Eti mshahara ni kama rushwa kwako,hahah
Jadili maada achama na Personer attack. Kuanza ku attack mtu ni dalili za kwamba huna uwezo wa kujenga hoja
 
sio lazima sote tuwe matajili wengine inapendeza tukawa kweny kiwango cha kati....alafu utajili wa Afya ndo tuanauitaji sana .
 
Kuna mmoja kama hawa akawa anajisifia kuwa aliacha kazi akajiajiri anatuponda kwelikweli anadai yeye ameshatoboa maisha ile anainuka suruali inabonge la kiraka na kiatu kimepinda upande,Mungu si athumani nikakutana nae kumbe anauza genge
Kwani kuuza genge sio biashara? Au uliambiwa biashara ni kuwa na Yard ya kuuza Magari?

Anauza genge anapata pesa yake, unajua MacDonard mgahawa walianza vipi?

Usha wahi kusoma jinsi cocacola walivyo anza?

Usha wahi soma yule Mmiliki wa Amazon alivyo anza na hata offisi yake ya mwanzo alio kuwa anatumia?

Biashara si kuwa na Ofisi ya AC biashara ni malengo.

Hilo genge lake kuna watu wanaenda kupata huduma na anapata pesa
 
(1.) Mshahara wako hautakutajirisha. Maana bosi wako sio mpumbavu wa kiwango hicho.

(2.) Mshahara wako umepangwa ili kutosheleza mahitaji yako ya kila siku na hata ukizidi, hauwezi kukufaa kwa siku 100 zijazo. Sana sana hulautoshlezi kabisaaa.

(3.) Ikiwa kampuni yako inakupa thamani halisi ya huduma unayoitoa, ujue wanafanya kazi kwa hasara na hakuna wajiri mwehu kwa kiwango hicho.

(4.) Mara baada ya kupata ajira (HIRED), wakati wowote unaweza fukuzwa kazi (FIRED) au kustaafu (RETIRED), unaweza pia kujiuzulu wakati utapochoka (TIRED)

(5.) Mshahara ni rushwa unayopewa ili kusahau ndoto, familia, uhuru, kujiheshimu, thamani halisi ya elimu yako, maisha ya kijamii na malengo mengine binafsi.

(6.) Watoto wako hawataweza kurithi nafasi yako katika kampuni hiyo uliyoajiriwa. Ajira sio urithi. Amka kijana.

(7.) Kama mshahara wako hautoshi kulipa bili zako na mahitaji mengine mengi ya msingi na kukubakishia akiba. Yatosha sasa kujiandaa kwa umaskini baada ya kuacha kazi.

(8.) Ikiwa wewe ni mwajiriwa waza zaidi ya kula na kuvaa. Waza uzee, waza magonjwa yanayoweza kukufanya ukalala kitandani kwa muda mrefu ikiwemo kupooza. Utakapo patwa na haya utaweza tumia akiba yako na ikakufaa, je itatosha?

(9) Kuwa mfanyakazi ni sawa na kuwa mtumwa, kuwa mwajiriwa ni sawa na kuwa mke. Kwani unaishi kwa maelekezo ya bosi, wala huwezi kujiamulia tu bila ruhusa ya bosi.

(10.) Kwenye jarida la Forbes linalo ripoti watu matajir duniani, ulishawahi ona tajiri aliyeajiriwa?
Unalojambo la kuufanyia mshahara wako. Tumia mshahara wako kama ufunguo wa kukufikisha kwenye malengo yako.
Ukweli mchungu lakini ndo hivyo,umesomeka sana kiongozi kwa kweli tubadili mindset yetu kuhusu ajira.
 
Back
Top Bottom