Ukweli kuhusu mshahara wako

Ukweli kuhusu mshahara wako

Unahamisha magori?.jadili alicho post achana na yeye hata kama anashindia mihogo au anaishi kwa shemeji
Safii. Mtu anaanza kumjadili mwandishi baada ya kujadili ujumbe. Jitu linataka sijui aje apa aseme nna gari 4 nyumba 3 etc ndo liamini.
 
Vijana tujadili hoja hizi,mimi nakaribia kuacha kazi na kujiweka mbali kabisa na siasa, taarifa za habri zenye siasa naacha kwa mwaka mmoja then nitaleta mrejesho hapa,tuombe uzima. Mtoa mada shukrani kwa kutukumbusha hili
 
Kwani kuuza genge sio biashara? Au uliambiwa biashara ni kuwa na Yard ya kuuza Magari?

Anauza genge anapata pesa yake, unajua MacDonard mgahawa walianza vipi?

Usha wahi kusoma jinsi cocacola walivyo anza?

Usha wahi soma yule Mmiliki wa Amazon alivyo anza na hata offisi yake ya mwanzo alio kuwa anatumia?

Biashara si kuwa na Ofisi ya AC biashara ni malengo.

Hilo genge lake kuna watu wanaenda kupata huduma na anapata pesa
Sijasema ni vibaya kuuza genge, ila ni ustadi wake wa michanganuo yake ya kibiashara na akidai yeye ndiyo iliyomfikisha hapo kumbe anachotushauri sicho anachokifanya na ametoa ushuhuda wa uongo
 
Umenena lakin only fittest people ndo watakao survive.. na sio employed na kama ni employed tafuta chako sepa.
 
sio lazima sote tuwe matajili wengine inapendeza tukawa kweny kiwango cha kati....alafu utajili wa Afya ndo tuanauitaji sana .
Kitu ambacho hatujui ni kuwa duniani tunategemeana kwenye utoaji huduma ungeanza Kwanza na burter trade mpaka sasa ungepata jibu sahihi na ungeipuuza hi thread sio kila kitu lazima kiwepo Kwa vile unataka hapana sometimes nature of existence lead us to life, keep it in your brain mkuu
 
Kwa hiyo watu waache kazi ?

Sasa tukiwa wote matajiri tutasaidianaje? nani atayefanya kazi za mwenzie?

Tuache kudanganya watu hakunà kazi ngumu kama kutunza Pesa ni Kipaji sio kila mtu anacho.
Hakuna mtu ambaye hataki kuwa tajiri. Mazingira, umasikini, serikali na mtu mwenyewe vinaweza sbbsha ukawa masikini au tajiri.
Basi ww endelea kuwa masikini ili uwafanyie watu kazi
 
Kitu ambacho hatujui ni kuwa duniani tunategemeana kwenye utoaji huduma ungeanza Kwanza na burter trade mpaka sasa ungepata jibu sahihi na ungeipuuza hi thread sio kila kitu lazima kiwepo Kwa vile unataka hapana sometimes nature of existence lead us to life, keep it in your brain mkuu
Siyo burter ni Barter trade.
 
Kuna mmoja kama hawa akawa anajisifia kuwa aliacha kazi akajiajiri anatuponda kwelikweli anadai yeye ameshatoboa maisha ile anainuka suruali inabonge la kiraka na kiatu kimepinda upande,Mungu si athumani nikakutana nae kumbe anauza genge
Duhhh!!!
 
(1.) Mshahara wako hautakutajirisha. Maana bosi wako sio mpumbavu wa kiwango hicho.

(2.) Mshahara wako umepangwa ili kutosheleza mahitaji yako ya kila siku na hata ukizidi, hauwezi kukufaa kwa siku 100 zijazo. Sana sana hulautoshlezi kabisaaa.

(3.) Ikiwa kampuni yako inakupa thamani halisi ya huduma unayoitoa, ujue wanafanya kazi kwa hasara na hakuna wajiri mwehu kwa kiwango hicho.

(4.) Mara baada ya kupata ajira (HIRED), wakati wowote unaweza fukuzwa kazi (FIRED) au kustaafu (RETIRED), unaweza pia kujiuzulu wakati utapochoka (TIRED)

(5.) Mshahara ni rushwa unayopewa ili kusahau ndoto, familia, uhuru, kujiheshimu, thamani halisi ya elimu yako, maisha ya kijamii na malengo mengine binafsi.

(6.) Watoto wako hawataweza kurithi nafasi yako katika kampuni hiyo uliyoajiriwa. Ajira sio urithi. Amka kijana.

(7.) Kama mshahara wako hautoshi kulipa bili zako na mahitaji mengine mengi ya msingi na kukubakishia akiba. Yatosha sasa kujiandaa kwa umaskini baada ya kuacha kazi.

(8.) Ikiwa wewe ni mwajiriwa waza zaidi ya kula na kuvaa. Waza uzee, waza magonjwa yanayoweza kukufanya ukalala kitandani kwa muda mrefu ikiwemo kupooza. Utakapo patwa na haya utaweza tumia akiba yako na ikakufaa, je itatosha?

(9) Kuwa mfanyakazi ni sawa na kuwa mtumwa, kuwa mwajiriwa ni sawa na kuwa mke. Kwani unaishi kwa maelekezo ya bosi, wala huwezi kujiamulia tu bila ruhusa ya bosi.

(10.) Kwenye jarida la Forbes linalo ripoti watu matajir duniani, ulishawahi ona tajiri aliyeajiriwa?
Unalojambo la kuufanyia mshahara wako. Tumia mshahara wako kama ufunguo wa kukufikisha kwenye malengo yako.
Sawa, wamekusikia wanotaka utajiri...! Mimi nahitaji pesa ya kuendesha maisha yangu tu.
 
Lazima utambue kuwa wote hatuwezi kuwa matajiri, haitakaa itokee na hao matajiri wamefanikiwa kwa juhudi za wafanyakazi wanaolipwa mshahara huo unaouponda....

Maisha ni kutegemeana...Huo mshahara unauponda ndio unafanya watu waishi na kuendesha maisha yao

Lengo la maisha ni kuishi sio kuwa tajiri kwani mwishoni ukifa hutazikwa na utajiri wako.. Tafakari
 
mada kama hizi zinatakiwa zitolewe na watu ambao wameishia darasa la 7 au form 4 ,ni aibu kwa mtu mwenye elimu kuanzia degree ku support mada kama hii.
 
Motivational speakers noma saana lkn cha ajabu wanaishi kwa hela za viingilio tu hapa town,hawanaga biashara nyingine yoyote ile
Sure mkuuu...jamaa niliwah kumwambia hawa wanajiita motivational speakers hakuna kitu baadh yao hawana magumu mengi kama baadh ya watu mtaan mengi sanasema hayana uhalisia na maisha yao
 
Back
Top Bottom