Ukweli kuhusu maziwa ya soya (soy milk)

cadey

JF-Expert Member
Oct 14, 2014
1,455
4,410
Je ni upi Mchakato sahihi wa kuandaa soya kwa ajili ya maziwa ili kumuepusha mtumiaji na side effects za soybeans,?

maana nimesikia na kusoma Mengi kuhusu maharage ya soya ,sokoni yapo maharage ya soya yasiyokobolewa na yaliyokobolewa sielewi yapi yanafaa kwa ajili ya maziwa,

Naona unga wa lishe asilimia kubwa unachanganywa na soya je ni salama wa watumiaji hasa watoto.?

Je soya inaweza kuwa salama kwa watumiaji endapo itaandaliwq kama inavyotakiwa?
 
Underrated thread!

Soya ni nzuri sana mkuu, kama ulivyosema inatumika kwa unga wa lishe ni sahihi kabisa kutokana na kuwa na kiwango kikubwa cha protein kuzidi hata maziwa ya ng’ombe. Ikumbukwe protein ni content kubwa zinazotakiwa kwa mtoto hata watu wazima.

Maandalizi, chukua soya loweka kwenye maji kwa muda mrefu( loweka usiku asubuhi andaa), chukua soya ulizoloweka usiku pikicha kuondoa maganda ya juu kisha saga kwenye blander kwa kuongeza maji kidogo ili upate ule urojo au uji uji kisha chuja kwa kitambaa sahihi ili kupata yake maji yanayofanana na maziwa.

Hadi hapo utakua ushamaliza kuandaa unaeza kuchemsha na kuweka sukari/athari ili kuongeza ladha na tiyari kwa matumizi.
 
Back
Top Bottom