Ukweli kuhusu Madiwani watano wa ACT Wazalendo waliohamia CCM

Abdul Nondo

JF-Expert Member
Oct 28, 2016
515
2,875
Habari wakazi wa kigoma-Ujiji na watanzania wote.

Nimeona leo chereko chereko pale ofisi ya Lumumba-CCM. Makada na viongozi wakicheka na kufurahia kupokea madiwani kutoka ACT - Wazalendo kuhamia CCM waliopanda ndege kutoka Kigoma kuja kujiunga na CCM Dar es salaam (Lumumba).

Madiwani wote (5) waliohamia CCM ninawafahamu vyema, Fuwadi Seif ni kaka yangu na pia ni rafiki wa baba yangu na siku 5 zilizopita alinitafuta kwa texts kutaka tuongee ila hakunipata na sikuwahi mpata tena. Hamdun ni mzee wangu nimekulia na kucheza kwake, Ismail, Ngongolwa (Ndege boy ), Hamis wote hawa ninawafahamu na ninawaheshimu sana.

Kila mtu ana haki ya kuhamia chama anachokipenda. Na sio kosa kabisa wao kuhamia CCM kutoka ACT Wazalendo.

Mwalimu Nyerere aliwahi kusema "CCM sio mama yangu" na "Lowassa akaongezea akisema "CCM sio mama yangu wala baba yangu " alipohamia Chadema mwaka 2015.

Kabla ya serikali ya awamu ya 5, tulizoea kuona watu wakihama kutoka katika vyama vyao aidha kwa sababu ya migogoro ndani ya chama, kufukuzwa au pia kutoridhishwa na utendaji au itikadi ya chama chake kwa muda huo.

Ila sasa hivi mwenye macho anaona na mwenye masikio anasikia, yaani viongozi waliochaguliwa na wananchi wanatangaza kuhamia CCM mbele ya vyombo vya habari na wananchi wao waliowachagua huku viongozi hao wakisema wamekoshwa na utendaji wa Mh. Rais yaani Rais sasa hivi anafanya kila kitu hivyo wao hawapaswi kuwa viongozi sababu Rais anafanya kila kitu na hivyo wanajiuzulu ili kuunga mkono juhudi.

Hizi ni akili za hovyo kabisa, kana kwamba wananchi wao sasa hivi hawana shida yeyote tena wanaishi kama wapo peponi.

CCM wanawatumia hawa madiwani wa Kigoma kujiunga CCM wakidhani ndio njia ya kuisaidia CCM kuonekana inakubalika Jimbo la Kigoma mjini, wakidhani ni njia ya kumkomesha Mbunge Zitto Kabwe, wakidhani ni njia ya kuisambaratisha ACT wazalendo, wakidhani ni njia ya kuonesha kwamba Mh.Magufuli anakubalika Kigoma.

Hizi ndio sababu za CCM kuwanunua hao madiwani sio kwasababu wamewapenda sana ila ni njia ya kuwatumia tu kama Big-G na watawatema tu.

Ukweli ni kwamba hakuna diwani kati hao aliyejiunga na CCM kwa lengo la kuunga mkono juhudi za Mh. Rais au kuipenda CCM.

Ila ni kwasababu zilizo katika kategori kuu mbili, ambazo ni Pushing factors for defection (Sababu zilizowasukuma wao kutoka ACT kuhamia CCM) na Pulling factors for defection (Sababu zilizowavuta wao kutoka ACT kwenda CCM).

Nianze na Pushing factors for defection (Sababu zilizowasukuma wao kutoka ACT kuhamia CCM).

1. Kutokuwa na uhakika katika kura za maoni kugombea tena udiwani katika uchaguzi mkuu 2020.

Kutokana na uwezo wao mdogo wa uwajibikaji katika kata zao.

Hivyo hawakuwa na matumaini tena hivyo wakaona njia nyepesi ni kwenda CCM.

Mfano:

a) Fowad Seif Diwani wa Kata ya Kasimbu. Hajawahi kukaa kikao cha kata (Ward C) na wenyeviti, afisa watendaji mtaa wala wa kata tangu 2015.

Hajawahi fanya mkutano na wananchi wake tangu 2015 mbali na kupewa fedha bure na taasisi ya KDT za kufanya mikutano akala, amewahi pewa barua na chama kwa kujihusisha na rushwa na alikuwa mtoa siri za chama alipewa onyo mara zote na alikuwa na tamaa ya kupewa kamati Halmashauri.

Hivyo alijua hachaguliwi tena ndio maana alitaka ahamie kata ya Kitongoni. Ila akaona pale hakuna nafasi hiyo ametimkia CCM.

b) Ismail Mahmoud
Diwani wa Kagera. Hakuwa tena na matumaini sababu alikuwa anajua fika chama hakitampitisha kura za maoni kutokana na utendaji wake.

Alishindwa kutumia fedha za miradi ya kata, alikata miti ya mikorosho akauza fedha (Mil.2 na laki 6) akala yeye na watendaji wake bado anachunguzwa, alishindwa hata kusimamia ujenzi wa matundu ya vyoo ya shule ya msingi Kagera.

Hivyo alikuwa anajua kwamba hawezi tena kupita kura za maoni.

c) Hamis Rashid, huyu ni diwani wa Gungu.
Alikuwa anaishi kwa hofu kubwa kutoka na shutuma zake za uuzaji wa open space ya machinjio, pia baada ya kusikia Katibu wa Jimbo Kigoma, Ndugu Iddy Sivya kwamba ana nia ya kugombea udiwani Gungu, hii imemkatisha tamaa na matumaini kabisa. Hivyo akaona atimkie CCM.

d) Mussa Mngongolwa (Ndege Boy).
Huyu ni Diwani wa Kipampa. Hata yeye hakuwa na matumaini yeyote kuendelea kuwa Kiongozi sababu ya uwezo wake moja, mosi katika ilani yake aliahidi zahanati Ila hakuwa na fedha, akadai ana kiwanja Mh. Mbunge akapendekeza fedha itoke kutoka mfuko wa maendeleo ya jimbo ili iende kujenga zahanati.

Kumbe hata kiwanja hana alienda vamia kiwanja cha mtu, mgogoro mkubwa ukainuka kati yake na viongozi wa serikali ya mtaa.

Hivyo wananchi waliapa kutompigia kura sababu ya kutotekeleza ahadi. Ndege Boy alipewa kukusanya ushuru wa maji ya Rutale, kwa wachotaji beskeli, toroli kwa siku ni 500, magari kwa siku 2000 ili fedha hizi zisaidie kidogo maendeleo ya kata Ila fedha zote diwani huyu alikula zote (Shahidi Mfisa mtendaji wa mtaa Filipo Maganga tayari amestasfu)

Huku wananchi wakidai mapato na matumizi bila mafanikio. Chama kilimpa barua ya onyo na barua ya kuagiza fedha hizo azilipe na atoe mapato na matumizi kwa wananchi.

Hatimaye amehamia CCM bila kulipa fedha wala kutoa mapato na matumizi kwa wananchi.

e) Hamduni Nassoro, huyu ni mzee wangu, nimekulia na kucheza nyumbani kwake. Ni diwani wa Kata yetu ya Kasingirima, Hamduni tangu mwanzo alikuwa ana hofu kuwa hawezi pita hofu yake kubwa ilikuwa ni fedha za uchaguzi akiwaza kwamba washindani wake wa CCM wanatumia fedha sana kurubuni Vijana, yeye akajiona hana fedha za kuhonga ili achaguliwe hatimaye ameamua kuhamia CCM penye fedha za kuhonga vijana ili achaguliwe bila kujua vijana wa Kigoma - Ujiji sio mazwazwa au mazezeta wana akili timamu wanakula fedha ukiwahonga na kura hawakupi.

Pia aliwahi toa kauli kwa wananchi kwenye mkutano wake kwamba "Mwananchi mwenye shida asimfuate kwake,aende Ofisini "hii kauli iliwakera sana wananchi.

Hatimaye ameamua kuhamia CCM akidhani atamshinda Mlekwa Mfaume wa CCM, Mzee York wa CCM, Abdallah Kiembe wa CCM katika kura za maoni, labda Kama wameahidiwa na Katibu mkuu wa CCM Bashir Ally au Polepole kwamba watapitishwa bila kupingwa kugombea udiwani labda.Ila kama ni hivi ni huzuni kubwa kwa Mzee wetu Mzee York, Mwenyekiti Mlekwa Mfaume na rafiki yangu Abdallah Kiembe kwani wamekuwa wakijipanga sana na udiwani kugombea upande wa CCM.

Pulling factors for defection (Sababu zilizowavuta wao kutoka ACT kwenda CCM).

1. Fedha walizopewa na ahadi za kupitishwa katika kura za maoni kugombea tena udiwani uchaguzi huu wa 2020.

Huwezi chaguliwa na wananchi ukaamua kuacha alafu ukapanda ndege hadi Dar es saalam Lumumba, ukajiuzulu udiwani na kuhamia CCM kwa lengo la kuridhishwa na maendeleo ya Mh. Rais bila kuwepo kwa maslahi au makubaliano, ndio maana kulikuwa na vikao vilivyokuwa vinaendelea na watu waliotumwa kutoka CCM Taifa katika nyumba ya Diwani mmoja kati ya waliokwenda CCM.

2. Kudhani kwamba uchaguzi wa 2020 utakuwa Kama wa serikali za mitaa kudhani kwamba watapita bila kupingwa. Na kuthani upinzani wataendelea kuonewa na kudhulumiwa tu.

CCM imewatumia hao madiwani na wao bila kujua .Asili ya mji wetu Kigoma - Ujiji ukihamia kwenda CCM bila sababu za msingi kama hizo walizotoa, hawawezi kushinda tena, yaani waelewe kuwa tayari wameisha kisiasa.

Kama CCM - Taifa akina Dr. Bashiru na Polepole watalazimisha hao waliojiunga CCM wapitishwe kwa lazima katika kura za maoni, CCM itapasuka pasuka kila kata ya uchaguzi.

Kama kutakuwa na kura za maoni CCM, hao waliohamia hawatapenya sababu kuna watu tayari wamejipanga kwa muda mrefu kugombea CCM, mfano kata ya Kasingirima kuna Mlekwa Mfaume, Mzee York, Abdallah Kiembe wote hawa ni CCM. Hivyo Mzee wangu Hamdun sidhani kama atafua dafu.

Mwisho, nakumbusha CCM kata zote katika uchaguzi huu 2020 na Jimbo linarudi ACT-Wazalendo hayo tunakumbushana tu.

Abdul Nondo.
abdulnondo10@gmail.com
0772151432.

FB_IMG_1581549592630.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mwisho,nakumbusha CCM kata zote katika uchaguzi huu 2020 na Jimbo linarudi ACT-WAZALENDO hayo tunakumbushana tuu.
Abdul Nondo.
Yaani Chadema walikusaidia weee wakakupigania weweee VIKESI VYAKO.

Badala ya kuipigania Chadema unawapigania ACT WAZALENDO kuwa hilo jimbo Chadema wasahau.SAWA MESEJI SEND KWA CHADEMA WAO HAWANA CHAO KWENYE HILO JIMBO

kweli shukrani ya punda ni mateke

Chadema hiki kitoto KI Abdul Nondo mlishokisaidia mnaona kinavyowarushia mateke? Mbowe upo?
 
Kijana lazima uelewe kuwa huwezi kupambana na ukweli na ukashinda lakini pia ukweli una tabia ya kujilipiza kisasi kama utapuuzwa.

Kumbuka kuna watu/wabunge/madiwani waliupuuza ukweli na wakawa wanaita waandishi wa habari na kuandika kwenye mitandao wakiwaponda wale wabunge na madiwani waliokuwa wakihama vyama vya upinzani na kujiunga CCM lakini kwa sababu ukweli haupuuzwi, leo hii hao hao wamejiunga pia CCM.

Hatuwezi kushangaa tukisikia hata wewe pia umejiunga CCM kwa sababu mbinu unayotumia ya kupuuza ukweli imeishatumiwa na wengine ambao leo wako CCM.

Leo hawa madiwani unadai walikuwa hawafai baada ya kukihama chama cha ACT-Wazalendo lakini unashindwa kuelewa kuwa hoja yako inatoa angalizo kuwa chama cha ACT-Wazalendo kinalea viongozi ambao hawafai na hawawezi tena kushinda katika chaguzi zijazo.

Badala ya kujiuliza kwa nini wanahama na mfanye nini ili kuzuia hamahama ya madiwani wenu wa ACT-Wazalendo, unachofanya ni kutueleza sababu za wao kuhama.

Hoja ya msingi sio sababu ya wao kuhama bali mnatakiwa mfanye nini ili wengine wasihame na kujiunga CCM.
 
Hawa Madiwani nawakumbusha toka enzi ya Dr, Aman Waridi Kaburu (R.I.P.) ,akirejea toka ughaibuni kipindi cha Mageuzi, na kuwa Mbunge Chadema,na hata baada ya kuhamia CCM,

Kigoma uwa ni ngone ya Upinzani wewe njoo na Mbwe Mbwe zako sijui hamia CCM ,unga Mkono juhudi Kigoma utapigwa chini asubuhi tu.

Kitu ambacho Wananchi wa Kigoma hawataki kusikia ni neno.CCM.
 
Hawa Madiwani nawakumbusha toka enzi ya Dr, Aman Waridi Kaburu (R.I.P.) ,akirejea toka ughaibuni kipindi cha Mageuzi, na kuwa Mbunge Chadema,na hata baada ya kuhamia CCM,

Kigoma uwa ni ngone ya Upinzani wewe njoo na Mbwe Mbwe zako sijui hamia CCM ,unga Mkono juhudi Kigoma utapigwa chini asubuhi tu.

Kitu ambacho Wananchi wa Kigoma hawataki kusikia ni neno.CCM.
Kigoma haijawahi kuwa ngome ya wapinzani labda kama huijui historia na tabia ya watu wa Kigoma!

Watu wa Kigoma hufuata upepo wa kisiasa na jina katika kuchagua viongozi wa kisiasa ndio maana hawa madiwani 5 wamehamia CCM kwa sababu wamejua upepo wa kisiasa unaelekea wapi.

Tabia ya wananchi wa Kigoma kuchagua kiongozi kufuatana na upepo wa kisiasa na jina hutafsiriwa na baadhi ya watu kuwa wana kigeugeu au hawana msimamo thabiti lakini nadhani sio kweli.

Kumbuka hata Zitto ilibidi abadilishe Jimbo la Uchaguzi baada ya kugundua upepo wa kisiasa sio mzuri katika Jimbo lake na akahamia Jimbo la Kigoma Mjini mwaka 2015.
 
Yaani Chadema walikusaidia weee wakakupigania weweee VIKESI VYAKO.

Badala ya kuipigania Chadema unawapigania ACT WAZALENDO kuwa hilo jimbo Chadema wasahau.SAWA MESEJI SEND KWA CHADEMA WAO HAWANA CHAO KWENYE HILO JIMBO

kweli shukrani ya punda ni mateke

Chadema hiki kitoto KI Abdul Nondo mlishokisaidia mnaona kinavyowarushia mateke? Mbowe upo?
Chadema hainunui hii bidhaa yako mbovu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom