Ukweli kuhusu kilimo cha machungwa

Mkulima na Mfugaji

JF-Expert Member
Jul 26, 2013
1,013
1,634
Habar wanajamvi, nimeona nirudie hii mada kuhusu kilimo cha machungwa, maana nimeona watu wakidanganyana kuhusu kilimo cha machungwa, mimi ni mkulima mdogo wa zao hili na hiki ninachotoa ni uzoefu kutoka field sio kukopi mtandaoni.

Mimi nipo Muheza Tanga na mkulima mdogo wa machungwa. Mbegu zipo nyingi ila zinazotumika kwa sasa ni msasa na valencia. Tofauti yake ni kwamba msasa unakomaa mapema na unakulazimisha kuuza mapema mbegu hii hulimwa na wakulimawenye kipato cha chini ambao hawawezi kuvumilia njaa. Bei yake shambani huanzia Tsh. 20 mpaka Tsh 50.

Valencia ndio mbegu inayopendwa na wakulima wengi kwani inaweza kukaa muda mrefu shambani. Pia chungwa linaweza kuuzwa mpaka Tsh 100 au zaidi ya hapo.

UNAPATAJE FAIDA?
Ukiwa na shamba ekari moja inaweza kuingia michungwa 80 ambao utakapokomaa vizuri unaweza kuzaa hata machungwa 1000. Wekea umezaa machungwa 800 zidisha mara michumgwa 80 unapata 64000 zidisha mara 100 kama ni valencia unapata Tsh 6400000/=

GARAMA ZA KUHUDUMIA
Shamba la michungwa litahitaji huduma za ukaribu katika miaka mitatu ya mwanzo baada ya hapo itakuwa ni kulimia tu na kufanya usafi Mwingine kama prunning ambazo hazifiki hata laki tano kwa mwaka. Kumbuka hapo nimepiga hesabu ya ekari moja tu.

CHANGAMOTO
Machungwa hasa valencia uwezekano wa kushambuliwa namagonjwa ni mdogo sana changamoto kubwa ni wezi na
machungwa kuanguka kama utakuwa unasubiri bei kubwa.

SOKO
Zamani soko la machungwa lilikuwa ni changamoto kubwa kwani mikoa iliyokuwa inapokea machungwa ilikuwa ni Dar na Arusha tu ila kwa sasa soko ni kubwa mpaka Nairobi na Mombasa kwa mfano inafikia kipindi ukiwa na machungwa
shambani wateja wanakusumbua wewe.

UPATIKANAJI WA MASHAMBA
Mashamba yanapatikana ila kwa tabu na bei yake iko juu kidogo.

KUHUSU WAFANYAKAZI
Wafanyakazi wanapatikana pia unaweza kujenga nyumba ya kawaida shambani na Mtu akakaa huko huko kwa Ulinzi.
Nafikiri nimekujibu japo kidogo. Pia nimepiga hesabu ya ekari moja na pia mchungwa unaweza kuzaa mara mbili kwa mwaka.
 
Sijajua jiografia ya kasuru kama machungwa yanakubali, kama yanakubali basi otesha miche ya milimau halafu unafanya burding na hiyo valencia, unaweza Pata mbegu kwa kuagiza kama una ndugu maeneo ya Muheza Tanga
Samahani nipo kasulu nawezaje kupata hizo mbegu za Valencia?
 
Mkuu hongera sn kwa jitihada zako shambani pia tunashukuru kwa ufafanuzi mfupi na unaoleweka kuhusu machungwa, nilikua naomba kujua malimao na ndimu kdg uotaji wake ni muda gani na changamoto katika wadudu , natanguliza shukran
 
Kuhusu ndimu sina uzoefu nazo ila malimao yanachukua mpaka miaka Mitano kuzaa kwani unaanza kuotesha kitalu cha malimao na kupeleka shamba mche wa mlimao ila ukichanganya kuzaa unaweza kuzaa mpaka malimao 3000
Mkuu hongera sn kwa jitihada zako shambani pia tunashukuru kwa ufafanuzi mfupi na unaoleweka kuhusu machungwa, nilikua naomba kujua malimao na ndimu kdg uotaji wake ni muda gani na changamoto katika wadudu , natanguliza shukran
 
Hongera Sana kaka kwa jitihada hizo. Mimi ninavutiwa na kilimo cha michungwa na minazi naamini ni mazao yanayoweza kukaa miaka na miaka huku ukiendelea kuvuna na kulihudumia kwa gharama ndogo.

Swali langu ni je mti wa mchungwa huweza kuvunwa kwa miaka mingapi kabla haujachoka?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom