"Ukweli" kuhusu kifo cha RPC Barlow ni huu hapa...

Baija Bolobi

JF-Expert Member
Feb 25, 2009
1,093
1,726
Mod Tafadhali usiunganishe thread hii. Najua iko inayoripoti kifo, iko ya maswali.

Hii inahusu majibu na revelations zilizoingia kwenye dish langu.
===========

-Kamanda Barlow alikuwa na mwanamke ndani ya gari wakiwa peke yao wawili
-Mwanamke si dada yake wala ndugu yake
-Lilikuwa gari la binafsi na Kamanda aliendesha mwenyewe.
-Walitoka kwenye kikao La Kairo Hotel na siyo Florida Hotel kama IGP alivyosema katika taarifa yake
-Walipofika Kitangiri, Kamanda aliamua kumpeleka yule mama ndani kwnye uchochoro badala ya kumwacha barabarani
-Si mara ya kwanza Kamanda kumpeleka mama yule eneo lile
-Walipoingia uchochoroni, waliwakuta the so called "polisi jamii" wakiwa kwenye doria
-Kamanda alishusha kioo na kuwauliza ni kina nani, na wao walimjibu kuwa ni polisi jamii.
-Aliwahoji kwa nini wamevaa mikanda ya polisi wakati waliishazuiwa
-Ulitokea ubishi kidogo
-Kamanda akainua redio call kuwaita vijana wake waje kuwakamata
-Polisi jamii wakamdaka kumnyanganya redio call hiyo na kumpiga risasi ya shingoni
-Wakamvuta na kumlaza chini ya uvungu wa gari
-Yule mama ndiye aliyemwita mlinzi wa RPC na kumwambia aje kumchukua "mzee" maana ameuawawa
-Mama anaisaidia polisi hata sasa.

MY Take:

-Jeshi la polisi linajaribu kusafisha hali ya hewa kwa kufanya damage control
-Mme wa mama yule amekuwa akilalamika kuwa analiwa mali yake
-Kuna uwezekano, polisi jamii walijua kamanda anakuja saa ile na yule mama, na walitekeleza maagizo waliyopewa
-Kuna other underlying issues ndani ya jeshi la polisi Mwanza
-Uchunguzi hautapata ushirikiano wa kutosha kwa sababu ya chuki kubwa kati ya jamii na jeshi hilo.

 
Hoja ya kuuwawa na majambazi haiingi akilini hata kidogo. Muda utasaidia kujua nini hasa sababu ya mauaji haya. Hata hivyo, toka lini polisi jamii wanatembea na bunduki kwenye kuangalia usalama wa maeneo yao? Huo pengine ulikuwa mtego.
 
naona muda unaanza kuamua now yote yaliyobehind the scene yatagundulika muda utasema
 
Kwa jinsi JF ilivyo, ukweli wote utajulikana tu, ni suala la muda tu. Inahitaji zaidi ya busara kwa jeshi la polisi kuhandle hii issue properly, vinginevyo litajivua nguo!! Subirini muone.
 
Tatizo ni kwamba huyo mama anaisaidia polisi ambayo mwisho wa siku itaficha ukweli na kusema yale yawapendezayo. Ila hiyo ndio picha halisi ya maadili ya viongozi wetu.
 
Bado kuna uongo ndani yake hapo,Polisi jamii bunduki wanatoa wapi?hiyo ya kula mke wa mtu inawezekana,maana maaskari na uhamisho wa mara kwa mara huwa hawajimuvuzishi na wake nae,wanakuwaga mene alone!
 
Kwa jinsi JF ilivyo, ukweli wote utajulikana tu, ni suala la muda tu. Inahitaji zaidi ya busara kwa jeshi la polisi kuhandle hii issue properly, vinginevyo litajivua nguo!! Subirini muone.

Mpaka sasa hawana nguo, wanatembea uchi wa mnyama, wamevua nguo zao kumvisha sisimwewe aka nyinyiem.
 
nadhani hii ni information ya uhakika... kuhusu polisi jamii wapo wengi sana mwanza..tena inaonekana vijana hao walitumia bunduki ya kamanda na kummaliza papo papo....ila ninachojiuliza kama kweli walitumwa why walimuacha huyo jike hai??
 
86 Reactions
Reply
Back
Top Bottom