DELETED ACCOUNT
JF-Expert Member
- Mar 25, 2010
- 9,805
- 15,470
Nitalielezea hili jambo kwa ufupi sana, mengine mtajalizia wenyewe. Nimeacha kuongelea sana soka la Tanzania maana wababaishaji ni wengi, kuanzia viongozi, wachezaji, wachambuzi na waandishi wa habari hadi mashabiki.
Kiufupi ni kwamba jezi za Simba zinazoenda kuzinduliwa J5 ni zile zile ambazo Simba ilivaa kipindi hiki cha pre-season.
Kabla haujaja na maneno, "oooh wameona wameharibu na jezi zilizovuja zimepondwa wakaamua kubadili gia", fahamu huu ndiyo ulikuwa mpango wa Simba toka mwanzo walipozindua zile jezi.
Ndiyo maana walizindua jezi tatu, home, away na third kit. Sasa jiulize pre-season unahitaji jezi zote hizo kwa ajili gani?
Kuna sababu kadhaa kwa nini waliamua kuzindua jezi mwanzoni mwa pre-season:
Keshokutwa watasema walisikia maoni ya watu wengi waliosema jezi zile zile za preseason ndiyo zitumike ila huo ndiyo ulikuwa mpango wa toka awali.

- Kupata muda wa kuzitangaza. Ingekuwa soko letu linaweza kudhibiti uuzaji wa jezi feki, kuzindua jezi kwenye pre-season na kuacha wachezaji pekee wavae kwa muda fulani ingekuwa ni mbinu bora sana ya kuzitangaza. Ila kwa soko letu, ni ngumu sana. Kwa hiyo unawaambia hizo ni za pre-season na unatoa onyo kali. Muda ukifika unazitoa kwa mashabiki.
- Kuepusha utengenezaji wa jezi feki. Kuendelea na point ya kwanza ila kwa upana zaidi. Kwa soko hili ambalo watu ndani ya masaa 24 wanaweza kutengeneza na kusambaza jezi feki, imagine unawapa mwezi mzima wajiandae kutengeneza jezi feki, si ni kujitengenezea bomu? Kwa kusema zile ni za pre-season na kuonya mtu asiyehusika asionekane amevaa mtaani, iliondoa uwezekano wa wahuni kuziingiza sokoni Ila wakati huo huo ameweza kuzitangaza machoni pa mashabiki wa Simba.
Keshokutwa watasema walisikia maoni ya watu wengi waliosema jezi zile zile za preseason ndiyo zitumike ila huo ndiyo ulikuwa mpango wa toka awali.