Ukweli kuhusu ishu ya Stephen Masele

Ukweli kuhusu ishu ya Stephen Masele

EINSTEIN112

JF-Expert Member
Joined
Oct 26, 2018
Posts
21,709
Reaction score
35,701
Kwa hisani ya Malisa GJ

Kwa wasioelewa yanayoendelea kuhusu Masele. Ni kwamba Masele ni Makamu wa kwanza Rais wa bunge la Afrika (PAP). Hivi karibuni ameingia kwenye mgogoro na Rais wa bunge hilo Bw.Roger Nkodo Dang raia wa Cameroon. Masele anamtuhumu Dang kwa ubadhirifu wa pesa za bunge hilo, hivyo ameunda kamati ya kumchunguza.

Dang amekasirishwa na uamuzi huo na anaona Masele anafanya mbinu za kumuondoa ili yeye akalie kiti cha Urais wa bunge hilo. Kwahiyo Dang ameamua kumng'oa Masele kwenye nafasi yake ili yeye aweze kuwa 'safe'.
_
Dang amempigia Spika Ndugai kumuomba amuite Masele nchini ili yeye aweze kusurvive. Na Spika Ndugai leo kwa jazba amemsimamisha Masele ubunge wake na kuagiza arudi nchini haraka kwa kile alichokiita mambo ya hovyo. Lengo la Spika ni kumuokoa Rais 'fisadi' wa bunge la Afrika, Roger Dang. Yani Ndugai anatumika kwenye mgogoro usiomhusu.

Leo Masele ameliambia bunge la Afrika kwamba hatarudi nchini kwa agizo la Spika kama alivyoamriwa. Amesema Waziri Mkuu Mhe.Kassim Majaliwa amemruhusu aendelee na shughuli zake za bunge la Afrika (PAP).
_
Amesema Rais wa bunge hilo Roger Nkodo Dang hataweza kumng'oa kwenye nafasi yake ya Umakamu wa Rais kwa sababu hakuteuliwa, bali alichaguliwa na wabunge wa bunge hilo. Amesema na kushangiliwa na wabunge hao.

Nafikiri mmeelewa sasa. Maana wengine mlishaanza kumuwazia jiwe.!
FB_IMG_1557992899035.jpeg
 
Amesema Rais wa bunge hilo Roger Nkodo Dang hataweza kumng'oa kwenye nafasi yake ya Umakamu wa Rais kwa sababu hakuteuliwa, bali alichaguliwa na wabunge wa bunge hilo. .....

Ngoja atandikwe BAKORA alafu tuone hiyo sentenso kama ina mashiko maana msingi wa yeye kuwa Makamu wa Rais wa PAP ume-originate from bunge la tanzania!
 
Maskini Ndugai hata watu wa nje wamemtambua ni wa jazba na ana mambo ya hovyo wameanza kumshirikisha kwenye mambo yao ya hovyo, nae kwa vile ni wa hovyo hajatambua anatumika hovyo na anaendelea kujipambanua ulimwenguni jinsi alivyo wa hovyo..
 
Hivi Cameroon si wanaongea zaid kifaransa kuliko Kingereza? Muda mwengne muwe mnamuelewa jaman
 
Waziri Mkuu na Spika Ndugai nani Mkubwa kwenye Issue za Wabunge na za Kibunge?

Serikali kuu imeanza kutoa miongozo ya Kibunge kwa Wabunge baada ya kuona Dish la Spika Lina Yumba
Kuna kitu sijaelewa, yaani mtanzania Job Ndugai ameamua kumhujumu mtanzania mwenzie ili kumtetea mkameruni katika bunge la Afrika?

Ana bifu gani hilo na Masele?

Yaani kwamba amehongwa na mkameruni? Spika wa bunge la Tanzania ana njaa kiasi cha kuhongwa na mtu wa nje ili kumhujumu mbunge mwenzie ili kumtetea mtu wa nje? Mkuu nakuamini haya mambo una uelewa nayo sana, wewe unahisi kuna nini hapa?
 
Ila Masere kapuuza amri ya Spika na kafuata ya Waziri Mkuu, jee Masere na Majaliwa watapelekwa kamati aliyopelekwa Prof Assad?
Kwa maelezo ya Spika ni kwamba aliyegonganisha mihimili ni Masele na ndiye anayetakiwa kuwajibika!
 
Ndugai kanyea Kambi we unasema Bandari ya Bagamoyo ni Bora kuliko stegler gorge.Upande wa Pili wamemchoka Huyo PM ni maelekezo ya Mzee Baba.Masele ataendelea kumnyoosha kwa mwogozo kutoka whitehouse Karibu na wavuvi.
 
Back
Top Bottom