Ukweli Kuhusu Edward Lowassa na Urais 2015

Ukweli Kuhusu Edward Lowassa na Urais 2015

Mbonica VJ

Member
Joined
Sep 27, 2012
Posts
76
Reaction score
43
Naipenda Nchi yangu Tanzania, Namwamini Edward Lowassa 2015 kwa haya tu inatosha mimi kumpatia kura yangu pamoja na familia yangu yote

1. Mwasisi na msimamizi wa Ujenzi shule za Kata zilijegwa jumla ya shule 2000 ndani ya miezi 6 tu ni kasoma leo watoto wa masikini wapo University .

2. Ujenzi wa Mradi mkubwa wa maji kutoka ziwa Victoria kwenda shinyanga, Tabora na Singida,

3. Kuvunja mkataba wa City water services bila kuogopa wa kuhofia chochote.

4. Kuzuia Uuzwaji wa shirika la Nyumba NHC,

5.Kuwaachia UVCCM kitega uchumi cha Jengo la maana

6. Alidhubutu kuchukua maamuzi magumu kwa masilai ya Tanzania na kulinda heshima ya CCM

7.Kuwafukuza wakurugenzi na wafanyakazi wa dhaifu serikali bila kuogopa chochote

8.Kuruhusu Bodaboda kuingia Nchini na kutengeneza Ajira za Kutosha kwa Vijana

9. Kuheshimu kanuni na taratibu zote za CCM

10. Kutekeleza ILANI ya chama chake na Kutimiza ahadi kwa asilimia 100% Jimboni kwake Monduli hivyo Nampendekeza Kuwa Rais wangu 2015.
 

Attachments

  • 1405254505154.jpg
    1405254505154.jpg
    20.4 KB · Views: 1,600
Naipenda Nchi yangu Tanzania, Namwamini Edward Lowassa 2015 kwa haya tu inatosha mimi kumpatia kura yangu na familia yangu pia

1. Mwasisi na msimamizi wa Ujenzi shule za Kata zilijegwa jumla ya shule 2000 ndani ya miezi 6 tu ni kasoma leo watoto wa masikini na walala hoi wapo University.

2. Ujenzi wa Mradi mkubwa wa maji kutoka ziwa Victoria kwenda shinyanga, Tabora na Singida,

3. Kuvunja mkataba wa City water services bila kuogopa wa kuhofia chochote.

4. Kuzuia Uuzwaji wa shirika la Nyumba NHC

5.Kuwaachia UVCCM kitega uchumi cha Jengo la maana

6. Alidhubutu kuchukua maamuzi magumu kwa masilai ya Tanzania na kulinda heshima ya CCM

7.Kuwafukuza wakurugenzi na wafanyakazi wa dhaifu serikali bila kuogopa chochote

8.Kuruhusu Bodaboda kuingia Nchini na kutengeneza Ajira za Kutosha kwa Vijana 9. Kuheshimu kanuni na taratibu zote za CCM

10. Kutekeleza ILANI ya chama chake na Kutimiza ahadi kwa asilimia 100% Jimboni kwake monduli hivyo Nampendekeza Kuwa Raisi wangu 2015.
 
Lowassa sio mwizi wamiliki wa Richmond wanajulikana na pia kampuni ya Richmond,ndo ile ya Dowans na sasa ni Symbion ambayo ilizinduliwa obama Kwa mbwembwe nyingi sana je Ufisadi wa Lowassa upo wapi hapo
 
Acha kutuongopea Monduli shida ya maji ni kubwa sana kuanzia monduli mjini hadi sehemu zingine kama vile Engutoto, dukabovu, loksale, lashaine, makuyuni, nanja n.k. halafu we unasema ametekeleza asilimia mia. Labda ufisadi ndo mia kwa mia.
 
Porojo zenu achenimpango mzima ni dr.W.P.slaa,hao wezi hatuwahitaji Tena,Tena tutawafilisi mali zote walizoiba.
Shule za kata kuna watu walifungwa kwakushindwa kulipa michango we unasifia wakati huo Wao wanaiba na kuficha uswisi kodi zetu.
Umeshawahi kujiuliza kwanini watoto Wa wakubwa hawasomi shule za kata?
Kwnini wasitunge sheria itakayowalazimisha watoto Wao kusoma shule za kata?
Kwanini viongozi wote Wa ccm wanarithisha watoto Wao nafasizao?
Hao waliosoma shule za kata lini watamewa hizo fursa wakati hawajasoma ng'ambo au shule nzuri?
Lowasa wiki iliyopita alienda kumtambulisha mwanae Monduli kuwa atakuwa mgombea Wa ubunge,yeye anaishi dar,monduli kuna watu wanafahamu mahitaji halisi ya watu Wao kuliko huyu kijana wa lowasa,lakini kwakuwa ni utamaduni Wa ccm kurithishana wanyonge hawana nafasi.
 
Lowassa sio fisadi, hizi ni propaganda za maadui zake ndani ya Chama, wanamuogopa sana. Wenye akili tunajua hali halisi.
 
Huyu Magamba si ndio wanampinga? Labda wanaogopa kasi yake. Kama anataka urais ajiengue ktk chama chake cha kifisadi..
 
Kuunyamazia ufisadi maana yake ni nini?
Pili hatupeleki wagonjwa ikulu ili baada ya miaka 3 tufanye Tena uchaguzi mwingine.Lowasa akikaa kunyanyuka mpaka asaidiwe kunyanyuka,anatetemeka mpaka anywe gongo ndo atleast,accentuation. Mzaha na watanzania baba.
 
Mkuu katiba mpya vipi
?

Ufisadi wa escrow account vipi?
 
Hizo sifa ulizoorodhesa ni za kweli alisimamia ila kwanini lowasa amekaa kimya kuhusu tuhuma za Richmond? Kwanini wapambe mnamsemea wakati yeye mwenyewe yupo Hai? Kama ni kweli anaogopewa CCM ndo maana wamemfanyia fitna kwanini asitumia nafasi hiyo ya kuogopewa akajiweka huru na hizi tuhuma mbele za Watanzania? Pia kuna tetesi wasiwasi kuhusu afya yake, vipi ataweza kumudu majukumu ya nchi? Pia msimamizi wa mwisho katika mchujo wa majina ya wagombea ni mwenyekiti wa Taifa wa chama je unadhani jina la Lowasa linaweza kurudi kupigiwa kura na mkutano mkuu wa Ccm na hatimaye kushinda fitina akapewa ilani ya chama?
 
Acha kutuongopea Monduli shida ya maji ni kubwa sana kuanzia monduli mjini hadi sehemu zingine kama vile Engutoto, dukabovu, loksale, lashaine, makuyuni, nanja n.k. halafu we unasema ametekeleza asilimia mia. Labda ufisadi ndo mia kwa mia.

Sasa hauoni kama ana sio Mbinafsi kama Maraisi wengine kwamba ameweza kupeleka Maji Mikoa ambayo sio kwao, kama Shy, MZ, TB, SgD n.k?
Yaani yuko kimaslahi ya Watz zaidi, siyo kwa kuwa tu anatoka Monduli basi lazima kwanza ipelekwe huko, na hiyo ndiyo sifa ya Kiongozi ambayo TZ hatujawahi kuwa naye, wote wanaangalia kwao kwanza!

 
Kama amefanya yote hayo si basi inatosha wacha wengine wachukue kijiti wasonge mbele.
 
Na kashfa ya udokozi ya RICHMOND je?


Hah hah hah,
Kwa taarifa yako hayo mambo muhimi 10 kwako aliyoyashughulikia mgombea wako si Chanzo cha matatizo ya watanzania.

Matatizo ya watanzania yanatokana Na ufisadi, wizi rasilimali zetu Na viongozi kugawia wageni rasilimali zetu Kama vile dhahabu, tanzanite, Gesi nk
 
J.K.Nyerere alisema,IKULU KUNA NINI?
kwa nini hizi sifa zisijitangaze zenyewe hadi kutumia nguvu nyingi sana.

Kila Kiongozi akisema ajitangaze aliyofanya kwa madaraka aliyopewa, Basi Magufuli angeonekana angalau amegusa maisha ya watu kwa kiasi fulani. Lakini yuko bize na ujenzi wa taifa. Huyu mkuu sijawahi kumsikia akitetea maslahi ya taifa bungeni tangu alipojiuzu. Kama taratibu za chama ziko wazi, sioni haja ya kuwa na wasiwasi kama mtu anafaa atapewa, kama hafai hata kama akipewa nchi kwa nguvu itamshinda.

Huu ni muda wa kijenga taifa na sio kutangaziana sifa za viongozi ambazo ni jitihada za watu wengi lakin zote apewe mtu mmoja. TAifa hili Bado liko nyuma sana kuanza kupoteza muda kujadili witu bila kufuata utaratibu.
 
Back
Top Bottom