Kati ya watanzania ambao ni ngumu kumuingia kwa hongo ni Mh Tundu LISSU ukiachlia mbali Dr Slaa na Mnyika!
Tundu LISSU ni aina ya binadam ambaye tokea maisha yake ameshajiapiza kutopokea wala kutoa Rushwa, huyu ni mtu ambaye anaamini zaidi katika midingi ya haki zaidi.
Kuna propaganda zinaenezwa kwamba eti Mh LISSU amepokea shi mil180 ili kukubali kumpokea Lowassa! Ningweza kusema kwamba kama vigingi vigumu kuviingia kwa Rushwa ni pamoja na Mh LISSU, Tuache kuudanganya umma kama mtu humfahamu LISSU ni bora ukae kimya tu! Hiki Kichwa nilishawahi kukaa nacho kimajukumu mbali mbali ya kijamii Namfaham vizuri huwezi kuniambia kitu juu yake.Ni mtu mwenye misimamo ya ajabu juu ya nadhiri zake, Naye ni binadamu ana madhaifu yake lakini kuja na propaganda eti amehongwa Mil 18 ni blaa blaa tu tusipende kuchafua watu kwa sababu zisizoeleweka!