Ukweli kuhusu Dr. Slaa

Ukweli kuhusu Dr. Slaa

tatizo mbowe ameweka pesa mbele

Ili tuwe Wazalendo wa kweli ktk nchi yetu hii Tanzania, tunapaswa tuwe wakweli.

Inaweza kuwa ni kweli kuwa mh. Mbowe akawa kapewa kweli pesa mnazomtuhumu, lkn kusema ukweli, hayupo mwenye ushahidi kwa hayo myasemayo au mnayomnenea huyo. Lkn najiuliza, mbona hatuongelei zile fedha zilizokamatwa kule Dodoma, kule Kilimanjaro, kule kwa Nape na sehemu nyingine nyingi zinazowahusu maccm?

Au ni kwa vile nadhani, uozo huo ukitendeka ndani ya ccm ni mafuta tena yenye harufu nzuri kwa wahusika; isipokuwa hata pale ambapo hatuna ushahidi ili mradi tu tumefikiria hivyo yakiwa nje yetu, ndo tunakuwa na ujasiri wa kusema tu tunavyoweza?

Tuweni wakweli hata yale tunayoyafanya sisi wenyewe, kama kweli tunachukia masuala yote ya rushwa?

Tena mbona hatuongelei zile ngumi tulizotwangana kila kona ya nchi wakati wa zoezi la kura za maoni lililofanyika trh 01/08/2015?

Poleni sana!
 

Taharuki imetanda juu ya wapi alipo Katibu mkuu wa Chadema Dr.Wilbroad Slaa. kila mtu anazungumza lake kwa kadri anavyoelewa. wengine wakisema yupo kwenye maandalizi ya vikao vya kamati kuu na wengine wakisema amejificha kwa sababu hakubaliani na maamuzi ya kumleta EL kwenye chama.

Mimi kama kada wa chadema wa muda mrefu na mwanasheria mzoefu nimefanya utafiti na nimejiridhisha bila shaka yoyote kuwa hali si shwari ndani ya chadema licha ya juhudi mbalimbali zinazofanywa kuonesha kuwa hakuna tatizo.

Ukweli ni upi? Ukweli ni kuwa Dr.Wilbroad Slaa hakubaliani na maamuzi yaliyofanywa na kamati kuu ya Kumleta EL na kumpa nafasi ya kugombea Urais bila kufanya utafiti wa kutosha. Slaa anadai kuwa maamuzi haya ni ya haraka mno na chama kilitakiwa kijitafakari zaidi kabla ya kumpa ridhaa ya kugombea Urais.

Ikumbukwe siku ya jumapili tar.26 wakati UKAWA wamefanya kikao cha mwisho na EL Dr.Slaa alikuwepo na baada ya hapo akapotea kabisa na hajaonekana hadharani hadi leo.


Ukweli ni kwamba ndani ya kikao kile chs jumapili Slaa alionesha msimamo wake juu ya EL na kudai kuwa watanzania hawatatuelewa wakituona tukipita kumsafisha mtu yuleyule tuliyemchafua awali.

Hivyo Slaa akatoa masharti mawili makubwa. La kwanza ni EL aitishe Press na ajisafishe mwenyewe kabla hajatangaza kuja UKAWA. Aruhusu waandishi wamuulize maswali yote kuhusu Richmond na kashfa nyingine ikiwemo umiliki wa jengo la Ubalozi wa S.Africa na EL ajibu hoja zote kwa maelezo ya kueleweka. Sharti la pili la Slaa ni kuwa EL asupewe nafasi ya kugombea urais kwa sasa kwani ni ngumu kupima dhamir yake kama ni ya kweli. Slaa akapendekeza EL aje CHADEMA na aisaidie UKAWA kuchukua dola bila kugombea Urais.

Lakini Mbowe akampinga sana Slaa na akasema Katibu mkuu hawezi kuweka "ultimutum" ya EL kujiunga na chadema. Mbowe akapuuza mawazo ya Slaa na akaagiza mchakato wa kumpokea uanze mara moja na kesho yake Mbatia akaambiwa atoe tamko la kumkaribisha EL UKAWA.

Hali hii ilimfanya Slaa kujihisi mnyonge na aliyepuuzwa. akahisi hathaminiki ndani ya chama licha ya mchango mkubwa alioutoa kukijenga chadema. jambo la ajabu Mbowe alipopelekewa taarifa hizo alijibu kwa kejeli kuwa liwalo na liwe. yani yuko tayari kumpoteza Slaa na kumkumbatia EL.

Haikujulikana wazi Mbowe ana maslahi gani katika hili la EL na kwanini aamue kuwa na msimamo mkali hivyo wa kumtetea EL.

Inadaiwa tangu jumapili Slaa alipoachana na viongozi wenzie wa UKAWA hadi sasa yupo ndani hajatoka na hakuna mgeni anayeruhusiwa kumuona. Anautumia muda huu kusali na kushauriana na marafiki zake kwa njia ya simu (wengi ni maaskofu) juu ya nini afanye katika kipindi hiki.

Wengi wamemshauri aachane na siasa na ajiuzulu nafasi yake ya SG ndani ya chadema wazo ambalo limeungwa mkono na mkewe Josephine na baadhi ya watu wenye misimamo mikali.

Baada ya ushauri huu mkewe wa Slaa ameonekana kufurahia na ameanza kuelezea kwenye mitandao ya kijamii. Jsna kupitia kundi la Nyakahoja la whatsapp Josephine alisema mumewe ameteseka sana na chama hiki na amekitoa mbali sana. Dr.Slaa alivunjika mkono na hadi sasa ana ulemavu wa kudumu kwa sababu ya kuitetea chadema. yeye mwenyewe alipigwa na kuharibiwa mimba mwaka 2011 kwa sababu ya chadema halafu leo wanapuuzwa kama vile si chochote ndani ya chama.

Anasema ni afadhali Mbowe angesikiliza ushauri wa Slaa wa EL kujisafisha kwanza kabla hajaja chadema maana kuja bila kujisafisha ni kuwaweka viongozi wote wa chadema kwenye mtego.

Madai ya Mbowe kupewa fedha na EL. Yapo madai kuwa Mbowe amehongwa sh. bil 12 ili kumpokea EL. Fedha hizi ameziweka kwenye akaunti yake binafsi na amewawia kidogo wale aliowaona wanaweza kumchallenge. baadhi ya watu waliopata mgao ni wajumbe wa kamati kuu ili kuwaziba mdomo. na si wajumbe wote bali wale wachache viherehere. baadhi yao ni Godbless Lema (anadaiwa kupokea milioni 120), Peter Msigwa (mil 135), Tundu Lissu (mil 180), Salum Mwalimu (Mil 180).

Pesa hizi ndizo zinazodaiwa kuwafumba macho kamati kuu na kuamua kumpitisha EL bila kufikiri mara mbili. Kitu cha ajabu kamati kuu imefunga dirisha la kuchukua fomu na kusema eti kamati kuu inamuunga mkono Lowassa tu.

Huu ni ujinga ambao hata CCM haiwezi kuufanya. Kamati kuu inatakiwa kuwa neutral. kamati kuu haitakiwi kuwa na mgombea. kamati kuu haitakiwi kuzuia watu kuchuku fomu. acha wachukue wengi kadri iwezekanavyo halafu wachujwe abaki mmoja.

Kama EL anajiamini yeye ni bora zaidi na ana nguvu zaidi kwanini anaitumia kamati kuu kuzuia watu wasichukue fomu? Siku chache zilizopita watu walilalamikia kamati kuu ya CCM kuwa ilikua na mgombea wake mbona hawaoni hili la kamati kuu ya chadema?

Ikiwa madai haya ya kuhongwa kamati kuu ni ya kweli basi chadema inaelekea ukingoni katika siasa za nchi hii. jambo la ajabu viongozi wanaodaiwa kuhongwa akiwemo Mbowe hawajakanusha habari hizi. halafu wanatuma ujumbe kw Slaa eti wakamsihi asiondoke. wajumbe wote waliotumwa wakaishia getini na hawakufunguliwa mlango. mlitegemea mfunguliwe mlango wakati kuna madai mmehongwa na hamjakanusha? kanusheni kwanza ndio muende kumuona Slaa. Au mnataka mkamhonge na yeye? Kama msipokanusha habari hizo mkienda mtafungiwa tena nje maana nyumbani kwa Slaa hakitaingia chochote kilicho kichafu.

Response ya Chadema. ni kama vile hawajali yanayoendelea. na bahati mbaya zaidi vijana wa chadema wameanzisha movement ya kumtukana Josephine kuwa yeye ndio anamponza mumewe. kwenye mtandao wa jamiiforums, facebook ma magroup ya whatsapp wanamtukana sana.

kwenye group moja la wabunge wa chadema wameanzisha movement iitwayo "Josephine Bring Back our Dr". wengine wanamwita mwanamke mpumbavu, wengine wanasema ana hasira ya kukosa ufirst lady, lakini wengine wamefika mbali na kudai anatumiwa na TISS na CCM.

Kimsingi madai yote hapo juu hayana mashiko. Josephine hatumiwi na TISS wala CCM. Hana uchungu wa kukosa ufirst lady wala nini. anachofanya ni kutetea haki ya mumewe. haki ya kuthaminiwa, haki ya kuheshimiwa, haki ya kutoa mawazo yake na kusikilizwa.

Hivi mumeo anapuuzwa kwenye vikao vikubwa vya maamuzi halafu unaambiwa waliompuuza wamehongwa fedha na hawajakanusha habari hizo, halafu ukimtetea mumeo unaambiwa unatumika na TISS. this is ridiculous.

Hakuna cha TISS wala CCM mchawi wa chadema ni chadema wenyewe na mchawi wa ukawa ni chadema. Hizi porojo za TISS ni mbinu inayotumika ili Slaa akiamua kutangaza msimamo wake ionekane anatumiwa na CCM. Chadema acheni siasa za kitoto. hivi Slaa aliyepigania chadema zaidi ya miaka 20 akitoa sadaka maisha yake kwenu ndio wa kutumika na TISS leo aache kutumika huyo EL aliyekuja jana? this is very interesting. chadema kitaingia katika rekodi za dunia za kuwa chama cha kwanza kumtilia shaka mwanachama wake wa miaka 20 na kumuamini mwanachama wa siku moja.

Nini kifanyike? Jambo linaloweza kufanyika na kusaidia kuiokoa chadema na UKAWA kwa ujumla ni mediation. zitafutwe mbinu nzuri za kukutana na Slaa na kuongea nae. aeleze yanayomhusu na chama kioneshe concern ya kuyatatua.

pia kwa kuwa Josephine anaonekana kuwa na nguvu kubwa sana kwa Slaa hivi sasa ni bora Watafutwe wanawake wenye heshima ndani ya chama wakaongee nae. kwa mfano Mama Regina Lowassa, mama Ntagazwa na mama Mbatia waende kumuona mwanamke mwenzao waongee nae. hii itasaidia kupunguza hasira za huyu mama maana tangu juzi anatukanwa mitandaoni akidaiwa ndiye anayemzuia Slaa.

Ni vizuri mambo haya yafanyike mapema maana taarifa zilizopo ni kuwa kufikia wiki ijayo kama chama kitakua hakijatoa msimamo kuhusu Slaa basi yeye atatangaza msimamo wake wa kujiuzulu wadhifa wake chadema na kuamua kuachana na siasa kabisa. kisa wataondoka nchini yeye na familia yake kwenda Italia ambapo ataishi huko kwa miaka mitano kabla ya kurudi nchini na kumalizia maisha yake Karatu. mipango ya Slaa kwenda kuishi Italia kwa miaka mitano inaratibiwa na shirika mija la kiroho la kanisa katoliki na maandalizi yanaendelea vizuri.

Hivyo basi ni vema kazi hii ikafanywa mapema na kwa umakini ili tusivuruge kazi yote ya kuijenga Ukawa na kuujenga upinzani nchini. ukweli ni kuwa Slaa akiamua kujiuzulu siasa za upinzani zitapoteza uelekeo na tutashindwa vibaya kwenye uchaguzi mkuu kuanzia udiwani, ubunge hata urais. maana yake ni kuwa kazi yote iliyofanyika kuujenga upinzani inabomolewa siku moja na kuifanya CCM izidi kushamiri. na ikiwa Slaa ataondoka itachukua miska zaidi ya 100 kupata upinzani mwingine wenye nguvu kama huu. hivyo basi juhudi za haraka zinatakiwa.

Mwandishi wa makala haya ni ndugu A.N Chilongola, mwanachama wa chadema na mkurugenzi wa kampuni ya uwakili ya Chilongola &Advocates iliyopo Mabibo
Dar.anchilongola@gmail.com
Mwandishi wa makala hii ni mwongo sana! Kaandika sanaaaa mwishowe anajifanya kutoa ushauri kwa CHADEMA! Kama hamjui watu wanaotumika kijanja ni pamoja na huyu mwandishi, Anaandika kwa kuponda na kulalama sana eti mwishowe anajifanya ana uchungu na CHADEMA! Kweli?
Mbona kuandika kote huku pamoja na yeye kua mwanachama wa CHADEMA hatuoneshi chanzo cha kuaminika cha taarifa zake? Hivi ni mtu unahitaji kua na akili ya namna gani ili kutambua kua huyu mwandishi anatumiwa?
Katika kitu kilichonisikitisha sana sana ni kusema hadi "TUNDU LISSU naye amehongwa mil 180" LISSU naye ni binadamu ana madhaifu yake lakini ni kati ya watu Wagumu sana kuhongeka Tanzania hii ukimwacha Dr Slaa na Mnyika.Nimjuavyo LISSU mimi kote nilikokua naye karibu na hata kwenye majukumu ni binadamu aliyekwisha kujiapia hawezi kupokea wala kutoa hongo katika maisha yake yote.Ya Mbowe, Msigwa, Lema na Salim Mwalimu siyajui lakini kwa LISSU tungeni uongo mwingine hata kama ni kweli kuna sintofahamu juu ya CHADEMA na Dr Slaa.
 
Tatizo mfumo wa chama na sio huyo mama wa watu acheni siasa za kitoto, hili lilionwa mwanzo na watu kama kina Chaha Wangwe RIP, ZZK na Kitila Mkumbo lakini wapenda ushabiki walifumbwa macho na kuamini yanayotolewa na viongozi. Wenye uweledi walijua kuwa kilichomponza ZZK kilikuwa ni kuutaka uenyekiti (hii kutokana na baadhi ya makala na tetesi nyingi zilizoenea humu JF na nje ya JF) Watu walikuwa wanalalamika ila kwakuwa mlikuwa vipofu hamkuona na kwakuwa mlikuwa viziwi hamkusikia.

Ikiwa Dr alishiriki kumtoa ZZK alietumikia CDM tangu uchanga wake kisiasa mpaka anafukuzwa basi pengine kilichotokea dhidi yake ni malipo ya hapa hapa duniani. Wanachama na wasio kuwa wanachama wa CDM wanajua alikotokea ZZK na wanajua alikotokea Dr kabla ya kuingia CDM na ndio wanatakiwa watulie wachambue kwa kina hii sinema maana hii sijui ni episode ya ngapi.

All in all kwa mara nyingine tena upinzani na UKAWA kwa ujumla unatiliwa mashaka na Watanzania lukuki wenye kura zisizofungamana na vyama. Hii nafasi haitakuja tena.

NOTE***

Haina tija yoyote ndani ya CDM/UKAWA wala ndani ya CCM na jamii nzima kwa ujumla kukebehiana kwa maneno ya karaha na mipasho. Huu sio ustaarabu wa Kitanzania na wala sio siasa. Siasa ni hoja na hoja hujibiwa na hoja. Itakuwa vizuri kuweka hoja kuliko kusema maneno ya karaha kama badilikeni mnatia aibu.


Umeongea kwa hekima na busara sana mdau humu kuna ushabiki sana ambao hata haueleweki mwanzo wake na mwisho wake sijui tumerogwa na nani
 
‎HABARI‬ DR. SLAA AMEPEWA LIKIZO IKISHA ATAUNGANA NA CHADEMA - MBOWE
Katika mkutano wa Baraza kuu la CHADEMA unaoendelea hivi sasa, Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman MBOWE amesema hakuna ugomvi na Dk. SLAA, amepewa likizo na ikiisha ataungana nao baadaye ili shughuli za Chama ziendelee.
Mbowe- Tumekubaliana Dr SLAA apumzike kwa muda na atakapokuwa tayari ataungana nasi mbele ya safari
Mbowe- Chama hiki hatukiendeshi kwa siri, tunakiendesha kwa mikakati.
Mbowe- Tulilazimika kutumia kila mbinu halali ambayo inakiwezesha chama chetu kusaka matumaini na matarajio ya wananchi.
Mbowe- Tuliridhika pasipo shaka kwamba ugeni wa Edward Lowassa katika chama chetu ni mpango wa Mungu.
Mbowe- Umoja wetu ndio ushindi, fursa iliyojitokeza ni nadra.
Mbowe- Mtikisiko huu umekuja kwa CCM kipindi ambacho Watanzania wanamatamanio ya mabadiliko
Mbowe- Hatuwezi kuwa chama cha kuendelea kuhubiri mabaya ya jana tukashindwa kuhubiri maendeleo ya kesho
Mbowe- Kipigo wanachopata CCM, hawajawahi kukipata tangu tuanze siasa za vyama vingi
Mbowe- Kila tunayeweza kumpokea kutoka vyama vilivyo nje ya UKAWA tutamchukua
Mbowe- Mungu ameamua kutumia chama chetu kujeruhi na kuangusha CCM.
Mbowe- CHADEMA ni chama cha siasa, ni chama makini, chama makinI ni chama cha watu, chama kisichokuwa makini ni chama cha viongozi.
 
msichokijua wengi ni kuwa slaani mkatoliki na siasaza ccm ni kuubeba ukatoliki no matter what haya yanayotokea kwa slaa si bahati mbaya kwa vile magufuli pia mkatoliki lazima atumiwe slaa kupunguza nguvu na kura za wapinzani na ikiwezekana edo ashindwe ili wakatoiki watawale ndio maana anaandaliwa safari ya Italy akatumikie kanisa lake at the sametime aitie damage chadema ishindwe ili mkatoliki ashinde
 
Mfa maji tu amna lolote mtakoma ata dr slaa akijiengua bado ukawa utasimama vizuri lowasa anakubalika sana
 
Umeongea kwa hekima na busara sana mdau humu kuna ushabiki sana ambao hata haueleweki mwanzo wake na mwisho wake sijui tumerogwa na nani

No one will really understand politics until they understand that politicians are not trying to solve our problems. They are trying to solve their own problems of which getting elected and re-elected are number one and number two. Whatever is number three is far behind.

At that point then we will stand as one and demand manifest know our rights what they are going to do for us ila kwa siasa hii ya kupenda watu nachelea kusema safari hata kuanza haijaanza ni kama tunavuta shuka kulala vizuri wakati kumeshakucha.
 
wazo la el kujisafisha naliunga mkono. lkn km kweli anakipenda chama na taifa y ajitoe???? kuna ubaya gan el akigombea? as long as hata yy alitoka ccm na akapewa nafac agombee. ooooh siasa. upuuuz mtupu..... nampenda sla bt kura yangu kwa ukawa ipo palepale. wananch tushakubaliana na hiyo hali viongoz msituvuruge. i wish slaa angekua mgombea mwenza.


Inasikitisha kuona sisi wananchi wa kawaida kabisa tumemwelewa Mh Lowasa alivyoelezea kwa undani sakata la Richmond na mhusika wake mkuu lakini kiongozi mkubwa wa CDM kama Dr. Slaa unakuwa huelewi. Dr Slaa ili uitendee haki CHADEMA na UKAWA ni vema utulie kwenye chama mpaka uchaguzi mkuu upite ndipo uchukue hatua ya kuachana na siasa kama ni kweli una nia hiyo. Kiukweli katika uchaguzi huu ujao Dr Slaa hauna nguvu kisiasa ya kumshinda Magufuli kwenye uchaguzi ujao. Ukweli ndio huo. Na CHADEMA na UKAWA wameshachoka kushindwa katika kila chaguzi tangu mfumo wa vyama vingi uingie nchini 1992. Kumpata EL ndani ya CHADEMA na UKAWA kipindi hiki is a golden chance that might never come twice. Tushirikiane na EL kuiondoa CCM madarakani. By mwananchi wa kawaida sana Ester John
 
Tulieni maccm dawa iwaingie mtanyoka tuu mwaka huu mnajitahidi kumuongerea dr slaa ana wahusu nini ata akiama yeye ni mungu kwetu
 
msichokijua wengi ni kuwa slaani mkatoliki na siasaza ccm ni kuubeba ukatoliki no matter what haya yanayotokea kwa slaa si bahati mbaya kwa vile magufuli pia mkatoliki lazima atumiwe slaa kupunguza nguvu na kura za wapinzani na ikiwezekana edo ashindwe ili wakatoiki watawale ndio maana anaandaliwa safari ya Italy akatumikie kanisa lake at the sametime aitie damage chadema ishindwe ili mkatoliki ashinde

Angalia unayoongea yasije kugeuka majuto. Usipende kuongea maneno ya vibarazani utaombwa ushahidi halafu itakula kwako. #cyberCrimeLaw
 
duh yAn mbowe kafanya hv?yan chama kimekuwa kama mali yake au taasis yake.namiunga mkono mzee slaa ana busara huwez lamba matapishi kumbuka cku za nyuma lowasa ndo ilikuwa sera ya cdm leo unaongea nn na amejisafisha nn? kifup hata cdm kupokea na kuwa hadhi ya kugombea tena ubunge udiwan wale walio shindwa ccm haifai sabb waliopiga kura za maon ccm ndo asilimia kubwa watakao piga kura ktk uchaguz mkuu.tatu iweje watu wamejenga chama chao miaka 20 leo aje mtu kwa cku mbil achukue chama kirahis tu.
 
No one will really understand politics until they understand that politicians are not trying to solve our problems. They are trying to solve their own problems of which getting elected and re-elected are number one and number two. Whatever is number three is far behind.

At that point then we will stand as one and demand manifest know our rights what they are going to do for us ila kwa siasa hii ya kupenda watu nachelea kusema safari hata kuanza haijaanza ni kama tunavuta shuka kulala vizuri wakati kumeshakucha.

True muddy
 
''Josephine hatumiwi na TISS wala CCM. Hana uchungu wa kukosa ufirst lady wala nini''
''
Hivi mumeo anapuuzwa kwenye vikao vikubwa vya maamuzi halafu unaambiwa waliompuuza wamehongwa.....''
''
hii itasaidia kupunguza hasira za huyu mama''

Quotes from a learned Brother!!


Slaa ana conflict of interest kwenye maamuzi yake ya ama kumpokea au kutompokea Lowasa chadema, kwakuwa Slaa anataka yeye awe ndo mgombea urais
 
Siasa za mwaka huu zina shida sana yaani kila mtu anakuwa mchambuzi wa mambo ya kisiasa

Haya ngoja tuone
 
mkuu kwanza heshima yako ... mkuu naomba nikuulize baadhi ya maswali hv unavyoona kati ya ukawa na lowassa nani anamuitaji mwenzie sana? pili unavyoona ni mwanachama gani aliejiunga na chama flan kwa kuonga hela ndo ajiunge tatu nani mwenye ushahidi wa kusema lowassa ni mchafu kiasi kwamba kujiunga na vyama vingine mpaka atumie pesa

kingine mbona watanzania mmekuwa mabingwa wa kukariri yani mmekuwa kama meli hata iwe kubwa kama kisiwa inavutwa na ki targ boat chenye ukubwa wa center ya tani 3 ni miaka 8 toka habari ya lowassa kuwa ni fisadi bt cjawahi kuona mwandishi yeyote wa habari za kiuchunguzi kuingia chimbo na ku investigate newz hii naamini hata vyombo vikubwa vya habari duniani wangeinunua habari hii japo kuna magazeti zaid ya 10 ya habari za kiuchunguzi bt na wao pia wapo kama mama wa nyumbani anae msubili mumewe arudi nyumbani ndo wapakue chakula watoto wapate kula tumekuwa tunasubili pakuche tukanunue magazeti kana kwamba magazeti ni bible na msaafu kwamba ni maneno ya mungu so yatakuwa ni ukweli mtupu wakati tofauti ya magazeti haya na magazeti ya udaku ni ya udaku yanatoka kwa wiki haya yanatoka kila siku kumbuka chadema inataka watu kushinda uchaguzi na lowassa tayali anawatu sasa hapo nani anamuitaji mwenzie mpaka fedha imtoke kwa kupata kadi ya chadema ?
cdhani kama kuna mpuuzi yeyote duniani anaweza kutoa fedha wakati ujui kama utashinda uchaguzi watu wanatoa fedha wapate kazi coz anajua akitoa atapata kazi kiwepesi si ktk uchaguzi na kama kuna mtu wa namna hiyo huyo anatakiwa kuwepo mental institutions si mtaani

Tukitumia theory yako maana yake Tanzania hakuna Ufisadi na Chadema wafunge Midomo yao kwa Kuwa Tenant wenu Lowassa kishasema kama una Ushahidi wa Rushwa au Ufisadi nenda Mahakamani (sio) kupost au kuandika humu otherwise kaa kimya tena kutumia neno (Shut up).
 
Binadamu bwana majizi hayaoni lowasa tu escrow lowasa anahusika? Alijiudhulu na ufisadi kama kawaida bomba la gas mtwara dar ambalo lina ufisadi wa kutisha lowasa anahusika acheni kujifanya mnajua kumbe ni mazuzu mbona hamthibitishi ufisadi wake swala la richmond ameongea na wahusika mnawajua lkn mmetia pamba masikioni kama hamjui nani mhusika dhuluma rushwa ndiyo mwongozo wenu ameamua kuhama mwacheni mzee wa watu,
 
Msomi wakili,unataka kutuaminisha kuwa kila msimamo wa Dr Slaa,lazima uwe sahihi? wajumbe wengine wasisikilizwe kwakuwa Mawazo ya Dr hayana kasoro?!! sio aquement za kisomi hizo.pia kumbuka swala la kupata mgombea wa UKAWA na CDM linatakiwa lifanywe haraka sio la kusubiri ili atambulishwe kwa wananchi, Rating ya LOWASA ktk nafasi ya Uraisi kwa tafiti za nyuma ipo juu,rejea walio mdhamini majuzi,ukilinganisha na Dr Slaa. Wote ni muhimu lkn LOWASA ni muhimu zaidi ndo maana hata Ukawa members wengine wamekubaliana apitishwe,is Dr Slaa genius that all opposition power house? Personally idont believe that.Siasa ni ushawishi,sio ultimatum
 
Back
Top Bottom